Mwanamke kumuita boyfriend mume

Jeanclaude

JF-Expert Member
Aug 30, 2013
259
237
Ni halali kwa wanawake kuwachukulia wapenzi wao kama waume wa ndoa ilihali hata uchumba bado? Nimeshuhudia marafiki zangu wawili waliokuwa na tabia hiyo na walipoachika wakakata tamaa utadhani wamepewa talaka. Wanawake msijiaminishe kihivyo mtaumia bure..
 
Kwani tatizo nini? Kwani wamevunja sheria ya nchi? Si mapenzi yao binafsi?
 
Na haya majina ya BABY yafutike basi maana sio kweli ni watoto!
 
Kuachwa kunauma wewe haijalishi unaitwa mke,mchumba ,girlfriend wala pass tym..
Kuachwa ni kuachwa tu...

Mh ila mtu anaachikaje iwapo si mke au mume.
 
Kwani tatizo nini? Kwani wamevunja sheria ya nchi? Si mapenzi yao binafsi?

Hakuna tatizo kisheria labda kimaadili iwe kwa misingi yoyote ile, ni sahihi kujibebesha majukumu ya kuwa mke ungali bado kwenye hatua ya urafiki?
 
acha mambo yako,wengne tunapata na tunajisikia raha sana kuitwa hivyo,pia acha kukalili kua mwanaume ni yule anaefunga ndoa kanisan
 
Ni halali kwa wanawake kuwachukulia wapenzi wao kama waume wa ndoa ilihali hata uchumba bado? Nimeshuhudia marafiki zangu wawili waliokuwa na tabia hiyo na walipoachika wakakata tamaa utadhani wamepewa talaka. Wanawake msijiaminishe kihivyo mtaumia bure..

Kweli aisee. Yani wengine wanabweteka tu utadhani ndoa kesho wakati sie tunakuwa tupo kwenye mchakato
 
hehehehe! wangu anapenda nimuite hivo madai anakuwa anahisi uwepo wangu pembeni yake.. teheeee! kumbe wengine hampendi?
 
Ni halali kwa wanawake kuwachukulia wapenzi wao kama waume wa ndoa ilihali hata uchumba bado? Nimeshuhudia marafiki zangu wawili waliokuwa na tabia hiyo na walipoachika wakakata tamaa utadhani wamepewa talaka. Wanawake msijiaminishe kihivyo mtaumia bure..

mkiitwa majina mazuri mwalalama,
subiri uitwe kibuzi ndo utafurahi na roho yako!!
 
Wanapenda wenyewe!!!!

baby.jpg
 
Back
Top Bottom