Mwanamke epuka haya makosa upunguze nafasi ya kuumizwa kwenye mahusiano.

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Huu ni ushauri wangu wa bure kwa kina dada. Mwanamke unapaswa kuepuka haya makosa ambayo hua mnayafanya bila kutegemea au kwa kudhamiria na mwisho wa siku wengi wenu huishia kulia. Haya ndio makosa(common mistakes) ambayo wanawake mnapaswa kuyaepuka.

1. Epuka kumpenda mwanaume mwanzoni, mwanzo wa mahusiano yenu baada ya kumpima mwanaume na kujiridhisha kua anakidhi vigezo vyako unavyovitaka basi usikimbilie kumpa moyo wako, usikimbilie kumpenda, acha yeye akupende.

Najua hii ni ngumu kwa wanawake maana mnaongozwa na hisia zaidi kwenye mapenzi kuliko uhalisia, ila kwa tahadhari na kwa mahusiano endelevu usimpende mwanaume, mtengenezee mazingira ya kukupenda kwanza, mwanaume akikupenda, mahusiano yenu yatafika mbali, ila ukimoenda wewe na bahati mbaya yeye hakukupenda alikutamani tegemea lolote wakati wowote.

2. Usikubali kuingia kwenye mahusiano uliyounganishwa na ndugu, jamaa au marafiki kwa urahisi. Wanawake mnapenda sana kuwaamini watu kwa haraka kisa tu mmeunganishwa na ndugu na jamaa, kuunganishwa na mtu sio kigezo cha wewe kumpa moyo wako haraka, wanaume wengi hutumia ndugu na jamaa au marafiki kuwapata marafiki zao kiurahisi, na wengi hua mnaingia huo mkenge kwa urahisi. Simaanishi wanaounganishwa kwenu wote ni wabaya ila usijiaminishe kwao kiurahisi. Jiridhishe kwanza kama kweli ni mtu atakaekufaa mbeleni.

3. Epuka outing na marafiki zako ambao huja na watu usiowajua. Wanawake wengi hutafunwa kiurahisi kwa mtindo huo hasa wanywa pombe. Unaitwa mtoko na rafiki yako, kisha yeye anakuja na marafiki zake wa kiume ambao wewe huwajui ndio mara yako ya kwanza kuwaona, ni bahati sana hiyo siku ikaisha bila wewe kuliwa hasa kama wewe ni mlevi. Wanaume wengi hutumia hiyo mbinu kuwanasa wanawake kwa urahisi bila kuwatongoza. Sio marafiki zako wote wana nia njema na wewe, anaweza kupanga mchongo na mwanaume ili akupate kiurahisi kwa kumpa udhaifu wako na wakaamua kutumia huo udhaifu wako kukuingiza matatizoni.

4. Usirudiane na mwanaume uliemuacha kwa sababu zozote. Ni mara chache sana mahusiano ya mwanaume wako wa zamani mlierudiana yakafanikiwa, mara nyingi huishia pabaya kuliko ilivyokua awali. Usikubali kurudiana na ex wako kwa sababu zozote. Wanaume wengi kama mimi hua hatuachi wanawake hata kama hatuwapendi, unaweza kuniacha na bado kila siku nikawa nakusisitiza kua bado nakuhitaji ingawa sio kwa kumaanisha, kua makini unapotaka kurudiana na ex wako.

5. Usipime dhamira ya mwanaume kwa utayari wake wa kuwajua ndugu zako au kuja kwenu. Wanawake hua mnaniacha hoi sana. Vigezo vyenu vya kupima dhamira ya mwanaume anaekutaka kwa mara ya kwanza hua ni vyepesi sana, na ni rahisi sana kwa mwanaume kuvitimiza na mwisho wa siku ukaja kujua kua hakua na nia au dhamira ya dhati. Kwa mwanaume anaekutaka iww kwa dhamira safi au mbaya sio vigumu kwake kuja kwenu au kuwajua ndugu zako, hvyo ukimwambia mwanaume aje kwenu au awajue ndugu zako na akawa tayari kuja sio sababu wewe umuamini kwa haraka, mabazazi wengi hiyo sio shida kwao. Jipe muda zaidi na utafakari.
Yani kua watu anakwambia kama kweli uko serious njoo uonane na dada, unaenda kesho anakupatia uchi bila hata condom. Hatari sana.

Huu ni ushauri wa bure kwa kina dada, ni hiyari yako uupokee na kuutafakari au kuachana nao.
 
Ukiona mtu ambae hajasomea "mahusiano" kama fani halafu anajifanya kutoa ushauri mwingi sana kuhusu mahusiano hayo hayo,kuna uwezekano mkubwa sana yeye binafsi mahusiano amekua akifeli sana hivyo yuko obsessed nayo..

Hii ni normal kabisa..anaefeli kitu sana,hua anajifanya "kuwaelewesha" kitu hicho wengine ili apate kujisikia vizuri kwenye moyo wake unaofeli sana hicho kitu husika....

It is very very funny!
 
Namba nne umenikosea sana blaza kwa kuuza silaha zetu wanaume.
Ila flessshhh ndo kama ivyo tena wanaume hatuachi mwanamke na huo ndo ukweli hata kama una sura personal aje but NGEZI zikitudaka tutakusaka tu.
Blaza umeblast mbaya.
 
wape kubwa tu waepuke kujitongozesha tu.

Sijui ni mimi peke angu au na wanaume wenzangu ila kila nkienda sehemu nakuta type mbalimbali za wanawake wakijitongozesha kwangu au kwa rafiki yangu.

Bahati mbaya, mwanaume ukimeet mahitaji yake ya kingono atakugonga tu,sometimes anaweza kukuonea huruma kukugonga na kukuacha basi atakuwa anakuchekea tu,we unadhani labda mtu domo zege kumbe mwenzako anakuonea huruma.

Unajiletaleta hovyo komaaaaaa linda thamani yako,matokeo yake uje kulata uzi bwana ako anakuomba hela,Ndio acha akuombe si ulijileta mwenyewe.Hapa sio ulaya,kajitongozeshe kwa wazungu huko.
 
Huu ni ushauri wangu wa bure kwa kina dada. Mwanamke unapaswa kuepuka haya makosa ambayo hua mnayafanya bila kutegemea au kwa kudhamiria na mwisho wa siku wengi wenu huishia kulia. Haya ndio makosa(common mistakes) ambayo wanawake mnapaswa kuyaepuka.

1. Epuka kumpenda mwanaume mwanzoni, mwanzo wa mahusiano yenu baada ya kumpima mwanaume na kujiridhisha kua anakidhi vigezo vyako unavyovitaka basi usikimbilie kumpa moyo wako, usikimbilie kumpenda, acha yeye akupende.

Najua hii ni ngumu kwa wanawake maana mnaongozwa na hisia zaidi kwenye mapenzi kuliko uhalisia, ila kwa tahadhari na kwa mahusiano endelevu usimpende mwanaume, mtengenezee mazingira ya kukupenda kwanza, mwanaume akikupenda, mahusiano yenu yatafika mbali, ila ukimoenda wewe na bahati mbaya yeye hakukupenda alikutamani tegemea lolote wakati wowote.

2. Usikubali kuingia kwenye mahusiano uliyounganishwa na ndugu, jamaa au marafiki kwa urahisi. Wanawake mnapenda sana kuwaamini watu kwa haraka kisa tu mmeunganishwa na ndugu na jamaa, kuunganishwa na mtu sio kigezo cha wewe kumpa moyo wako haraka, wanaume wengi hutumia ndugu na jamaa au marafiki kuwapata marafiki zao kiurahisi, na wengi hua mnaingia huo mkenge kwa urahisi. Simaanishi wanaounganishwa kwenu wote ni wabaya ila usijiaminishe kwao kiurahisi. Jiridhishe kwanza kama kweli ni mtu atakaekufaa mbeleni.

3. Epuka outing na marafiki zako ambao huja na watu usiowajua. Wanawake wengi hutafunwa kiurahisi kwa mtindo huo hasa wanywa pombe. Unaitwa mtoko na rafiki yako, kisha yeye anakuja na marafiki zake wa kiume ambao wewe huwajui ndio mara yako ya kwanza kuwaona, ni bahati sana hiyo siku ikaisha bila wewe kuliwa hasa kama wewe ni mlevi. Wanaume wengi hutumia hiyo mbinu kuwanasa wanawake kwa urahisi bila kuwatongoza. Sio marafiki zako wote wana nia njema na wewe, anaweza kupanga mchongo na mwanaume ili akupate kiurahisi kwa kumpa udhaifu wako na wakaamua kutumia huo udhaifu wako kukuingiza matatizoni.

4. Usirudiane na mwanaume uliemuacha kwa sababu zozote. Ni mara chache sana mahusiano ya mwanaume wako wa zamani mlierudiana yakafanikiwa, mara nyingi huishia pabaya kuliko ilivyokua awali. Usikubali kurudiana na ex wako kwa sababu zozote. Wanaume wengi kama mimi hua hatuachi wanawake hata kama hatuwapendi, unaweza kuniacha na bado kila siku nikawa nakusisitiza kua bado nakuhitaji ingawa sio kwa kumaanisha, kua makini unapotaka kurudiana na ex wako.

5. Usipime dhamira ya mwanaume kwa utayari wake wa kuwajua ndugu zako au kuja kwenu. Wanawake hua mnaniacha hoi sana. Vigezo vyenu vya kupima dhamira ya mwanaume anaekutaka kwa mara ya kwanza hua ni vyepesi sana, na ni rahisi sana kwa mwanaume kuvitimiza na mwisho wa siku ukaja kujua kua hakua na nia au dhamira ya dhati. Kwa mwanaume anaekutaka iww kwa dhamira safi au mbaya sio vigumu kwake kuja kwenu au kuwajua ndugu zako, hvyo ukimwambia mwanaume aje kwenu au awajue ndugu zako na akawa tayari kuja sio sababu wewe umuamini kwa haraka, mabazazi wengi hiyo sio shida kwao. Jipe muda zaidi na utafakari.
Yani kua watu anakwambia kama kweli uko serious njoo uonane na dada, unaenda kesho anakupatia uchi bila hata condom. Hatari sana.

Huu ni ushauri wa bure kwa kina dada, ni hiyari yako uupokee na kuutafakari au kuachana nao.
POINT YA MSINGI NI KUWA WAACHE KUOMBA OMBA HELA OVYO.
 
Ukiona mtu ambae hajasomea "mahusiano" kama fani halafu anajifanya kutoa ushauri mwingi sana kuhusu mahusiano hayo hayo,kuna uwezekano mkubwa sana yeye binafsi mahusiano amekua akifeli sana hivyo yuko obsessed nayo..

Hii ni normal kabisa..anaefeli kitu sana,hua anajifanya "kuwaelewesha" kitu hicho wengine ili apate kujisikia vizuri kwenye moyo wake unaofeli sana hicho kitu husika....

It is very very funny!
Sio mbaya kutuhabarisha mapungufu yake tujifunzee yasirudie kwetu
 
Eti mtu anasema niweke profile nijue kama unanipenda na huna mtu mwingine. Mtu kablock namba zote hatarishi na mdada kawekwa profile mwezi mzima. Baada ya hapo unajua nini kilifuata kati ya hao wawili.. My point, hawa watu vigezo vyao ni zero
 
Back
Top Bottom