Mwanamke auawa kwa kuchinjwa koromeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke auawa kwa kuchinjwa koromeo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 21, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Mwanamke auawa kwa kuchinjwa koromeo


  na Gordon Kalulunga, Mbeya


  [​IMG] WAKATI serikali na asasi za kiraia zikiendelea kupiga vita mila za ukeketeji nchini, wimbi la mauaji limeikumba wilaya ya Ileje mkoani hapa baada ya watu watatu kuuawa hivi karibuni na mwanamke kuchinjwa kikatili. Aliyechinjwa kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili chake ni Tabu Mwashitete ambaye baada ya tukio hilo la kinyama mwili wake uliokotwa katika kijiji cha Chitete kitongoji cha Lusungo.
  Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki ambapo imeelezwa kuwa mwanamke huyo alipatwa na mauti hayo baada ya kutekwa na watu wasiofahamika akitokea katika kilabu cha pombe cha Ikumbilo kisha mwili wake kuokotwa ukiwa umekatwa koromeo.
  “Mwanamke huyu amekutwa akiwa ameuawa kwa kukatwa koromeo lake jambo ambalo linatishia usalama wa wananchi wengi wa eneo hili na wilaya nzima kwa ujumla kutokana na wilaya yetu kuwa nje ya jiji hata habari haziandikwi,’’ alisema mmoja wa viongozi wa eneo hilo (jina tunalo).
  Kwa upande wao, baadhi ya askari polisi wa kituo cha Itumba wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo waliliambia Tanzania Daima kuwa hawawezi kutoa tamko lolote kwa sababu si wasemaji wa jeshi hilo.
  Habari kutoka eneo la tukio zimeeleza kuwa matukio ya kikatili ya namna hiyo siyo mageni katika eneo hilo hususan katika kata ya Chitete na Ukinga ambapo hivi karibuni wanaume wawili wameuawa kikatili kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hata huyu mama lazima itakuwa ni masuala ya mapenzi na kuchanganya watu!
   
Loading...