Mwanamke: Je unashindwa kujenga uhusiano imara, sababu ni hizi hapa….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke: Je unashindwa kujenga uhusiano imara, sababu ni hizi hapa….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 26, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Labda nianze na swali:


  Je umewahi kuwa na mtoko na mwanaume na baada ya kuwa naye karibu kwa miezi labda tuseme mitatu, sita au muda mrefu zaidi ya hapo ukamuona kuwa huyo ndiye mwanaume sahihi na anayekufaa, lakini kila unapojaribu kuwa naye karibu zaidi kwa mazungumzo ya kina anaamua kuadimika kwako na uhusiano wenu ukaisha muda mfupi baada ya hapo?

  Kama jambo hilo liliwahi kukutokea, basi naamini mpaka leo hii utakuwa unafikiria kwamba huenda utakuwa umemfanyia kitu kibaya mwanaume huyo! Kwa bahati mbaya ni kwamba hisia zako ziko sahihi.
  Baadae nitakuekuleza sababu.

  Tatizo kubwa linalowakabili baadhi ya wanawake ni kutowajua wanaume. Ukweli ni kwamba ni vigumu sana kuwajua wanaume na wanawake wengi hawajui kwamba wanaume ni watu wa siri sana. Si rahisi kumjua mwanaume mara moja, labda uwe na bahati sana. Mtaalam mmoja wa masuala ya uhusiano, John Gray anasema wanaume wanatoka kwenye sayari ya Mars na wanawake wanatoka kwenye sayari ya Venus, ina maana kwamba wanatofautiana sana.Kwa maneno yake mwenyewe John Gay anasema:

  "Men Are from Mars, Women Are from Venus is a manual for loving relationships in the 1990s. It reveals how men and women differ in all areas of their lives. Not only do men and women communicate differently but they think, feel, perceive, react, respond, love, need, and appreciate differently. They almost seem to be from different planets, speaking different languages and needing different nourishment."

  Wanawake wengi hawapati wanaume waliowakusudia, na ina kuwa mbaya zaidi hasa pale mwanaume mwenyewe anapokuwa ni wa shoka, mwenye mustakabali wa kusisismua. Unapompata mwanaume wa aina hiyo na uliyetokea kumpenda kwa moyo wako wote lakini akatokomea katika mazingira ya kutatanisha wakati tayari ulishamtia mkononi, inachanganya sana. Kusema ukweli wanaume wenye mwafaka ni wagumu kuwapata na wako wachache. Inapotokea kwamba umempata kwa bahati na ukajiona kama umelamba dume, halafu akakuponyoka kimzahamzaha inakuwa dhahama na balaa kubwa. Yaani unakuwa na mwanaume kwa miezi sita au zaidi halafu anakuponyoka hivi hivi, mchana kweupe…….! Haiyumkini ndio sababu ya wanawake wengi kwenda kwa waganga wa asili kujitizama kama wamelogwa……………

  Hapa chini nitadadavua makosa manne wayafanyayo wanawake kwa wanaume bila kujua. Yapo makosa mengine lakini haya ndio yanayotia fora:
  [​IMG]

  1. Kosa la kwanza: Kuishi na mwanaume katika hali ambayo unajifanya huko salama. (Yaani huamini kwamba, anakupendana mtaendelea kuishi wote). Ukifanya hivi, mwanaume hatafurahi. Muamini, halafu jiamini mwenyewe. Kwa bahati mbaya hata wanawake wanaoonekana wanajiamini sana nao hufanya makosa kama haya ya kutokujiamini. Kuanzia leo ujue kwamba, mwanaume ukimwonyesha dalili za kujifanya huna uhakika na uhusiano wenu, maana yake wewe ni king'ang'anizi na mpenda kumiliki. Mwanaume huyo atakuona hufai.
  [​IMG]
  2.
  Kosa la pili: Kuwaongelea vibaya mabwana zako wa zamani. mwanaume atakuwa na wasiwasi kama akiachana na wewe kwa bahati mbaya basi utamsilibia kama unavyowafanyia wanaume ulioachana nao. Usijifanye kumponda wa zamani, huna haja ya kumtaja au kumzungmzia kama sio lazima. Si hivyo tu, pia kuwaongelea vibaya wanawake wengine ina mchango wake katika kumkimbiza mwanaume umpendaye. Wanawake wana kawaida ya kuwaponda wanawake wenzao kwa kuwaita Malaya na maneno machafu kama hayo. Hii mara nyingi inatokana na kuwaonea wivu wanawake hao kutokana na uzuri wao. Wanakuwa na wasiwasi kwamba, watawachukua mabwana zao. Mwanaume akigundua kwamba unamponda mwanamke mwenzio kwa sababu tu ya uzuri wake, anajua hujiamini na unajihisi huko salama. Atakuona hufai

  [​IMG]
  3.
  Kosa la tatu: Kufikiria kwamba kwa kufanya sana naye ngono ndio kumweka kwapani badala ya kumshika kihisia. Wanawake wengi wanaota ndoto kwamba wanaume wana usongo sana na ngono na ndicho kipaumbele chao pekee….. na wanadhani kwamba ukimdhibiti mwanaume kingono ndiyo umemaliza kazi yote kwani itakuwa ni rahisi kumteka kihisia. Mwanaume ana kawaida ya kutenganisha uhusiano, anaona kuna uhusiano wa aina mbili ambao ni uhusiano wa kingono na uhusiano wa kihisia. Inatakiwa sanaa kubwa kwa mwanamke kuziunganisha aina hizo mbili za uhusiano ili mwanaume asiendelee kuzitenganisha. Mwanamke anayeweza kufanikiwa kumuweka mwanaume kwapani ni yule anayeweza kumnasa mwanaume kingono na kihisia. Lakini kikubwa zaidi ni kihisia kuliko ngono. Juhudi za kumpa ngono kwa njia hizi au zile haziwezi kuzaa matunda kama kihisia watu wako mbali.
  [​IMG]
  4. Kosa la nne: Uzuri wa mwanaume. Wanawake wengi wanakuwa na kigugumizi kuhusu kuweka uzuri wa mwanaume kama kipaumbele cha kwanza. ndiyo, uzuri ni jambo jema, lakini linaweza kuwa jambo la hatari. Tatizo ni kwamba mkiendelea kumchagua mwanaume kutokana na uzuri wake ni rahisi kuvurugikiwa na akili kutokana na uzuri huo kiasi cha kushindwa kuyaona makosa yake mapema. Unakuja kugundua kwamba, pamoja na uzuri wa mwanume huyo. Si lolote si chochote kitabia. Unaanza kuchanganyikiwa wakati uko ndani ya ndoa. Na mara nyingi, uhusiano unaolegalega ni kwa sababu wanawake waliwachagua waume zao kutokana na uzuri wao wa sura na maumbile………………..

  Nitaendelea kudadavua sababu nyingine nikipata fursa ya kufanya hivyo…………….
   
 2. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  nimependa picha
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,520
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  namba 3 inahuu aisee...watu bize ufundi wa 6X6 kumbe kuna mengi zaidi.
   
 5. chameli

  chameli Senior Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kuzungumzia mabwana wa zamani kwangu ngumu sababu jamaa atachoka yaani mabwana wangu wa zamani wanajaa Dar Express na wengine wanasimama.
   
 6. telitaibi

  telitaibi JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tumekupata mkuu sasa nakaa mkao wa part 2 ya hii
   
 7. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  haya kazi ipo na ndio maana miye huwa nawashangaa sana ambao kwao akipata bf kesho ngono inaanza kumbe ni kujizeesha tu. mwanmke ujitunze wasikurubuni manake wanaume huwa hata siku moja hawachoki kufanya ngono. kwao kila akipewa basi atakubali na huwa wala haimaanish chochote katk maisha yao zaid ya starehe tu.
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Mimi namsubiri Zinduna aje hapa!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  hapo namba mbili, hiyo inaboa si tu kwa wanaume hata mwanamke....kwa nini umdiss ex wako?....

  Halafu namba nne unaongelea uzuri upi? Wa sura? Yaani handsomeboys? Au? Kama handsomeboys oooophs huwa hawafai.....

  Lakini heri uwaambie wanawake, mchezo wa kujiachia siku mbili tu anaishia kitandani kwa mwanaume haufai.....
   
 10. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Out of topic kidogo, Nilipomaliza form six, my cousin sister (older than me) alinipa hiki kitabu cha Men are from Mars, Women are from Venus. Its one of the best book I have ever read. It opened up my mind big time, I think kila mwenye kujua kusoma akitafute.
   
 11. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Asante kwa somo babu
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  umenikumbusha marehemu jamaa yetu aliwahi kusema kuwa hata kama hatukumzika mabibi zake wote wakifika kaburini na kila mmoja akadodosha chu.pi yake moja kaburini litajaa,ndo hayo ya dar express,hongera kwa kuji express,mwili wako babu utumie utakavyo!
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  ama kweli umebadili tabia,hongera!
   
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Zinduna anasumbuliwa na ujauzito,niko naye hapa clinic amana,nimwambieje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mimba ya mkeo inaendeleaje?
   
 16. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  gfsonwin,NYIE NDO MNACHOKA NGONO? ULIZA MWANAUME YEYOTE AMBAYE ANA BIBI MWENYE UMRI WA KUANZIA 35-45 AKUELEZE SURUBA ANAYOPATA.KATIKA UMRI HUU MWANAMKE NDO ANAPEVUKA (NA KUANZA KUMWAGA MAYI) BASI SHUGHULI YAKE UTATAMANI NYUMBA UHAME,ASK ANY MAN AKIWA MKWELI ATAKWAMBIA.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  umesikia yaliyotokea juzi asubuhi new york karibu na empire building? nikikushukia kile kitakuwa cha mtoto.
   
 18. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  umekariri eh? utekelezaji?
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Aug 27, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I can vouch for you.

  Your wife loves me a lot because I lay down the pipe more than you could ever do.

  And that's why she calls you Ngabu when your name is Bishanga.
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Duh!Kumbeee!!Sasa wewe upo nae kiaje?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...