Mwanamke mmbeya....

Ni wimbo tu..sijui kama kuna uhusiano wowote.
Ngoja wahusika waje kukujibu wenyewe!
 
aisee... haya bhana, imekugusa??
walaaaaa, sema naona hapa huwezi kupata jibu sababu hatukuona context na mwenyewe hayupo. ila pale pale ungemquote, unapigilia rangi ya bluu na unamuuliza hapa una maana gani? Ila kuanzisha thread ili tuchangie kumsema mwenyewe naona kama ni a bit too excessive. unless awe amekukera sana...
 
RR... fuatilia hiyo yu tyube ndio uelewe... i asked coz kuna mdada humo kwenye nyimbo anaua midomo myeusi
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Ahahahaaaa....Mwanne Othman kiboko yao aisee! Hivi bado ana-host kipindi cha rusha roho C2C?

Hilo la mwanamke mmbea kuwa na midomo myeusi kaa kunguru nadhani lilikuwa dongo kwa Baby J. Si unajua kuna beef kati ya Offside Trick na AT. Sasa Offside Trick walimshirikisha Baby J kwenye wimbo wao wa Kidudu mtu. Baby J ana midomo myeusi ndiyo maana nahisi kuwa hilo dongo lilirushwa kwake.

AT alipojibu naye ndo akamshirikisha Mwanne. Huyu mdada ni noumer! Kuna mstari anakwambia "mnajua kuchumu lakini mnanuka midomo". Madongo yake hunichekesha sana.

Sasa mtu ukitaka uuelewe vizuri Vifuu Tundu sikiliza kwanza Kidudu Mtu ya Offside Trick. Ukimaliza ndo usikilize na Vifuu Tundu. Ukimaliza kusikiliza Vifuu Tundu sikiliza Dege ya hao hao Offside Trick safari hii wakimshirikisha Hammer Q. Nadhani Dege ni jibu la Vifuu Tundu. Namsubiri AT naye aijibu Dege.

Haya mambo ya mduara, chakacha, na taarab hapa ndo mwake bana. Penda sana mimi hizo genres!
 
Hilo la mwanamke mmbea kuwa na midomo myeusi kaa kunguru nadhani lilikuwa dongo kwa Baby J. Si unajua kuna beef kati ya Offside Trick na AT. Sasa Offside Trick walimshirikisha Baby J kwenye wimbo wao wa Kidudu mtu.

AT alipojibu naye ndo akamshirikisha Mwanne. Huyu mdada ni noumer! Kuna mstari anakwambia "mnajua kuchumu lakini mnanuka midomo". Madongo yake hunichekesha sana.

Sasa mtu ukitaka uuelewe vizuri Vifuu Tundu sikiliza kwanza Kidudu Mtu ya Offside Trick. Ukimaliza ndo usikilize na Vifuu Tundu. Ukimaliza kusikiliza Vifuu Tundu sikiliza Dege ya hao hao Offside Trick safari hii wakimshirikisha Hammer Q. Nadhani Dege ni jibu la Vifuu Tundu. Namsubiri AT naye aijibu Dege.

Haya mambo ya mduara, chakacha, na taarab hapa ndo mwake bana. Penda sana mimi hizo genres!
SALUTE NN, mchezo umeuelewa khaswaaa, ila naskia wale offside trick mashoga!!!

kuna sehemu anasema siingii mlipotoka
 
Hiyo ya wao kuwa mashoga sijui na sina uhakika maana inaweza ikawa ni dongo tu. Si unajua tena mambo ya mabeef. Mtu unasema chochote tu ili kumkera na kumuudhi hasimu wako.

Mstari unaouzingumzia wewe ni huu "hodi hodi naingia, nazirejesha salamu, mlango walopitia, kupita mimi kharamu"

Sasa hata wao Offside Trick kwenye kidudu walirusha madongo ambayo yanaweza kutafsiriwa kuwa AT naye ni shoga. Na ukisikiliza Dege pia waweza pata picha kuwa AT naye ni shoga.

Binafsi sidhani kama hao wote ni mashoga. Offside Trick na AT wameshirikiana kwenye nyimbo kadhaa halafu baadaye ndo wakaja kufarakana. Wewe mwenyewe si unaona hata hapa JF mtu akimkasirisha mwenzake tu tusi la kwanza ni kumwita huyo mwenzake shoga. Je, hiyo inamaanisha kweli huyo aliyeitwa hivyo ni shoga? La hasha!
 
WanaMMU leo mnisamehe... nikiwa kwenye browsing ziszo na maana nikakutana na semi moja inasema "utamjua mwanamke mmbeya - midomo ya ke myeusiiiiiiii"

Hawa jamaa huwa wanafikiria nini??

na mwanaumme mwenye midomo miyeusi tii kama mimi yukoje?

watu waache kujitungia mambo ambayo hayana uhusiano hata chembe.....................
 
Usitafute sana mantiki kwenye madongo ya mirindimo ya pwani. Rusha roho siyo Reggae bana! Rusha roho ni madongo na mipasho tu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
NN bro nimekukubali kaka yabgu duh mpaka naanza kuwa mpenz wa hizo makitu! Aksante sana

Habari za J'mosi dadangu?

Asikwambie mtu bana...mirindimo ya Pwani ndo yenyewe. Mimi ninaipenda sana na wala siogopi wala kuona aibu kukiri hivyo.

Karibu ukaribie kwenye jahazi la wapenzi wa hayo mavituz.
 
Ahahahaaaa....Mwanne Othman kiboko yao aisee! Hivi bado ana-host kipindi cha rusha roho C2C?

Hilo la mwanamke mmbea kuwa na midomo myeusi kaa kunguru nadhani lilikuwa dongo kwa Baby J. Si unajua kuna beef kati ya Offside Trick na AT. Sasa Offside Trick walimshirikisha Baby J kwenye wimbo wao wa Kidudu mtu. Baby J ana midomo myeusi ndiyo maana nahisi kuwa hilo dongo lilirushwa kwake.

AT alipojibu naye ndo akamshirikisha Mwanne. Huyu mdada ni noumer! Kuna mstari anakwambia "mnajua kuchumu lakini mnanuka midomo". Madongo yake hunichekesha sana.

Sasa mtu ukitaka uuelewe vizuri Vifuu Tundu sikiliza kwanza Kidudu Mtu ya Offside Trick. Ukimaliza ndo usikilize na Vifuu Tundu. Ukimaliza kusikiliza Vifuu Tundu sikiliza Dege ya hao hao Offside Trick safari hii wakimshirikisha Hammer Q. Nadhani Dege ni jibu la Vifuu Tundu. Namsubiri AT naye aijibu Dege.

Haya mambo ya mduara, chakacha, na taarab hapa ndo mwake bana. Penda sana mimi hizo genres!

Kumbe wapo kwenye majibizano nlikuwa sielewi......... mi mwenyewe huu wimbo unaniacha hoi sana na mistari yake,
Ila ndo mambo ya pwani bila madongo na mafumbo wimbo haujaingia sokoni,
 
Ile kitu ni noma yule kijana ni mkali mjibuni basi bwana wenu mnajifanya wakali wa hizi kazi au wakali wa mashuzi ni sehemu ya maneno ya wimbo
 
na mwanaumme mwenye midomo miyeusi tii kama mimi yukoje?

watu waache kujitungia mambo ambayo hayana uhusiano hata chembe.....................
mwanaume watasema anavuta sigara....

Mkuu mirindimo ya pwani ina messages usizoweza kuzipata mahala popote...
 
Ahahahaaaa....Mwanne Othman kiboko yao aisee! Hivi bado ana-host kipindi cha rusha roho C2C?

Hilo la mwanamke mmbea kuwa na midomo myeusi kaa kunguru nadhani lilikuwa dongo kwa Baby J. Si unajua kuna beef kati ya Offside Trick na AT. Sasa Offside Trick walimshirikisha Baby J kwenye wimbo wao wa Kidudu mtu. Baby J ana midomo myeusi ndiyo maana nahisi kuwa hilo dongo lilirushwa kwake.

AT alipojibu naye ndo akamshirikisha Mwanne. Huyu mdada ni noumer! Kuna mstari anakwambia "mnajua kuchumu lakini mnanuka midomo". Madongo yake hunichekesha sana.

Sasa mtu ukitaka uuelewe vizuri Vifuu Tundu sikiliza kwanza Kidudu Mtu ya Offside Trick. Ukimaliza ndo usikilize na Vifuu Tundu. Ukimaliza kusikiliza Vifuu Tundu sikiliza Dege ya hao hao Offside Trick safari hii wakimshirikisha Hammer Q. Nadhani Dege ni jibu la Vifuu Tundu. Namsubiri AT naye aijibu Dege.

Haya mambo ya mduara, chakacha, na taarab hapa ndo mwake bana. Penda sana mimi hizo genres!

Burudika mkuu...
Off Side Trick Ft Baby J- Kidudu Mtu - YouTube
Offside Trick ft Hammer Q Dege - YouTube
 
Back
Top Bottom