Mwanamke kuchukua vitu vya ndani kupeleka kwao.

MAKINYA

Senior Member
Dec 20, 2012
139
54
Wapendaw salaam na heri kwa sikukuu.
Naomba ushauri wa nini cha kufanya hapa niko kwenye ndoa mwaka mmoja sasa,hivi karibuni nimegundua kuwa mke wangu anachukua vitu vya ndani madhalani vyakula na kuvipeleka kwa wazazi wake kisiri bila hata kunambia, nimeona mwenyewe asubuhi akimtuma dereva yebo . Alijua mm bado nimelala kumbe niko chumba kingine ambacho dirisha halikufungwa na kila kinachofanyika nje kinaonekana.nimekuwa na tatizo la vitu kuisha ndani kabla muda wake kwa mfanoo na nunua consumables kwa ajili ya mwezi mzima matokeo yake kabla ya mwezi utaambiwa vimeisha.
Nampenda mke wangu ila kwaa hili amenikwaza kwan ndo kwanza tumeanza maisha sasa kama kila hela itaishia kwenye vyakula tutafanya cha maana kweli?
 
pole ila nafikiri zungumza naye na kuwa wazi mwambie achane na tabia hiyo akiendelea utamrudisha kwao akaishi na wazazi wake ajifunze namna ya kuishi na mme.
 
Hebu ongea naye kwanza ujue sababu ya yeye kufanya hayo
Pengine kwao wanamsumbua sana au wewe umekuwa mkali sana mpaka anaogopa kukushirikisha matatizo ya nyumbani kwao,au anajua hali ya nyumbani kwao na anajua anapaswa kuwasaidia ila hana kipato au ... au.......
Possible reasons ni nyingi na huwezi kujua ipi ni sababu mpaka uongee naye kwa upole.
Pangeni utaratibu wa kusaidia pande zote mbili bila kuathiri ustawi wa familia yenu changa.
Merry Christmas.
 
Hakuna ubaya kwa yeye kuwasaidia wazazi wake tena kwa vitu kama chakula kibaya tu ni yeye kufanya kwa siri. Lakini naamini kuna sababu za yeye kuamua kufanya kwa kificho. Inawezekana kwa namna alivyokusoma kwa mda mliokaa naye anajua akikushirikisha kuna ugumu atakutana nao. Kaa naye muongee kwa uwazi, tatizo ni dogo tu hilo unless awe ana tabia za uswahilini.
 
Wapendaw salaam na heri kwa sikukuu.
Naomba ushauri wa nini cha kufanya hapa niko kwenye ndoa mwaka mmoja sasa,hivi karibuni nimegundua kuwa mke wangu anachukua vitu vya ndani madhalani vyakula na kuvipeleka kwa wazazi wake kisiri bila hata kunambia, nimeona mwenyewe asubuhi akimtuma dereva yebo . Alijua mm bado nimelala kumbe niko chumba kingine ambacho dirisha halikufungwa na kila kinachofanyika nje kinaonekana.nimekuwa na tatizo la vitu kuisha ndani kabla muda wake kwa mfanoo na nunua consumables kwa ajili ya mwezi mzima matokeo yake kabla ya mwezi utaambiwa vimeisha.
Nampenda mke wangu ila kwaa hili amenikwaza kwan ndo kwanza tumeanza maisha sasa kama kila hela itaishia kwenye vyakula tutafanya cha maana kweli?

wazazi wake wana njaa na hana hela ya kutosha kuwanunulia.........msaidie ongea nae umuongezee pocket money awe anawanunulia separate na bajeti yenu.....
 
........Sasa kama wazazi wake hawana mlo, na yeye ana uwezo wa kuwalisha kuna tatizo gani?

Acha kulalamika, je mkeo yeye hana kipato?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuna ubaya kwa yeye kuwasaidia wazazi wake tena kwa vitu kama chakula kibaya tu ni yeye kufanya kwa siri. Lakini naamini kuna sababu za yeye kuamua kufanya kwa kificho. Inawezekana kwa namna alivyokusoma kwa mda mliokaa naye anajua akikushirikisha kuna ugumu atakutana nao. Kaa naye muongee kwa uwazi, tatizo ni dogo tu hilo unless awe ana tabia za uswahilini.

ni jambo la msingi sana kukaa chini na kuzungumza ili kujua upande wa ndani wa tatizo..
..labda huyo mwanamke anaogopa kuwa wazi juu ya familia yake,yote hii ni kutokana na msingi mzima wa mahusiano yenu..
...
 
yaani kwenu chakula kipo afu wazazi wake walale njaa? unaonyesha kuwa unatabia za kichoyo na ndiyo maana anafanya kwa siri. HONGERA ZAKO DADA KWA KUIBA CHAKULA.NA KUPELEKA KWA WAZAZI WAKO.... Miaka michache iliyopita nilikuwa sipendi kabisa nije kuzaa mtoto wa kike ila siku zinavyozidi kwenda nimezidi kugundua kuwa watoto wakike wanahuruma sana kwa wazazi wao. HAPO UTAKUTA HILI JAMAA WAZAZI WAKE WANALALA NJAA LAKINI WALA HALINA MUDA NAO
 
Ukitumia busara kidogo tu km ya binti yangu wa darasa la tatu, utagundua jamaa halalamikii wazazi wa mkewe kupewa msaada bali tabia ya wizi wa mkewe. Huwezi kuhalalisha wizi kwa kigezo cha msaada. Kama ana nia njema, kwanini asimhusishe mmewe?
 
ukipenda boga penda na mizizi yake.wazee walale njaa chrismas hii nyie mna ziada ya vyakula.huyu mwanamke anakufunza kuwakumbuka wakwe mudu mwingine hasa ktk sikuu
 
Ukitumia busara kidogo tu km ya binti yangu wa darasa la tatu, utagundua jamaa halalamikii wazazi wa mkewe kupewa msaada bali tabia ya wizi wa mkewe. Huwezi kuhalalisha wizi kwa kigezo cha msaada. Kama ana nia njema, kwanini asimhusishe mmewe?

.......Inawezekana mume mnoko, ndio maana bidada kaamua kufanya kwa siri.
Wapo wanaume wengi hawapendi wake zao wasaidie kwao, wanaona kama wanafilisiwa.

Tena kuna baadhi ya wanaume utakuta mke ana kipato chake, lakini bado tu wanataka usisadie kwenu.

Ya nini wazazi wafe na njaa, na wakati bidada anaweza kusaidia wazazi.
 
CHAGUA KIMOJA

1. Agawe papuchi kwa vijana wa mjini ili apate pesa ya ziada ya kusaidia familia yake (awe mgawaji) au

2. Awe anachukua vitu vya nyumbani ili kusaidia familia yao
 
Ukitumia busara kidogo tu km ya binti yangu wa darasa la tatu, utagundua jamaa halalamikii wazazi wa mkewe kupewa msaada bali tabia ya wizi wa mkewe. Huwezi kuhalalisha wizi kwa kigezo cha msaada. Kama ana nia njema, kwanini asimhusishe mmewe?

ukiamua kufikiri hata kwa kutumia ma$abur! yako tu, utagundua kuwa jamaa ni mchoyo na hapendi mke wake atoe vitu ndiomaana anafanya siri. kila kitu kina sababu nyuma yake mpuuz wewe
 
Yani mimi nile pilau na makuku halafu wazazi wangu wale dagaa kukicha nooo way....km sina kazi ntachukua tu vya ndani....wao ndo walinifanya mpk ukaniona na kunioa....inaonyesha jamaa ni mchoyo na hupendi kusaidia na amekusoma..yani unalalamikia vitu vidgo km chakula.??? Ss hapo tu ni wazazi je angekua ni bwana .......mana yako mzazi umemtumia kweli ht hela ya sikukuu wewe...hao ni bibi na babu wa watoto wako dont be selfish.....
 
Kuna wanawake wana nyota ya panya buku au fuko...huyo wa kwako ni dizaini hizo.

Kaa chini ongea naye kinagaubaga, itajua ti shida ipo wapi...
 
Wapendaw salaam na heri kwa sikukuu.
Naomba ushauri wa nini cha kufanya hapa niko kwenye ndoa mwaka mmoja sasa,hivi karibuni nimegundua kuwa mke wangu anachukua vitu vya ndani madhalani vyakula na kuvipeleka kwa wazazi wake kisiri bila hata kunambia, nimeona mwenyewe asubuhi akimtuma dereva yebo . Alijua mm bado nimelala kumbe niko chumba kingine ambacho dirisha halikufungwa na kila kinachofanyika nje kinaonekana.nimekuwa na tatizo la vitu kuisha ndani kabla muda wake kwa mfanoo na nunua consumables kwa ajili ya mwezi mzima matokeo yake kabla ya mwezi utaambiwa vimeisha.
Nampenda mke wangu ila kwaa hili amenikwaza kwan ndo kwanza tumeanza maisha sasa kama kila hela itaishia kwenye vyakula tutafanya cha maana kweli?

Sharing is Caring !! MpendwaEee maisha sii kukusanya tu, bali kutumia.... wewe hesabia kama msaada na sadaka tu.
 
Hizo ni tabia za wizi ambao baadae huzaa uongo.
Ongea nae vizuri akwambie kinagaubaga
 
  • Thanks
Reactions: BAK
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom