Mwanamke kama hujui kuhesabu siku zako tumia kinga. Ukipata mimba ya mwanaume asiye mumeo ni hatari


Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
7,707
Points
2,000
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
7,707 2,000
Dada zangu kama hujui siku zako yaani huwezi kuhesabu vizuri hakikisha unatumia kinga, huyo mwanaume hatakuoa, iko hivi kama mwanaume hajakuoa si mume wako, ukibeba mimba yake basi jua kuwa wewe ni single mother. Ndiyo hata wewe ambaye unasoma hapa mimba ina miezi miwili kaikubali subiri ikifika miezi sita ndiyo utanielewa, narudia kama si mume wako basi acha kubeba mimba yake!

Sasa wewe jibebeshe mimba halafu uje kusema ni bahati mbaya, bahati mbaya kwani ulikua unapita njiani ukaikanyaga? Mwanaume ambaye hajaamua kuoa, ambaye hawezi kuoa basi jua kua hawezi hata kuhudumia mtoto? Sasa wewe jifanye una kizazi cha majaribio ndiyo uone? Kwanza nani kakudanganya kuwa uko peke yako, hivi mtu umejuana naye miezi sita unabeba mimba yake unafikiri kabla ya hapo hakua na mtu au hao aliokua nao hawkaua na vizazi!

Kuna sababu hawakutaka kuzaa naye na kuna sababu hakuzaa naye, hivyo ukijishaua kuwa unapendwa na kujiona kuwa ndiyo umefika nadhani itakua juu yako. Nikukumbushe tu kuwa wanaume wengi hawakatai mimba za miezi mitatu minne, mimba inakataliwa baada ya miezi sita au mtoto kuzaliwa, hapo anajua kuwa huwezi kuitoa hivyo anakataa akijua utapambanda mwenyewe mpaka mtoto akiwa mkubwa ndiyo atakuja kumchukua, nishamaliza, ambaye huniamini nenda kabebe na ambaye ushabebeshwa pole lakini sio mwisho wa maisha! Ulifanya hivyo kwa kua hukujua haya.. Sasa usitoe mimba maana tiari huyo ni kiumbe cha Mungu siyo cha huyo tena mwehu, mdanganyi ukizaa atakupa furaha na ukizaa kama amemkataa asimujue hivyo hivyo ila kutoa mimba ina madhara makubwa sana unaweza kua mgumba au ukasababisha kansa au ukasababisha mimba zako ziwe zinatungwa nje yamfuko wa uzazi, kuchelewa kupata mimba au kutopata kabisa sasa usitoe mimba ni kiumbe kisicho kua na makosa hicho ni malaika mwenye makosa ni mwanaume huyo asiyena huruma uliye dhani umepata kube laghai... UMENIELEWA?
 
mulwanaka

mulwanaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
2,549
Points
2,000
Age
35
mulwanaka

mulwanaka

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
2,549 2,000
Wewe unafikiri kila mwana mke anae taka kuzaa ana kiu ya kuolea? Ndoa ni matatizo kuliko kua singo maza......kwa taarifa yako.
 
Born2xhine

Born2xhine

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2014
Messages
482
Points
500
Born2xhine

Born2xhine

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2014
482 500
Ukiona wameanza kutoa povu ujue ujumbe wako umefika sehem husika

Message delivered
 

Forum statistics

Threads 1,285,016
Members 494,369
Posts 30,847,424
Top