Mwanamke: Dalili zitakazomfanya mpenzi mpya akuone wewe ni king’ang’anizi…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke: Dalili zitakazomfanya mpenzi mpya akuone wewe ni king’ang’anizi…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 15, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hizi ni miongoni mwa sababu ambazo wanaume wengi huchomoa mapema kwa wapenzi wao wapya kabla uhusiano haujashika kasi. Kuna wakati wanawake hukosea na kuvuka mipaka mwanzoni tu mwa uhusiano. Anamganda mwanaume haraka sana au anaonesha dalili zote za kujipendekeza kupita kiasi. Lakini jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba, wanaume wako makini sana kuwakwepa wanawake ving’ang’anizi……..

  Nitadadavua baadhi ya vijitabia vya wanawake vinavyowafanya wanaume wawaone kama ni ving’ang’anizi…..
  [​IMG]
  1. Unataka kuwa naye muda mwingi kuliko kawaida…
  Ni vizuri kwa wapenzi wapya kupata fursa ya kuwa pamoja peke yao, lakini kama unakataa kuwa na mtoko, kuhudhuria sherehe au kukutana na marafiki na kulazimisha kuwa pamoja peke yenu mahali fulani pa faragha, basi hapo ni lazima mwanaume atadhani kwamba unataka akupe umuhimu wa pekee muda wote. Unaweza kukuta mwanamke anakuwa king’ang’anizi kiasi kwamba hana muda na marafiki zake au watu wengine isipokuwa mpenzi wake. Anakuwa kama mzigo, muda wote yuko nyuma ya mwanaume kila anapokwenda…. Hapa ni lazima mwanaume atatemana na wewe kungali mapema. Hakuna mwanaume anayeweza kujenga mahusiano na mwanamke wa aina hii, watakukimbia kila siku.

  2. Unampangia mwanaume kila kitu… Unampangia aina ya mavazi ya kuvaa, unaanza kuboresha mazingira ya nyumbani kwake haraka sana kwa kununua vitu mbalimbali vya nyumbani kwake bila kushauriana naye. Hiyo ni dalili kwamba una matarajio makubwa kwake, jambo ambalo kwake yeye bado halijamuingia akilini. Hapa mwanaume ambaye huyachukulia mambo kwa tahadhari, hukuona kuwa wewe ni king’ang’anizi na unataka kukita mizizi kwake wakati bado anachunguza uhusiano wenu ili kujua iwapo utakuwa kama vile anavyotarajia yeye… Kumbuka kwamba kila mtu ana sifa azitakazo pale anapochagua mwenza, na ni vigumu kumjua mtu kwa muda mfupi. Kunahitajika muda wa kutosha mtu kumjua mwenzake vizuri linapokuja swala la mahusianao. [​IMG]
  3. Unatumia muda mwingi zaidi kukaa kwake….
  Unalala kwa mpenzi wako, na asubuhi mwanaume huyo anaondoka kwenda kwenye shughuli zake, na wewe unabaki labda ukidai unamsaidia usafi kidogo. Lakini anaporudi jioni anakukuta bado uko hapo nyumbani kwake ukiwa umejipumzisha. Inawezekana ukawa umeandaa chakula cha usiku tayari na pia huenda ukawa umebeba nguo za kubadilisha kwenye mkoba wako pamoja na vipodozi ukiwa umejiandaa kulala tena hapo kwake. Huonyeshi dalili za kuondoka hapo kwake zaidi ya kwenda kwako au kwenu na kubadilisha nguo na kuchukua viti vichache utakavyovihitaji utakapokuwa hapo kwake, lakini unapanga hayo yote bila kumshirikisha zaidi ya kukuona tu ukimganda kama luba. Huonyeshi kuwa na maisha yako kama wewe, zaidi ya kujipachika kwake……


  [​IMG]
  4. Unajenga urafiki na mama yake haraka sana……
  Baada ya kukutambulisha kwa mama yake na kubadilishana namba za simu au labda na email, unaanza kujenga ukaribu na mama yake kupita kiasi. Wanawake wengi hudhani kwamba, iwapo watajenga urafiki na mama wakwe watarajiwa, basi itakuwa rahisi kwao kumnasa mwanaume huyo, maana huamini kwamba watoto wa kiume hawawezi kwenda kinyume na mama zao linapokuja swala la kuchagua mwenza. Kwa kawaida wanaume humuona mwanamke anayejipendekeza kwa mama yake kama vile anataka kulazimisha uhusiano au ndoa, hivyo humchukulia kama ni king’ang’anizi.

  [​IMG]

  5. Unampigia simu na kumuuliza kama yuko wapi…..
  Unapompigia simu badala ya kumjulia hali unakuwa na maswali ya kipolisi.. ‘Uko wapi?’ ‘Unafanya nini? Maswali ya aina hiyo mwanaume huyachukulia kama ya kimtego na hawafurahishwi nayo. Wanawake wengi huamini kwamba wanaume huwa hawasemi ukweli kuhusu mahali walipo pale wanapoulizwa na wenzi wao. Jambo hilo linaweza kuwa kweli au lisiwe kweli. Inawezekana kuwa kweli kwa sababu labda ya wanaume kukwepa maswali mengi. Mara nyingi wanawake hawaridhiki na jibu moja. Mfano ni jioni ndio ametoka kazini, lakini nakapitia mahali fulani kukutana na rafiki yake, inawezekana ikawa ni kwenye mghahawa au kwenye baa. Kama mwanamke akipiga simu na mwanaume akamwambai yuko kwenye baa na rafiki yake, yatafuata maswali lukuki. Hakuna mwanaume anayependa kuulizwa maswali mengi kama vile anatuhumiwa. Na ndio sababu wanaume wengi wanakwepe kusema mahali walipo. Kwa hiyo ili kuepuka maswali anaweza kujibu kwa kifupi tu kwamba yuko kwenye kikao kazini na hatakuwa hewani, ili apate nafasi ya kuzima simu japo kwa muda. Mwanaume humuona mwanamke mwenye udadisi wa aina hiyo kama king’ang’anizi.


  [​IMG]
  6. Unakuwa na chuki na wanawake wenzako…
  Pale ambapo mwenzi wako anapomtaja mwanamke fulani, inaweza kuwa ni mfanyakazi mwenzake, mke wa kaka yake au mtu wanayeshirikiana kibiashara, unaonyesha kisirani cha waziwazi kwamba unakerwa na ukaribu wake na wanawake wengine. Tabia hii inaashiria kwamba wewe unapenda kumiliki na wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wenye vijitabia vya kupenda kumiliki. Hapo ni lazima utaonekana kuwa wewe ni king’ang’anizi na uhusiano wenu utavunjika mapema…..


  7. Unakubali kila analosema au kila anachokifanya….Kuna kitu kinaitwa ‘uhusiano wa kinyonga.’ Hapa mwanamke anajibadili kupita kiasi ili afanane na mwenzi wake. Unakuta mwanamke anakubali kila kitu anachokiamini mwenzi wake bila kuhoji. Anapoteza utambulisho wake na kujipachika utambulisho wa mwenzi wake. Mwanaume akikuona uko hivyo, atakukimbia, atajua wewe ni king’ang’anizi


  [​IMG]


  8. Unawazungumzia mabwana ulioachana nao kila wakati…
  Kama una kawaida ya kumzungumzia mwanaume uliyeachana naye mara kwa mara uwapo na mpenzi wako mpya, ina maana kwamba bado hujaachana na jakamoyo la kuachwa. Hakuna mwanaume anayependa kusikia kuhusu mahusiano yako ya nyuma, kwa sababu hayamuhusu. Kama ukiwa unapenda kumzungumzia mpenzi wako wa zamani kila uwapo na mpenzi wako mpya, jua kwamba na yeye pia utampoteza kwa sababu atakuona kuwa wewe ni dhaifu na king’ang’anizi na ndio maana umeshindwa kusimama kama wewe, na badala yake unawaza kuhusu mtu uliyeachana naye pamoja na kwamba uko naye. Sio kwamba ni vibaya kumzungumzia mpenzi mliyeachana, lakini ni vyema kama utamzungumzia pale ambapo kuna ulazima sana wa kufanya hivyo, labda kuna jambo ambalo limamhusu ambalo mnajadili, na ikakulazimu kumtaja…..

   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmmhhh, ntarudi
   
 3. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  tukishamaliza hii uje na ya kuwaalert wanaume kuwa wanapofanya mambo gani wanawake tunawaona kuwa ni vinGanGanizi!
   
 4. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Hamuwezi kutuona kuwa ving'ang'anizi kwa sababu ung'ang'anizi kwenu ni kitu positive. Tofauti iliyopo ni kwamba kwa wanaume ung'ang'anizi ni kitu negative, lakini kwa wanawake ni kitu positive. Mking'ang'aniwa ndo mnafurahi na kuona mnapendwa. Ikitokea mwanamke akakuona we king'ang'anizi basi labda hakupendi au hana matarajio yoyote na wewe.
   
 5. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Mkuu, hapo kwenye maswali hapo yaani, dah. Wanakera sana hawa na maswali yao ya jela.
   
 6. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  ukweli mtupu mkuu Mtambuzi.....wadada mjifunze hapa leo...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Inategema na mwanaume....Mimi napenda wanawake kama hao, kidogo point ya mwisho inaweza kunitisha...lakini kama hawaja-sex sijali hata aseme alipendana na Jini :biggrin1:
   
 8. ChaterMaster

  ChaterMaster JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 1,285
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  mkuu m wa kwngu ana cfa zote hzo na mda c mref ntamtema mana imekuwa kero na cdhan km tunafananA
   
 9. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kuna wanaume wanapenda sana kutambulisha wasichana wao kwa mama zao...ila mara nyingi ni dalili kuwa hayuko kupoteza muda. Na ni kweli it feels good ukiwa introduced.

  Ila kuomba mwenyewe eti nitambulishe mbona naona kama haiwezekani...unaanzaje anzaje?

  Na unajua ni ngumu kijana kutambulisha wasichana wengi kwa mama yake; ndio maana inaleta sense ya kuwa kijana yuko serious.

  Kama hayuko serious mbona hata kwa winchi hakutambulishi. Mama yake amuone muhuni?
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  itabidi nipunguze maswali kwa mchuchu kama....uko wapi? mbona kuna mdada anacheka hapo? kwanini unachelewa kupokea simu? nakwambia nakupenda unajibu na mimi pia, uko na mwanamke mwingine nini hapo? mbona hupokei simu zako? kwanini umezoeana sana na huyo dada hapo kazini?
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  leo naorodhesha ving'ang'anizi tu.
  Chukua namba moko
   
 12. N

  Neylu JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Aaah... Usiniteme tafadhali...! Nitaishije bila wewe Mupenziiiiiii!!
   
 13. Haven

  Haven Senior Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Afadhali umesema...maana nyuzi za Mtambuzi zimejaa jinsia yetu..
   
 14. Haven

  Haven Senior Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Well said NK, mwanaume kumtambulisha binti kwa mama yake mara nyingi ni dalili kuwa he's serious and ready to commit to the girl.
   
 15. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,266
  Likes Received: 1,197
  Trophy Points: 280
  kazi ipo...nway thanx nimejifunza kitu
   
 16. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mbona sie wengine hatuko hivyo.....
   
 17. data

  data JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,747
  Likes Received: 6,523
  Trophy Points: 280
  very true
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,094
  Trophy Points: 280
  Mhhhhh! imetulia hii...namba tano imenifanya nitabasamu.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,094
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha haaaaaa nimejua kwa nini umetabasamu..... we are in the same page my bro.....LOL
   
Loading...