Mwanamke: Muwindaji hachagui pori bali huchagua aina ya mnyama amtakaye ...!

Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,328
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,328 280

Mitoko (Dating) kwa wanawake wengi ni kama vile kwenda kununua Ice Cream. Kila mara mwanamke anajaribu aina tofauti ya Ice Cream ili kuangalia ni ipi yenye ladha nzuri itakayomvutia. Nyingine yaweza kuwa inavutia kwa nje lakini baada ya kuijaribu anakuja kugundua kwamba haina ladha aliyokuwa unaitarajia, nyingine inaweza kuwa haina mvuto kwa nje lakini baada ya kuijaribu anagundua kwamba ni nzuri na ina ladha aipendayo na hivyo inakuwa ndiyo chaguo lake la kila mara apatapo hamu ya kula Ice Cream.

Hivyo ndiyo ilivyo kwa baadhi ya wanawake, pale wanapokuwa katika harakati za kuwinda ili kumpata mwanaume sahihi wa kufunga naye pingu za maisha. Siku hizi si ajabu kukuta mwanamke anakuwa na mitoko na wanaume tofauti tofauti ikiwa ni katika kujipa nafasi ya kufanya uchaguzi sahihi wa mwanaume wa maisha yake.Ukweli ni kwamba si vibaya kwa mwanamke kuwa na mitoko na wanaume tofauti tofauti ili mradi tu isiwe ni zaidi ya mtoko. Kutoka na mwanaume kwa ajili ya kupata chakula cha mchana au cha usiku au hata kama ni kwa kupata vinywaji au kahawa haimaanishi kwamba tayari mmeshakuwa na uhusiano, bali inafungua ukurasa wa kufahamiana ili kila mmoja kumpima mwenzake kulingana na vigezo alivyojiwekea kwa mpenzi amtakaye.

Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba, si vibaya kwa mwanamke kuwa na mitoko na wanaume tofauti tofauti kwa sababu kuwa na mtoko na mwanaume haimaanishi kwamba ndio mmeshakuwa wapenzi, kwani hata huyo mwanaume unayetoka naye inawezekana na yeye pia anatoka na wanawake tofauti tofauti katika kutafuta yule atakayemfaa, kwa hiyo hilo siyo jambo la ajabu.Wapo baadhi ya wanawake wakishakuwa na mtoko na mwanaume mmoja basi hufunga milango kabisa na kukataa mitoko na wanaume wengine kwa hofu kwamba yule mwanaume aliyetoka naye awali akijua anaweza kumuona kama hana msimamo. Kama mwanamke ni mkweli wa nafsi na ameweka msimamo wake mapema kwa huyo mwanaume aliyeomba mtoko naye, ni lazima ataheshimu makubaliano.

Ukweli ni kwamba kung’ang’ania mtoko na mwanaume mmoja mara kwa mara hutengeneza mazingira ya kutamaniana kimwili na hapo ndipo utakuta mwanaume anatumia nafasi hiyo kutaka zaidi ya mlivyokubaliana na mwishowe mwanamke anajikuta ameingia katika hatua ya kukutana kimwili kabla hajajiridhisha kuhusu tabia na mwenendo wa mwanaume huyo.Hata hivyo ningependa kutahadharisha, wapo baadhi ya wanawake ambao wanaweza kuwa na mtoko na wanaume tofauti tofauti, lakini kwa bahati mbaya wengi huangalia zaidi uwezo kiuchumi wa kila mwanaume anayetoka naye badala ya kutumia nafasi hiyo kumjua mwanaume huyo kiundani kuhusu tabia na mwennedo wake katika uhusiano.

Kwa muktadha huo unaweza kukuta mwanamke anakuwa na orodha ndefu ya wanaume aliowahi kuwa na mtoko nao na kila akijaribu kumpima kila mmoja kulingana na kigezo cha uwezo wa kiuchumi na atakayeweza kumtimizia mahitaji yake yote anakuta hakuna hata mmoja, anajikuta amepoteza muda wake mwingi na hakuna alichaoambulia.Unaweza kumkuta mwanamke anakuwa na mtoko na mwanaume lakini kichwani amebeba orodha ya sifa za mwanaume amtakaye, hivyo katika mazungumzo yake na mwanaume huyo bila kujijua anakuwa kama vile anahakiki orodha yake ili kujua kama mwanaume huyo atafaulu vigezo vyake. Kwa hiyo atakuwa anawekea alama zake kichwani kulingana na kila sifa aliyojipangia na mwisho wa siku anamtosa huyo mwanaume kwa sababu hajafikia viwango alivyojiwekea.Tatizo ninaloliona kwa wanawake wengi ni kwamba, wanaume wenye sifa wanazozitaka hawajawahi kuwepo hapa duniani, na ndio maana hupoteza muda mwingi wakicheza mchezo wa kupapasa kama vile wanachagua embe. Inahitaji muda wa kutosha ili kumjua mtu vizuri zaidi na kama mwanamke akiutumia muda wake vizuri na kwa uhuru bila kusukumwa hakika atapata matokeo mazuri, lakini akisubiri mpaka machweo halafu jamii ikaanza kumnyooshea vidole ikijiuliza ana kasoro gani mpaka umri huo hajaolewa atajikuta anaolewa na yeyote kwa sababu ya kuogopa kunangwa na jamii.
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,724
Likes
3,408
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,724 3,408 280
Hata hivyo ningependa kutahadharisha, wapo baadhi ya wanawake ambao wanaweza kuwa na mtoko na wanaume tofauti tofauti, lakini kwa bahati mbaya wengi huangalia zaidi uwezo kiuchumi wa kila mwanaume anayetoka naye badala ya kutumia nafasi hiyo kumjua mwanaume huyo kiundani kuhusu tabia na mwenendo wake katika uhusiano.
Wa namna hii wapo wengi sana mkuu...
 
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
23,829
Likes
675
Points
280
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
23,829 675 280
kwa kifupi unatushauri tuwe na mitoko na wanaume tofauti tofauti? nani anagharamia hiyo mitoko sasa? lol
 
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Messages
5,554
Likes
193
Points
145
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined May 8, 2013
5,554 193 145
^^
Tamaduni za ulaya zinashika upesi akilini mwetu kuliko zetu.
Enzi zetu ulikuwa ukimtaka mwanamke unatupa fimbo mbele yake akiiokota umekubali,asipoiokota ndo basi wewe si chaguo lake,sasa izi dating dating!
^^
 
Heaven on Earth

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2013
Messages
37,147
Likes
5,606
Points
280
Heaven on Earth

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2013
37,147 5,606 280
Kuna ukweli kabisa..kweli we ni Mtambuzi

kwa experience yangu kuna kundi naangukia humo ndani
 
Last edited by a moderator:
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
23,829
Likes
675
Points
280
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
23,829 675 280
^^
Tamaduni za ulaya zinashika upesi akilini mwetu kuliko zetu.
Enzi zetu ulikuwa ukimtaka mwanamke unatupa fimbo mbele yake akiiokota umekubali,asipoiokota ndo basi wewe si chaguo lake,sasa izi dating dating!
^^
mmmh! wewe ni kibabu?
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,902
Likes
10,122
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,902 10,122 280
to every action there is an equal and opposite reaction,HATA SISI WANAUME KWA MINAJILI HIYO BASI TUNA RUHUSA YA KUONJA TASTE MBALIMBALI ILI KUONA YUPI ANAFAA KUTUNZA YUMBA YAKO
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,686
Likes
3,643
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,686 3,643 280
Mtambuzi leo umeleta mada nzuri sana ila inahitaj kwanza kunyumbuliwa manake kwa upeo wangu wa kizee naona ina vijimada vidogodogo kama vinne hivi ama vitatu

kwanza nianze
dating......mitoko, mitoko kwa kileo imekuwa na maana tofauti tofauti kulingana na aina ya mtu na mzingira yake.
wapo ambao kwao mitoko ni hobby huyu hutoka for funny na hana kitu kingine nyuma yake, binti kama huyu watu huweza kumhesabia kuwa na hatia ama kuwa na orodha kubwa ya mitoka lkn ukweli ni kwamba yeye hana kitu nyuma ya dating hizi bali tu ni sehem ya hobby yake. binti wa aina hii naomba nisimzungumzie manake ni mada pana kidogo.

dating kwa ajili ya selection mitoko hii mara nyingi huambatana na aina tofauti tofauti za watu. binti hapa hutaka kutoka na wanaume hata wa4 ili tu aweze kuchagua yupi ni the best kulingana na aina ya mtu amtakaye. hii nayo huwa ni mtihan na fumbo gumu sana kwa binti as sio mara zote unaweza kupatia ama kufumbua kitendawili chake all in all lazima achaguliwe mmoja ili maisha yasonge mbele

sehem ya pili ambayo nimeona inahitaj clarification ni ukweli kuhusu wanawake kujifungia baada ya first date........... ukweli ni kwamba mabinti wengi huwa wako innocent sana na wanaogopa kuitwa majina mabaya kama malaya nk hali hii humfanya mtu akitoka na mtu siku ya kwanza hata kama nafsini bado hajakaa vizuri basi huassume bwana ee nitajifunza taratibu kumpenda.........mwisho wa siku sasa unakuta kijana yy naye alikuwa anawinda na anakuja kukutana na mzuri zaid ana mwacha solemba huyu wa awali.

binti anachotakiwa kujifunza hapa dating sio kufanya ngono na siku zote mtoko wa kujuana haukulazimish kukubali kufanya ngono hivyo basi hukatazwi kuwa na mitoko na watu tofauti ili kuweza ku explore zaid aina gani ya mwanaume unaye mtaka.

usikubali mtoko wako ukawa kamba ya kukufunga, make it an open loop ili kwamba wewe huru kutoka na mtu mwingine kwa nia hiyo hiyo ya kumjua na yeye awe na uhuru wa kutoka na mtu mwingine kwa nia sawa na yako. usiweke terms na conditions kwenye mitoko yako bali nenda ukiwa na checklist ya criteria uzitakazo na ujiwekee kabisa nafasi kwamba huwez kukutana na malaika so atakaye mzidi mwenzie kwa vitu flan flan naweza nika define terms na condition kwake.

hukatazwi kueka criteria nyingi uwezavyo ili pia uwe na wigo mpana wa kumpata mtu anaye meet interest zako kwa asilimia kubwa manake nim wazi hakunaga mwanaume malaika useme utampata yule haswaa m,wenye kila utakacho wewe.

nimeandika sana mambo mengine mawili nitamalizia baadae.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,686
Likes
3,643
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,686 3,643 280
to every action there is an equal and opposite reaction,HATA SISI WANAUME KWA MINAJILI HIYO BASI TUNA RUHUSA YA KUONJA TASTE MBALIMBALI ILI KUONA YUPI ANAFAA KUTUNZA YUMBA YAKO
hivi ng yangau mwekundu kwani date ni kulana tunda??
 
Last edited by a moderator:
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,902
Likes
10,122
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,902 10,122 280
Halafu wanawake wengi wa Ki TZ kama ulivyochambua wanatumia fursa hiyo kujua una miliki nini na nini na mfuko wako umetoboka kiasi gani,sisi ma badboy tunakwepa hilo ili tusije kuumbuka bure.......yaani mtoko wa kwanza huohuo najipanga nampige pombe akishtuka .......!!anaamka the day after tomorrow ghetto kitanda cha kamba ameshaliwa !!
 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,153
Likes
1,595
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,153 1,595 280

Ukweli ni kwamba si vibaya kwa mwanamke kuwa na mitoko na wanaume tofauti tofauti ili mradi tu isiwe ni zaidi ya mtoko. Kutoka na mwanaume kwa ajili ya kupata chakula cha mchana au cha usiku au hata kama ni kwa kupata vinywaji au kahawa haimaanishi kwamba tayari mmeshakuwa na uhusiano, bali inafungua ukurasa wa kufahamiana ili kila mmoja kumpima mwenzake kulingana na vigezo alivyojiwekea kwa mpenzi amtakaye.

Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba, si vibaya kwa mwanamke kuwa na mitoko na wanaume tofauti tofauti kwa sababu kuwa na mtoko na mwanaume haimaanishi kwamba ndio mmeshakuwa wapenzi
, kwani hata huyo mwanaume unayetoka naye inawezekana na yeye pia anatoka na wanawake tofauti tofauti katika kutafuta yule atakayemfaa, kwa hiyo hilo siyo jambo la ajabu.
.
Asante kwa uzi mzuri Baba Ngina, hasa nilipokolea rangi nyekundu umenitouch screen!!!!!!
 
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
20,902
Likes
10,122
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
20,902 10,122 280
hivi ng yangau mwekundu kwani date ni kulana tunda??
MSILETE UZUNGU HAPA DATE MAANA YAKE NI "KUVIZIANA KULANA TUNDA" take it from me.........ukileta uzungu kwenye hili wanaume wenyewe hawa wa kibongo utakua unalia kila siku,yaani ukizubaa tu unaliwa siku hiyohiyo!!teh teh teh #TEAMUKWELIMTUPU
 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,153
Likes
1,595
Points
280
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,153 1,595 280
Mtambuzi leo umeleta mada nzuri sana ila inahitaj kwanza kunyumbuliwa manake kwa upeo wangu wa kizee naona ina vijimada vidogodogo kama vinne hivi ama vitatu

kwanza nianze
dating......mitoko, mitoko kwa kileo imekuwa na maana tofauti tofauti kulingana na aina ya mtu na mzingira yake.
wapo ambao kwao mitoko ni hobby huyu hutoka for funny na hana kitu kingine nyuma yake, binti kama huyu watu huweza kumhesabia kuwa na hatia ama kuwa na orodha kubwa ya mitoka lkn ukweli ni kwamba yeye hana kitu nyuma ya dating hizi bali tu ni sehem ya hobby yake. binti wa aina hii naomba nisimzungumzie manake ni mada pana kidogo.

dating kwa ajili ya selection mitoko hii mara nyingi huambatana na aina tofauti tofauti za watu. binti hapa hutaka kutoka na wanaume hata wa4 ili tu aweze kuchagua yupi ni the best kulingana na aina ya mtu amtakaye. hii nayo huwa ni mtihan na fumbo gumu sana kwa binti as sio mara zote unaweza kupatia ama kufumbua kitendawili chake all in all lazima achaguliwe mmoja ili maisha yasonge mbele

sehem ya pili ambayo nimeona inahitaj clarification ni ukweli kuhusu wanawake kujifungia baada ya first date........... ukweli ni kwamba mabinti wengi huwa wako innocent sana na wanaogopa kuitwa majina mabaya kama malaya nk hali hii humfanya mtu akitoka na mtu siku ya kwanza hata kama nafsini bado hajakaa vizuri basi huassume bwana ee nitajifunza taratibu kumpenda.........mwisho wa siku sasa unakuta kijana yy naye alikuwa anawinda na anakuja kukutana na mzuri zaid ana mwacha solemba huyu wa awali.

binti anachotakiwa kujifunza hapa dating sio kufanya ngono na siku zote mtoko wa kujuana haukulazimish kukubali kufanya ngono hivyo basi hukatazwi kuwa na mitoko na watu tofauti ili kuweza ku explore zaid aina gani ya mwanaume unaye mtaka
.

usikubali mtoko wako ukawa kamba ya kukufunga, make it an open loop ili kwamba wewe huru kutoka na mtu mwingine kwa nia hiyo hiyo ya kumjua na yeye awe na uhuru wa kutoka na mtu mwingine kwa nia sawa na yako. usiweke terms na conditions kwenye mitoko yako bali nenda ukiwa na checklist ya criteria uzitakazo na ujiwekee kabisa nafasi kwamba huwez kukutana na malaika so atakaye mzidi mwenzie kwa vitu flan flan naweza nika define terms na condition kwake.

hukatazwi kueka criteria nyingi uwezavyo ili pia uwe na wigo mpana wa kumpata mtu anaye meet interest zako kwa asilimia kubwa manake nim wazi hakunaga mwanaume malaika useme utampata yule haswaa m,wenye kila utakacho wewe.

nimeandika sana mambo mengine mawili nitamalizia baadae.
Well said dada mkubwa!!! Mekupendajeeeeeee........ Watu wengi huwa hawalitambui hili, kwamba ukitoka na Arushaone kesho ukatoka na PakaJimmy unakuwa katika selection zako. Wanaona kama hujatulia hivi, kumbe uliyetoka naye hana vile vigezo unavyotaka.

Wacha niendelee na mitoko ipo siku nitakutana naye!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,686
Likes
3,643
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,686 3,643 280

Tatizo ninaloliona kwa wanawake wengi ni kwamba, wanaume wenye sifa wanazozitaka hawajawahi kuwepo hapa duniani, na ndio maana hupoteza muda mwingi wakicheza mchezo wa kupapasa kama vile wanachagua embe. Inahitaji muda wa kutosha ili kumjua mtu vizuri zaidi na kama mwanamke akiutumia muda wake vizuri na kwa uhuru bila kusukumwa hakika atapata matokeo mazuri, lakini akisubiri mpaka machweo halafu jamii ikaanza kumnyooshea vidole ikijiuliza ana kasoro gani mpaka umri huo hajaolewa atajikuta anaolewa na yeyote kwa sababu ya kuogopa kunangwa na jamii.
hapa Mtambuzi ndipo shida kubwa ilipo lkn kuna jambo moja kubwa ambalo watu tunasahau .
binti ama kijana kabla ya kweneda kwenye mambo ya ndani yaani kuangalia huyu mtu anaweza kunipa raha nk angalia kwanza wasifi wake wa nje na wa ndani.

kwa asilimiam kubwa kila kijana ana matamanio ya aina fulan ya mtu anayemtaka awe mwenzi wake katika kila criteria ambayo kijana anaitoa lazima aangalie je ina umuhimu kiasi gani na je kama ikikosekana itamtesa kiasi gani. nasema hivyo kwasababu wapo vijana wengine unakuta kiukweli kabisa anataman kuwa na mwanamke mweupe mnene hasa wasukuma sasa mtu kama huyu ukimwambia aish na mwanamke mweusi mwembamba unamtesa na utamfanya aish kwa kujilaumu period.........

lakin sasa yupo kijana mwingine yeye hajali wasifu wa nje yaani uzuri yeye wale wa shoo rum hatak kabisa lkn ana vitu vya ndani zaid anavyo angalia kama vile utum wema, ukarimu, ucheshi, usafi, upendo wa dhati, etc

Sasa hapa kuna swala gumu ambalo ni lazima kijana awe na mitoka isopungua 4-5 ili aweze kumpata yule ambaye ana maksi za afadhali katika zile anazotaka yy. Hapa hatujaongela swala la ngono naongelea ule wasifu wa nje na ndani ila maswala ya kitandani haya nayapa nafasi ndogo sana as yanafundishika iwepo upendo wa kweli upo kati ya wawili hawa.
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,686
Likes
3,643
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,686 3,643 280
MSILETE UZUNGU HAPA DATE MAANA YAKE NI "KUVIZIANA KULANA TUNDA" take it from me.........ukileta uzungu kwenye hili wanaume wenyewe hawa wa kibongo utakua unalia kila siku,yaani ukizubaa tu unaliwa siku hiyohiyo!!teh teh teh #TEAMUKWELIMTUPU
kama unalazimisha sawa na siwez kukupinga abadan.
mitoko kama mitoko haina mahusiano ya kufanya ngono na take it from me. ila tu kwa vijana wa kileo sikatai kama mtaihalalishia upande huo.
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,798
Likes
125,794
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,798 125,794 280
Mmh Labda, pengine ni kweli
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,686
Likes
3,643
Points
280
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,686 3,643 280
Well said dada mkubwa!!! Mekupendajeeeeeee........ Watu wengi huwa hawalitambui hili, kwamba ukitoka na Arushaone kesho ukatoka na PakaJimmy unakuwa katika selection zako. Wanaona kama hujatulia hivi, kumbe uliyetoka naye hana vile vigezo unavyotaka.

Wacha niendelee na mitoko ipo siku nitakutana naye!!!!!!!
asante mdogo wangu..........
kutoka na mtu sio kufanya ngono bhana............manake kama ndivyo basi utajikuta mtu unafanya ngono kila siku na watu wa kila aina.

kwa binti kama ww jipe nafasi uchague ila uwe na akili usiwe too selective usije ukapata koroma..........muda mwingine mwenye half better ni mzuri zaid kuliko mwenye 3/4
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
351
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 351 180
Well said dada mkubwa!!! Mekupendajeeeeeee........ Watu wengi huwa hawalitambui hili, kwamba ukitoka na Arushaone kesho ukatoka na PakaJimmy unakuwa katika selection zako. Wanaona kama hujatulia hivi, kumbe uliyetoka naye hana vile vigezo unavyotaka.

Wacha niendelee na mitoko ipo siku nitakutana naye!!!!!!!
Selection tunafanya kimoyomoyo bana!...Unamchunguza mtu akiwa hajui kitu! Mimi nikisikia jana ulikuwa na Arushaone, halafu leo uko na mimi, nakumwaga wallahi!...UTAJARIBU wangapi?
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,252,184
Members 482,034
Posts 29,799,499