Mwanamke mmoja amwagiwa maji ya moto na mwanamke mwenzie kisa wivu wa kimapenzi...!

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281

Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Na Gadiola Emanuel -Arusha

Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.Neema Teti-Majeruhi
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali
nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini
Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo.Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa
 
Maskini keshakoma...aisee mkome sometymz...mume anauma mbayaa
 
Pole yake ila mbona dushelele zipo nyingi ugomvi wa nini
 
nani ameruhusu picha hyo ya mwisho,sidhani kama mgonjwa aliombwa na kuruhusu
 
Wanawake wengi wa choyo wanapenda wamiliki wenyewe dushelele
 
Du,na yeye alipata wapi guts za kwenda kwa mke wa jamaa?yeye hakustuka?mke wa jamaa anamwita akakae na watotonaona moyoni alifurahi,kumbe cha moto kinakuja
 
Aliyewachezea akili yeye ataendelea kupeta wakati mmoja ataishia jela na ngozi ndio hivyo tena.

Kweli hasira hasara!
 
Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Na Gadiola Emanuel -Arusha

Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.Neema Teti-Majeruhi
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali
nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini
Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo.Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa

Nashindwa kufahamu unyanyasaji wa kijinsia unamaanisha nini? Nikifikiri kuwa jinsia huzungumzwa pale panapotokea matokeo ya watu wa jisia tofauti?
 
Back
Top Bottom