Mwanamke atumia ARV miaka tisa bila ukimwi; Fidia Yake Sawa na 2.5 Billion Tsh.!!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Mwanamke atumia ARV miaka tisa bila ukimwi

*Alipwa fidia Sh 2.6 bilioni

BOSTON, Marekani

MWANAMKE mmoja, Audrey Serrano amelipwa fidia ya Dola za Marekani milioni 2.5 (zaidi ya Sh 2.6 bilioni za Tanzania) kutokana na makosa ya madaktari yaliyoonyesha kuwa ana virusi vya ukimwi na kutumia dawa kwa miaka tisa wakati hakuwa ameambukizwa.

Jumatano ya wiki hii mahakama ya Worcester Superior jijini Boston, Marekani ilimwamuru daktari aliyempima na kutoa dawa hizo mama huyo, kumlipa kiasi hicho cha fedha.

Mwanamke huyo amekuwa akiishi kwa miaka tisa akijua ameambukizwa virusi vya ukimwi kabla hajapima tena na kujikuta hana virusi vya ukimwi na hivyo kumfungulia mashtaka daktari huyo.

Katika kesi yake ya madai mwanamke huyo alisema kuwa, amepata madhara makubwa mwilini mwake kufuatia kutumia mchanganyiko wa dawa za kuongeza siku, ikiwemo kuvimba tumbo, kupungua uzito, msongo na uchovu wa mwili.

Alifafanua kuwa alipungua uzito kutokana na wasiwasi kuwa muda wowote anaweza kufariki kutokana na kuugua ugonjwa wa ukimwi.

Wakili wa mwanamke huyo, David Angueira aliieleza mahakama kuwa makosa hayo ya kitabibu hakuwahi kuyaona na daktari aliyemhudumia mteja wake alimpa mgonjwa dawa kwa kuangalia historia yake badala ya kujali vipimo.

Wakati wa kesi, mshtakiwa, Dk Kwan Lai, alijitetea kuwa mama huyo alipofika kupima alimueleza kuwa aliwahi kujihusiha na ukahaba, mumewe alikufa kwa ukimwi na kwamba alikuwa anaumwa kifua, ambacho kinahusishwa na ukiwmi.

Hata hivyo, mwanamke huyo alikana kuwahi kujihusiaha na ukahaba lakini akakiri kuwa bwana wake alikuwa na virusi vya ukimwi. Pia alikana kumueleza daktari kuwa alikuwa anaumwa kifua.

Mwaka 2003 mwanamke huyo alipima virusi vya ukimwi baada ya mpenzi wake kufariki kutokana na ugonjwa huo mwaka 1994.

�Ninakwenda kumalizi masomo yangu na nitaendelea kuwasaidia watu wengine, Serrano alilieambia Shirika la Habari la AP kwa njia ya simu na kufafanua kuwa atamtafuta daktari mwingine wa kumsaidia.

Mama huyo alikuwa akiugua ugonjwa wa kifua na hivyo kulazimika kupima virusi vya ukimwi Januari 4, 2004 na majibu yalipotoka yalionyesha kuwa ameathirika kwa ugonjwa huo.

Aidha wakili wa mwanamke huyo alidai fidia ya dola za Marekani 3.7 milioni ikiwa ni pamoja na fidia ya usumbufu alioupata mwanamke huyo kutoka kwa jamii, lakini mahakama ikaidhinisha Dola 2.5 milioni.

Source link: Mwananchi.

SteveD.
 
Mimi ninaona tatizo ni system failure. Mtu kuanzishiwa dawa za kurefusha maisha inabidi apitie hatua zifuatazo:
1. Apimwe na kuthibitika ameambukizwa
2. Mgonjwa huanzishiwa Dawa pale CD4 zinapopungua na kufukia 200-300 kutegemea cut off point ya nchi.
Vile vile wakati mgonjwa anaendelea na matibabu, CD4 levels zinatakiwa kuwa-monitored kila baada ya miezi 3-4.
Kwa nchi zilizoendelea, Viral load hupimwa angalau mara moja kwa mwaka.
Inashangaza kwa miaka yote tisa, hakuna aliyeweza kuona mapungufu haya.
Madawa haya ni makali na ndio maana yanahitaji close monitoring.
Mama huyu ana haki ya kumshtaki Daktari huyu kwa kutokuwa makini. Sio tatizo la bahati mbaya, ila kuna uzembe ulifanyika.
 
Mimi nadhani kuna tatizo linahitaji utafiti zaidi. Pengine baada ya kutumia dawa kwa miaka 9 amepona, ndio maana ameonekana hana tena hiyo HIV, au mnadai hilo haliwezekani? Hii kwangu ni fursa ya kiutafiti, ningeshauri wataalamu warudi wakawapime tena wale wagonjwa waliotumia hizo ARV kwa miaka 9 na zaidi, si ajabu wakakuta wengine wengi tu waliopona, na hii ikawa habari kubwa kwenye fani ya tiba! Au mnasemaje wakuu? Wataalamu wa tiba mlioko kwenye hii foramu hebu jibuni changamoto hii: haiyumkiniki huyo mama alipona hiyo HIV?
 
Not possible, kwa kutumia ARVs unaweza kupunguza kiasi cha virusi ulivyonavyo mwilini "Viral load" na kuwa "negligible", lakini ukipima antibodies (Kinga za mwili) lazima zitaonyesha ulishawahi kuambukizwa. This means that the HIV testing will never be negative even you have negligible viral load.
Natumai maelezo haya yatakusaidia.
 
Bado maelezo hayajanisaidia. Nadhani hizo unazosema "antibodies" zinazalishwa na mwili kutokana na kuwepo kwa virus wa HIV mwilini. Maana yake ni kwamba kama hamna HIV, hizo antibodies nazo hazizalishwi, kama HIV load ni kubwa na production ya antibodies inakuwa kubwa pia. Natumia logic tu hapa, ambayo ndiyo inayoongoza hypotheses formulation kabla mtu hajaingia kufanya research ku-test hiyo hypothesis. Kwa hiyo assumption yangu ni direct proportionality between antibody production and HIV load in the blood. Kama ni kweli ARV zinapunguza viral load kama unavyosema, inamaanisha pia zinapunguza antibody production, kwa hiyo zitaendelea kupungua hadi kwenye hatua ya kuwa undetectable (ambayo huko maabara ndiyo inaitwa "negative" au siyo?). Kwenye hesabu tunge-state hivi (kwenye conclusion tunapomalizia ku-derive hii expression): "as HIV load tends to zero, so does antibody production tend to zero, and HIV test result tends to negative".

Utanisamehe kubishana na wewe (yawezekana u mtaalamu wa fani ya tiba, kwa maelezo yako), lakini kwa taaluma yangu ya utafiti na falsafa, naona bado kuna jambo ambalo ama halijafanyika, lau kama lilishafanyika sina habari nalo. Je kuna mtafiti aliye-approach hii issue kwa mantiki niliyoainisha hapo juu? Na kama yupo (au wapo) ni nani, na matokeo yalikuwaje? Waweza kutuwekea reference hapa ili sisi tulio wadadisi zaidi tuweze kujisomea?
Asante.
 
Bado maelezo hayajanisaidia. Nadhani hizo unazosema "antibodies" zinazalishwa na mwili kutokana na kuwepo kwa virus wa HIV mwilini.
CORRECT
Maana yake ni kwamba kama hamna HIV, hizo antibodies nazo hazizalishwi, kama HIV load ni kubwa na production ya antibodies inakuwa kubwa pia.
PARTLY CORRECT. THERE MIGHT BE AN INCREASE IN ANTIBODIES IN EARLY INFECTION. MIND YOU, THE INFECTION DOES DESTROY THE SAME ANTIBODIES. THEREFORE UNTREATED THE ANTIBODIES LEVELS TEND WITH PROGRESSION OF THE INFECTION
Natumia logic tu hapa, ambayo ndiyo inayoongoza hypotheses formulation kabla mtu hajaingia kufanya research ku-test hiyo hypothesis. Kwa hiyo assumption yangu ni direct proportionality between antibody production and HIV load in the blood.
SEE ABOVE
Kama ni kweli ARV zinapunguza viral load kama unavyosema, inamaanisha pia zinapunguza antibody production, kwa hiyo zitaendelea kupungua hadi kwenye hatua ya kuwa undetectable (ambayo huko maabara ndiyo inaitwa "negative" au siyo?). Kwenye hesabu tunge-state hivi (kwenye conclusion tunapomalizia ku-derive hii expression): "as HIV load tends to zero, so does antibody production tend to zero, and HIV test result tends to negative".
NOT TRUE: THE BODY OS PROGRAMMED IN SUCH A WAY THAT WHEN THERE IS SOMETHING FOREIGN, IT DEVELOPMENT A DEFENCE MECHANISM (ANTIBODIES), EVEN AFTER RESOLUTION OF THE INFECTION, IT RETAINS THIS MEMORY FOR SUBSEQUENT INFECTIONS. IN SOME INFECTIONS SUCH AS SYPHILIS, ONCE YOU HAVE BEEN INFECTED, YOU WILL TEST POSITIVE FOR LIFE DUE TO THIS MEMORY CREATED.
Utanisamehe kubishana na wewe (yawezekana u mtaalamu wa fani ya tiba, kwa maelezo yako), lakini kwa taaluma yangu ya utafiti na falsafa, naona bado kuna jambo ambalo ama halijafanyika, lau kama lilishafanyika sina habari nalo. Je kuna mtafiti aliye-approach hii issue kwa mantiki niliyoainisha hapo juu? Na kama yupo (au wapo) ni nani, na matokeo yalikuwaje? Waweza kutuwekea reference hapa ili sisi tulio wadadisi zaidi tuweze kujisomea?
Asante.

Nitakutafutia references for further reading
 
Nitakutafutia references for further reading

Ndugu Dotori bado nasubiri hizo references ulizoniahidi. Katika falsafa tunaamini kuwa hakuna kweli za kudumu (absolute facts don't exist), kwa hiyo hayo uliyonijibu kwamba ati "CORRECT" mengine ukayaita "NOT TRUE", inaweza ikapatikana proof nyingine kuonesha kwamba ni kinyume chake. Na kuonesha Falsafa ilivyo sahihi, historia pia imethibitisha haya. Kumbuka kuwa falsafa ndiye muumbaji wa sayansi. Kabla ya enzi ya Galileo Galilei (aliishi kati ya mwaka 1564 na 1642), iliaminika na kukubalika kwamba ni FACT kuwa jua huizunguka dunia, na kauli kinyume cha hapo iliitajwa na wanasayansi wa kipindi hicho kwamba ni UONGO (kama ulivyosema "NOT TRUE"), lakini sasa wanasayansi kote ulimwenguni wanakubaliana na kinyume chake. "FACTS" nyingi za akina Isaac Newton na John Dalton zilikuja badilika sana baada ya mafikara na tafiti mpya za kina Albert Einstein na Ernst Rutherfold. Kwa hiyo bado miye naamini hayo unayotueleza kuhusu antibodies na HIV na vitu vinavyofanana hivyo, bado hazijawa absolute facts wala hazitakuwa, maana elimu inaendelea, utafutaji wa knowledge unaendelea, na mojawapo ya fursa za kutafuta knowledge zaidi ni huyo mama aliyetibiwa HIV kwa miaka 9 na sasa "amepona". Kwa kuwa hadi sasa hakuna ushahidi kwamba alikuwa HIV negative alipoanza dawa, sioni mantiki ya kupinga huu uwezekano kwamba HIV ilikuwako mwilini mwake na sasa haipo. Nakushauri ndugu Dotori, hebu jiruhusu kufikiri beyond the books you have read, utaiona hii potentiality ninayozungumzia, it is a research opportunity, na nitashangaa sana kama madaktari wenye MD zao na wanasayansi-uhai (biological scientists) wenye PhD zao hawataiona hii waichangamkie. Kuna mwenzetu humu ndani ana signature inayosema wasomaji wa vitabu ni wengi lakini watu wenye kufikiri (thinkers) ni nadra kupatikana. Madaktari wetu, jitoeni humo, msikariri tu kwamba ati kitu kikiwa hivi basi chatibiwa vile, hapana! Twahitaji kutumia kila nafasi inayopatikana ya kuboresha ujuzi uliopo.

Kwa hiyo changamoto yangu kwa madaktari wa matibabu (nadhani ndo kiswahili cha medical doctors, au?), nawachagiza mje na ushahidi hapa unaoonesha huyo mwanamke hakupona HIV! Mie hypothesis yangu ni kuwa alipona baada ya kutumia dawa kwa miaka 9, na inawezekana wako wengine waliopona hivyo, kwa hiyo ningekuwa katika nafasi yenu ningeandika pendekezo (proposal) ya kufanya utafiti wa ku-test hiyo hypothesis. Haya miye sio daktari, lakini hoja yangu ndio hiyo, nawachagiza madaktari wa tiba walete majibu ya kuridhisha. Karibuni.
 
Kithuku,
Simple, kwanza HIV ni RNA viruses. Hiyo story nyingine ndefu. Antibodies zinakuwepo baada ya infection nyingi wether bacterial or virus, maana yake ni kwamba body ina-recognize infection hiyo. Ktk issue ya HIV ukisema kwamba ni negligible maana yale ni kwamba viral load ni ndogo kuweza kuleta madhara lakini ipo incase kwamba ukiacha medication basi inaweza kuwa balaa. Ni kama Hepatitis C au B once you have it then its for life, ni suala la management tu ili isiwe full swing.......viral load ya ngoma ikiwa chini ya let say 2000mm3, basi ni poa lakini si kwamba huna tena.

Well, sidhani kama hiyo inatosha lakini inaweza kutoa idea.
Thanx.
 
Nashukuru Ndugu Kithuku kwa maelezo na changamoto zako.
Naomba kwanza niombe radhi kuwa mie sio mtaalamu wa Falsafa. Ila ninachofahamu ni kuwa wakati mwingine medical science na philosophy haviendani.
Kwanza, Tukianzia kwa huyu mama, Hii ni typical case of mismanagement. Makosa hufanyika katika utabibu (Refer to case ya MOI), lakini Daktari husika kama angekuwa makini alikuwa na nafasi ya kugundua kuwa alim-diagnose wrongly huyu mama. Kwani mgonjwa wa UKIMWI kama nilivyosema awali anatakiwa kuwa monitored regularly. Vipimo vingeonyesha normal CD4 range na kwa kuwa hakuwa na HIV basi the viral load ingekuwa negative au negligible.
Pili, Viral diseases are not treatable. Most are self limiting. Hakuna dawa inayoua vizuri. "Viruses have to strictly depend on living cells for replication. The narrow margin between the therapeutic dose of antiviral agents and lethal dose to the cells themselves is one of the major problems encountered in the development of viricidal drugs". Dawa zilizopo zinatumia mechanisms zifuatazo:
1. Kuzuia virusi visiingie ndani ya cells.
2. Kama vikiingia, basi dawa inazuia visizaane
3. Na kama vikizaana, dawa zinazuia visitoke ndani ya cells
Body defense mechanisms ndio inayoclear the infection.
Tatu, Virusi vya HIV vinashambulia kinga za mwili ambazo zinapaswa kukulinda dhidi ya maradhi na hivyo kuhurusu magonjwa nyemelezi (Opportunistic infections) kushambulia.
Kama nilivyosema awali, mtu anapopatwa na infection yoyote ile, body defense mechanisms tend to mount an attack(Create antibodies). Whether the infection has been resolved or not, the antibodies will retain the memory of this attack or infection. Kwa wataalamu wanaweza kujua kama hii ni recent infection au past infection kwa kuangalia aina ya antibodies in circulation, IgM huashiria recent infection na IgG past infection.
IgM huwa ni short lived and IgG tend to persist. Kinachopimwa katika HIV ni IgG.Therefore is one is infected, he/she is infected for life

Natumai maelezo haya yatasaidia kukuelewesha zaidi.
http://www.bmj.com/cgi/reprint/322/7297/1290
http://www.avert.org/testing.htm
http://www.forbes.com/home/feeds/afx/2007/06/28/afx3868315.html
http://www.natap.org/2005/newsUpdates/090805_09.htm
 
Ndugu Dotori,

Nashukuru kwa maelezo yako na hizo reference ulizoniwekea nitazisoma halafu nitarudi hapa.

Ila nadhani hiyo statement ya kwamba medicine na philosophy haviendani nadhani umepitiwa kidogo, ama umejisahau tu, nataka kuamini kwamba ni kwa bahati mbaya. Umesahau kwamba taaluma yenyewe msingi wake uliwekwa na philosopher maarufu Hippocrates aliyeishi kati ya mwaka 460 na 470 BC, na hata kiapo mnachoapa madaktari (Hippocratic oath) ni yeye aliyekianzisha. Huyu Hippocrates alitumia misingi ya kifalsafa (philosophical principles) kuijenga taaluma hiyo mnayoifurahia hii leo. Misingi mikuu ya falsafa ni Ethics, Aesthetics, Epistemology, Logic na Metaphysics, kama una nafasi angalia tu kwa kifupi hata kwenye web misingi hii inahusu nini, na utagundua kwamba taaluma ya utabibu ndicho inachohitaji, na ndicho matabibu maarufu wa zamani (wa kihistoria tuseme) walichosimamia. Wapo kina Galen, Avicenna (au Ibn Sina, alikuwa mwarabu huyu, tofauti na wenzie wengi ambao walikuwa wagiriki), na philosophers wengine wengi ambao ndio walioweka misingi ya kuiweka taaluma yenu hapo ilipo. Hata Akina Aristotle na Socrates wamechangia mengi sana katika medicine. Kwa hiyo ndugu yangu Dotori falsafa ndio mzazi wa sayansi zote na elimu yote ulimwenguni, ikiwemo hiyo ya tiba, na nyingine kama uhandisi, sheria, uchumi, utawala, Eli-Mungu (Theology), sema chochote utakuta misingi ya falsafa ndani yake.

Narudia kushukuru, nikishamaliza kusoma hizo rejea ulizoniwekea hapo nitarudi, usinichoke ndugu yangu, maana kujua vitu ni starehe ya pekee. Nafurahi kukutana na watu ambao wako tayari kushughulika na changamoto za kiakili, na kufanyia akili zetu mazoezi ya kufikiri na kupambanua.

Mlipotea hamkurud tena..
 
Not possible, kwa kutumia ARVs unaweza kupunguza kiasi cha virusi ulivyonavyo mwilini "Viral load" na kuwa "negligible", lakini ukipima antibodies (Kinga za mwili) lazima zitaonyesha ulishawahi kuambukizwa. This means that the HIV testing will never be negative even you have negligible viral load.
Natumai maelezo haya yatakusaidia.

Ndiyo maana aka suggest hii iwe baseline kwa ajili ya Research!
 
Mimi nadhani kuna tatizo linahitaji utafiti zaidi. Pengine baada ya kutumia dawa kwa miaka 9 amepona, ndio maana ameonekana hana tena hiyo HIV, au mnadai hilo haliwezekani? Hii kwangu ni fursa ya kiutafiti, ningeshauri wataalamu warudi wakawapime tena wale wagonjwa waliotumia hizo ARV kwa miaka 9 na zaidi, si ajabu wakakuta wengine wengi tu waliopona, na hii ikawa habari kubwa kwenye fani ya tiba! Au mnasemaje wakuu? Wataalamu wa tiba mlioko kwenye hii foramu hebu jibuni changamoto hii: haiyumkiniki huyo mama alipona hiyo HIV?
Nilisha shuhudia kwa macho yangu mtu mmoja ambaye anatumia ARV kwa miaka 9 sasa mwaka juzi alipimwa tena maambukizi ya VVU kwa lengo la kuhakiki ubora wa vitendanishi majibu yalikuwa ni non reactive kwa vyote determine na unigold ingawa kit hizo hizo zilionesha majibu sawia kwa watu wemgine wenye VVU.

Bahati mbaya hakukuwa na mtu wa kusaidia ku check viral load au DBS hivyo ilizaniwa labda viral load imeshuka sana kiasi cha kinga za mwili kushindwa Ku detect uwepo wa VVU ili kuzalisha antibodies za kusomwa na hizo HIV rapidly test.

Binafsi nafikiri kazi ya kutafuta matukio kama hayo na yale ya watu wanao ji exposure kwa wenye VVU kwa miaka mingi lakini bila kuambukizwa iendelee labda kuna kitu tutagundua mbele ya safari.
 
Mimi ninaona tatizo ni system failure. Mtu kuanzishiwa dawa za kurefusha maisha inabidi apitie hatua zifuatazo:
1. Apimwe na kuthibitika ameambukizwa
2. Mgonjwa huanzishiwa Dawa pale CD4 zinapopungua na kufukia 200-300 kutegemea cut off point ya nchi.
Vile vile wakati mgonjwa anaendelea na matibabu, CD4 levels zinatakiwa kuwa-monitored kila baada ya miezi 3-4.
Kwa nchi zilizoendelea, Viral load hupimwa angalau mara moja kwa mwaka.
Inashangaza kwa miaka yote tisa, hakuna aliyeweza kuona mapungufu haya.
Madawa haya ni makali na ndio maana yanahitaji close monitoring.
Mama huyu ana haki ya kumshtaki Daktari huyu kwa kutokuwa makini. Sio tatizo la bahati mbaya, ila kuna uzembe ulifanyika.
Siku hizi ukipima ukawa positive tu unaanzishiwa dawa haraka. Sasa kama kuna makosa kama haya ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom