Mwanamke kufukua makaburi bila sababu inatokana na nini?

Kuandika Uzi wa mapenzi asubuhi subuhi haimaanishi kwamba hatujengi Taifa. LAA!

Muhali gani wapendwa? Nawaombea muwe na afya njema.

Ni swali fupi tu
JE NINI KINAFANYA MTU KUFUKUA MAKABURI (MAMBO MAOVU) YA ZAIDI YA MIAKA MIWILI NYUMA?

Mpenzi wangu na mama mtoto wangu ambaye yuko mbali na mimi kwa sasa, Jana tulijikuta katika malumbano makubwa baada ya yeye kuanza kuniuliza kuhusu mambo flani mabaya ambayo niliyafanya Miaka ya nyuma.

Jambo lenyewe ni kwamba alinikuta na dalili na nyaraka zote zinazoonesha kuchepuka. (Nilikataa kata kata ingawa ilikuwa kweli)

Lakini mambo yalikwenda na yakaisha kwa amani na upendo ukaendelea.

Ajabu ni kwamba jana baada ya kukosa cha kuzungumza akaanza kunikumbusha yale mambo. Na sio kunikumbusha tu bali alijipanikisha baada ya kukumbuka lile tukio kana kwamba limetokea sasa hivi.

Nikamuuliza kwani mbona masuala yalishaisha? Au Kuna nini tena ?

Nikaona huku sasa ni kuzoeana vibaya. Nikaanza kumfokea na kuanza kujibizana hadi usiku mkubwa. Nikampiga biti na kumwambia kwamba KAMA UMECHOKA KUWA NA MIMI JIKATAE MAPEMA KUNGUNI WEE!

NIKABAKI NA MASWALI HAYA!

1. Hisia zake zimempotosha kwamba kwa sasa nachepuka kwa sababu niko mbali naye?

2. Amepata baharia mpiga makasia sasa ananikumbusha kwamba anauliza?

3. Amenichoka?
4. Kuyumba kwa uchumi kumempagawisha?
5. Mabadiliko ya hormone kwa kuwa ana muda mrefu hajafanya mapenzi? (Kwa MUJIBU WA imani yangu)

6. Amechoshwa na kasumba zangu

Au nini shida?

NB
Sharauti sana kwa wanangu wote mlio oa ama kuishi na Mwanamke kwa muda mrefu.
Si tulishawaambia MSIOE?
Mbona nyie viumbe huwa HAMSIKII?

Pambana tu na hali yako.

#YNWA
 
Sisi Wanawake ni wagumu sana kusahau matukio yanapokuwa yametuumiza kiasi kikubwa. Tunasamehe ila Hatusahau.
 
Back
Top Bottom