Mwanamke jela kwa kufanya mapenzi na mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke jela kwa kufanya mapenzi na mtoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Mar 25, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE ambaye ni mke wa mtu mwenye watoto watatu, amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 15.

  Mbali na mwanamke huyo, Sophia Philemon (44) mkazi wa kambi namba tisa katika kiwanda cha sukari cha TPC, wilaya ya Moshi vijijini kuhukumiwa kifungo hicho, pia ameamriwa kumlipa mwanafunzi huyo fidia ya Sh1 milioni.

  Hukumu hiyo, ilitolewa jana mjini Moshi na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro, John Nkwabi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.

  Nkwabi alisema ushahidi wa mashahidi hao, akiwemo mwanafunzi huyo wa sekondari ya Langasani, umeithibitishia mahakama pasipo shaka yoyote kwamba mwanamke huyo, alimlazimisha mtoto huyo kufanya naye tendo la ndoa.

  Kitendo hicho ni kosa chini ya kifungu namba 138B (1) (d) cha kanuni ya adhabu kinachosimamia makosa ya kimapenzi kwa watoto baada ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Hakimu Nkwabi alisema mahakama imeridhika na ushahidi kuwa Februari 28, mwaka jana, saa 1:00 usiku huko kambi namba tisa, mshitakiwa alimlazimisha mwanafunzi huyo kufanya naye mapenzi katika chumba anachoishi na mumewe.

  Muda huo, mwanafunzi huyo alikuwa ametoka dukani alikokuwa ametumwa na wazazi wake na mwanamke huyo, alimwita na kumshawishi aingie ndani ya nyumba yake na baadaye kumlazimisha kufanya naye tendo la ndoa.

  Baada ya kutiwa hatiani, wakili wa serikali, Hellen Moshi aliyeendesha kesi hiyo, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwani vitendo vya ubakaji vinazidi kuongezeka nchini hususan kwa watoto wadogo na wanafunzi.

  Katika utetezi wake, Sophia alisema ni mke wa mtu na hakubahatika kupata mtoto na mwanaume huyo, lakini kabla kuolewa alikuwa tayari amezaa watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume.
  Mshitakiwa alikuwa alikataa kufanya tendo la ndoa na mtoto huyo, licha ya kumfahamu kuwa ni jirani yake. Utetezi wake ulitupiliwa mbali na mahakama hiyo
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hii kali !
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mtoto ni under 18 alitakuwa afugwe kwa sheria ya kubaka - miaka 30 jela.
  Sasa sijui hii miaka 7 imekujajekujaje? kwa sheria ipi? wanasheria tufafanulieni
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu hakuna usawa wa kijinsia ila kna upendeleo wa kijinsia................
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa kuna upendeleo wa kijinsia kwa nini wanaume tu ndio wanafungwa miaka 30 au maisha jela?
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi ni kwamba kisheria 'kubaka' kunaambatana na 'kitendo cha kuingiza uume....'. Hivyo, technically mwanamke hawezi 'kubaka'!
   
 7. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kubaka ni kubaka, no matter what.........
   
 8. R

  Renegade JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 1,072
  Trophy Points: 280
  Mh. Haya mambo mengine hata huwezi kuelewa? Si angeamua kuwa kahaba tu, ukame gani huu sasa?
   
 9. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2010
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni kweli bro, miaka saba haimtoshi kabisa kwa unyama alioutenda
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  unyama gani kwanza na mtoto mwenyewe angepigwa mvua pia.kwani yeye alivoingia ndani uume wake si ulisimama au?so ali respond kwa tukio la kufanya ngono...hakuna kitu hapa
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha ha ha ha ha basi hapa mjini wadada mnatubaka sana na vivazi vyenu. :(
   
 12. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mh walah mazingira yananipa tabu kuelewa, hapo penye red ndo pananipa nami tashwishwi,ingekua wa kike tungesema mhusika alipenya tu bila kizuizi kulingana na maumbile,ila wa kiume alijipenyeza vipi pale kwa bi mkumbwa bila yeye pia kukubaliana na hali yenyewe then akaweza kupafom??? au kalikua kamchezo kao,ila baada ya wazee kugutuka katoto kakaona kaseme kali.....mh .....
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Aliyeuliza swali alitaka kujua sheria inasemaje. Kwa sheria ya makosa ya kujamiiana na penal code ya Tanzania, mwanaume ndio anaweza kushitakiwa kwa kubaka.

  Ingawa sio relevant sana, lakini ukirejea ile kesi ya Babu Seya, utaona jinsi wakili wao (wakati wa rufaa) alivyokuwa akijaribu kuishawishi mahakama kwamba hakukuwa na penetration (alikuwa ana hoji ni vipi watoto wale wodogo waliweza kutembea baada ya kuwa raped).
   
 14. N

  Nameless- Member

  #14
  Mar 25, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu mwanamke ana umri gani?
   
 15. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haba kosa nafikiri nila kumrubuni mtomto ili afanye mapenzi, amabayo ni aina fulani ya ubakaji!
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu Akili na SMU mna point kabisa!Haya ndio matokeo ya kupitishia Sheria kutokana na mlolongo wa harakati ( activism) badala ya kupitia mchakato makini zaidi utakaoingia kwa undani kutafiti tatizo, mapungufu yaliyopo na ufumbuzi muafaka.
  Sheria ya makosa ya Kujamiiana - sexual offences Special Provisions Act (SOSPA )1998 ina mapungufu mengi sana - mkazo na msisitizo umewekwa zaidi kulinda staha ( dignity) ya wanawake inayopotea kutokana na unyanyasaji wa kijinsia. In the process ikaacha gaps nyingi - mfano ndio kama huu wa kushindwa kuwalinda watoto wa kiume kwa kiwango kilekile wapatacho watoto wa kike.

  Vile vile sheria hiyo inawalinda watoto wa kike ( wasichana) wa chini ya miaka 18 wasikeketwe na kusahau kuwa kuna wanawake ambao hukeketwa wakishavuka umri huo na madhara ya ukeketeja ni yale yale.Hii ni mifano michache.

  Kuna Sheria ya VVU/UKIMWI ya 2008 ( HIV/AIDS( Prevention and Control) Act 2008 iliyoanza kutumika 2009 ila kiutendaji bado haijawekewa kanuni za kuitumia.Sheria hii nayo ni matokeo ya harakati hasa za kuzuia wale wenye kuambukiza kwa makusudi ( na hii ni kasheshe maana utakusanya vipi ushahidi kuwa umeambukizwa na mtu fulani tena kwa makusudi wakati mkifanya kitendo wote hamkupima kujua hali zenu?!)......Kufanya uambukizo kuwa kosa la jinai nako kutawazuia watu wasijiweke wazi kuhusu hali zao...hii itachochea maambukizi zaidi...

  Haya mapungufu yaliyopo yanahitaji kufanyiwa kazi haraka sana ili angalau tuone haki ikitendeka kwa wote - wanawake na wanaume.
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kigogo unaniangusha fikiria tena then repost

  Hivi umesoma bandiko la bujibuji au unauliza tuu swali?
   
 18. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wamemwonea yule mama bana! Kubaka ni kumuingilia mtu kwa nguvu na kufaidi alicho nacho. Mwanamke hawezi kumwingilia mtu kwa nguvu (kumbaka mwanaume) kwani ili afaulu lazima kuwe cooperation ya mwanaume, yaani anyanyue "winchi" yake - ambayo mpaka inyanyuke lazima mwanaume awe ameridhia, yaani hisia kaziachia kutoka ubongoni mpaka huko viungoni. Kwa hiyo, kwa kesi hii mi naona yule dogo aliridhia kufanya ngono na mama yule ndiyo maana alisimamisha, vinginevo asingetaka asingesimamisha. Labda tu tuseme yule mama alimshawishi kwa msisitizo dogo, naye akajikuta anajiaachia.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Swala la ridhaa katika kufanya kitendo na mtoto aliye chini ya miaka 18 kisheria huwa halipo ndugu yangu. Kabla ya 1998, ukimchukua msichana mkakubaliana na ukasema ulidhani ana miaka zaidi ya 15 ( umri uliowekwa kisheria kipindi kile) kwa vile ALIRIDHIA KUFANYA, na umbo lake lilikudanganya, ungeweza kabisa kukwepa kwenda jela. Siku hizi baada ya Sheria ya 1998 kuanza kutumika basi hakuna uteteze tena. Mradi binti yuko chini ya 18yrs na siyo mkeo hata kama kakubali kufanya, mvua 30 hutakwepa.

  Tukija kwa mtoto wa kiume, tunaona sheria haikuwekwa kwa makini kuwalinda. Hebu wewe fikiria kama una mtoto wa miaka 15 anayesoma, anarubuniwa kufanya kitendo hicho ni madhara mangapi atayapata? Masomo atazingatia tena? Je atakuwa salama asiambukizwe magonjwa ikiwemo UKIMWI?
   
 20. f

  fikrahuru Member

  #20
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kweli nashindwa kuelewa hii sheria ya SOSPA ipo kwa ajili ya kukomoa au kurekebisha tabia. au ni wanasheria wanaitafsiri vibaya kuwapendelea wanawake. wanasheria tufafanulieni plz.
   
Loading...