Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Karibuni sana tena Wazee wa Conspiracy Theories kwenye uwanja mwingine wa kujifunza masuala ya Mwanadamu kwa mtazamo wa kidunia. Najua humu kuna watu wana dini zao, so nitawaomba tuache pembeni imani zetu ili tuyafikirie haya wayasemayo Watafiti wenzetu katika Nchi za mbele.
Vyanzo mbalimbali vimekuwa vikitoa sababu mbalimbali zinazodai kuwa, changamoto zinazomkabili binadamu kulinganisha na viumbe wengine waliomo duniani, ni uthibitisho wa kipekee kuwa, asili ya binadamu siyo Dunia hii.
Baadhi ya hoja zinazotolewa kuonyesha kuwa, binadamu alitoka nje ya Dunia hii ni:
- Ukubwa wa vichwa vya watoto wachanga.
- Kuunguzwa na miale ya jua.
- Binadamu kuumwa umwa hovyo ni dalili hafurahii mazingira ya Dunia.
- Migongo kukaa vibaya na kutoendana na gravity.
- Kujihisi kuwa, hapa duniani siko nyumbani.
Humans do NOT come from Earth - and sunburn, bad backs and pain during labour prove it, expert claims | Daily Mail Online
Update:
Natumai mods watarekebisha title isomeke: Mwanamke kujifungua kwa tabu kutokana na ukubwa wa kichwa cha mtoto kulinganisha na wanyama wengine: Je, asili ya Binadamu siyo Dunia hii?