Mwanamke kumleta nyumbani mwanaume waliosoma nae, hii imekaaje?

Unatulia tu mkuu baada ya wiki nawe unaleta mwanamke uliye soma naye akutembelee weekend mshinde mle na lunch nyumbani then unamsindikiza jioni yake!
Ni kweli anakulazimisha uamini kitu na wewe unamuonyesha kwa vitendo kwamba umeamini hivyo .Akikuuliza ni kwa nini na wewe utamuuliza hivyo hivyo yaani tamu sana hii kitu.
 
kawaida tu sema umeshawazakuwa anakucheat nooo yawezekana kaja kumringishia sehemu anayokaa ilivyonzuri na alivyo na familia nzuri wanawake tuna mengi vichwani mwetu acha tu

sio hilo tu ukute alimtenda wakati wanasoma sasa Leo mdada kaolewa na gentleman, in short successful man sasa ndo anamkaribisha homeeee njo uone ya mungu yalivyomengi ahaaaaa

Mimi siwezi kufanya hivyo ila mashoga zangu nitawakomesha nikiolewa ndo maana napenda mwanaume msafiiii yani akitoka lazima wadada waangaike hii lazima niitimize.

ahaaa kuna shoga yangu M ananisubiri Kwa hamu eti siku nikiolewa lazima aje kushuhudia huyo Mme atakavyokuwa anavaa ahaaaa maisha haya bana.
 
Mimi alinikaribisha wakanipokea na mumewe na nikalala kwao. Mumewe naye ni rafiki yangu zaidi ya classmate. Mimi ni Me.
 
Mpaka anakuletea huyo aliyesoma nae.. mlishazoeana vibaya zamani sana... umleavyo ndivyo akuavyo...
 
Si unamkadiria tu kama unamuweza unampa kipigo cha fumanizi, yaani vitasa vya kufa mtu, hatorudia tena kukanyaga kwako
 
Hii imekaaje mkeo kumleta mtu waliosoma nae mwanaume nyumbani kwako alafu unafika nyumbani anakutambulisha huyu nimesoma nae.

Kama ni wewe unalipokeaje alafu ni usiku na anmshindikiza wewe upo ndani itakua kwenye hali gani na utafanyaje.
Huyo jamaa kagonga, au anagonga au atagonga mkeo, hutaki acha!! Si ajabu mkeo nae kaenda ghetto kwake.
Fanya unachotakiwa kufanya.
 
Iliwah kutokea hiyo,nilikutana na bint nilosoma naye ambaye ameshaolewa, akanielekeza kwake, kisha akanambia TWENDE KWANGU UKAPAONE. Binafs nilimkatalia na alijitahidi kunisisitiza twende nikakataa.Kwahyo hakufanikiwa.Sababu nilikuwa nazo.
1.Yule ni mke wa mtu, huwez kujua mume atalichukuliaje lile jambo.Na kwa mfumo dume tulionao MWANAMKE akimleta MWANAUME aliyesoma nae huwa na tafsiri mbaya kama mdau aliyeleta mada alivyowaza
2.Huwa sipendi ukaribu na wake za watu hata kama huyo mwanamke nilikuwa na uhusiano nae akishaolewa basi ndo nafunga milango
 
Back
Top Bottom