Mwanamke atalikiwa siku ya fungate baada ya mumewe kumuona kwa mara ya kwanza bila vipodozi

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Mwanamke mmoja anayetokea katika jimbo la Mpumalanga nchini Afrika Kusini amepewa talaka na mumewe siku ya fungate (honeymoon day) baada ya mume kuona sura ya mkewe kwa mara ya kwanza bila kupodolewa.

Bwana harusi alidai kuwa mkewe amemfanyia udanganyifu kwa kuwa na sura bandia, kope bandia na uso uliorembwa sana kiasi cha kushindwa kumtambua siku mkewe alipokutananaye bila kutumia vipodozi.

Wawili hao ambao walikutana Facebook wamekuwa katika uhusiano kwa miezi 3 kabla ya kufunga ndoa mapema mwezi huu lakini kwa kipindi chote hicho mume hakuwahi kumuona bibiye bila makeup.

Baada tu ya harusi, bibi harusi alipata ushauri wa kitabibu kutotumia tena vipodozi mana vinamwaathiri afya na akili yake ndipo alipoamua kuacha siku wakiwa fungate.

Mumewe anadai kuwa alipomwona mkewe asubuhi alishtuka akidhania amevamiwa na mtu mwingine lakini mkewe alikaza kuwa asiogope maana ndiyo yeye ila daktari amemshauri asitumie vipodozi.

FB_IMG_15766941540874144.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1296587

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata ningekuwa mimi ningemuacha kwa kweli.
 
Back
Top Bottom