Mwanamke kukuzidi uchumi/kupambana ni sababu ya kukataa kuhusiana naye?

livewise1

JF-Expert Member
May 25, 2019
837
952
Hehee [manake apo kwanza ncheke]

Nimekutana na mwanamke niliepotezana nae tangu mwaka 2007 kwa kuwa kila mtu alienda kusoma sehemu tofauti.

Nimekutana nae yuko vizuri kiutaftaji na anajiweza.

Tumesalimiana kisha akaniambia "Nimekuwa nakutafta sana hata katika mitandao ya kijamii bila mafanikio"

Akasema bado ananihitaji tufunge ndoa na yale mapenzi ya tangu zamani bado yanaendelea moyoni mwake siku zote.
Akanipeleka anapoishi na kuniambia mipango yake na hatua alizopiga na future zake, nikasema huyu kipindi kile haya mawazo chanya hakuwa nayo, saivi anaenieleza mipango hata mimi sijawahi waza haya mmh, lazima kuna mtu nyuma yake.

Nikamuuliza kuhusu maisha yake ya kimahusiano akasema kwa sasa ni single mother mumewe alikimbia majukumu kipindi wapo apeche alolo, walipata mtoto akawa na chengamoto za kiafya mume akatoroka.

Baada ya mwaka na nusu mume akamletea talaka, kisha akaondoka zake mkoa.

Baadae bibie akaanzisha biashara na dadaake mpaka sasa ndio wanapambana, ila ni parefu mno walipo maana wanauza mpaka nje ya TZ.

Wiki tatu nyuma alikuja sister wake akamtambulisha kwangu kuwa sisi ni marafiki wa mda mrefu, baadae alipoindoka sister wake akamtumia meseji "MDOGO WANGU KAMA HUYO JAMAA ATAKUBALI BORA AKUOWE UPATE MJI MA WEWE UONGEZE FAMILIA NA UPATE UTULIVU" akanionesha hiyo sms, akisema unaona hata sister ananipa support.

Akaniahidi kunipa support katika biashara kwa kuniongeza mtaji ambao utakuwa mara 4 ya huu nilionao kama labda nitahitaji.

Kwa kweli sina jibu maana nahisi nguvu ya uchumi na ile kupambana kwake kunizidi naona kama nakosa sifa ya kuwa mumewe!

Naona bora nikatae ili nisije kuishi bila amani ndani japo nampenda alivyo smart na namna alivyo kimaumbile sio haba.

Kama sina nguvu kubwa ya uchumi maamuzi mengi ya mwisho hayatatoka kwangu maana nitakuwa marioo flani hivi, lakini pia muda mwingi yupo kwenye mihangaiko mwishowe nije kum cheat bure wakati mimi sinaga hizo tabia.

Hii habari ni ya ukweli, japo muhusika ni ndugu yangu na sio mimi.

Nauliza swali kwa enzi hizi tunazoishi kweli nguvu ya uchumi tu ndio ifanye ushindwe kumpokea mwanamke?

Nawasilisha!!!
 
Wanawake wengi wa siku hizi wanahela na hawajui wapi kwa kuzipeleka au wafanyie nini.

Mkuu huyo mwanamke ni mission in town Kama na wewe ni mtu wa type hiyo kubali Ila Kama ni wale wazee wa kanisa achana nae mtazinguana tu.
 
Hapo tunaita win-win situation. 1. Singo maza anatafuta heshima kwenye jamii kwa kuolewa

2. Kijana marioo anatafuta mtaji wa kuosha jina hapa mjini

My take, sidhani kama hapo kuna mapenzi, in the future huyo dem lazma atamdharau jamaa kwa sababu atakua anaona ye ndo kamweka mjini, na ukitegemea mtaji ni mara 4, lazma atakua anajitahidi kuucontrol maana kawekeza. Huyo jamaa kama yuko JF tunamngojea na nyuzi nyingi za mafadhaiko.

Ushaur wa bure, aache ujinga. Kama walishindwana huko kitambo, bora apambane na hali yake atafte mtu waanze chini watafute mali, lakini mwanaume kupewa lifti lazma utangazwe
 
Mkuu hela ya mwanamke ni ya masimango always..hata kama unamuona anakupenda vipi,,
Unaweza usinielewe leo but One day and one time,,, in a one way or the Other utaelewa ninachozungumza.... Fucck it..



JIFUNZE KUJITEGEMEA....
 
Back
Top Bottom