figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,484
Mwanamke mmoja Siwema Alex miaka (36) mkazi wa kata ya Magomeni wilaya Kilosa mkoani wa Morogoro amekufa papo hapo baada ya nyumba yao waliokuwa wakiishi kuangukiwa na mti kufuatia mvua iliyo ambatana na upepo mkali huku mumewe na watoto watatu wakinusurika katika ajali hiyo.
Nisauti za vilio na majonzi vilivyo tawala baada ya marehemu huyo kutolewa katika kifusi cha nyumba baada ya kuangukiwa na mti ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamesma marehemu huyo alikuwa akipika ndani kisha mti ukaangukia nyumba hiyo ndipo umauti ulipo mkuta mama huyo.
Nae kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kilosa dokta Dicksoni Masele amekiri kupokea mwili wa mwanamke huyo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kilosa.
Chanzo: ITV