Mwanamke asiyejaliwa na Mume wake ni sawa na Nchi isiyotawalika

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,712
26,039
Assalamu Alyekum!

Mwezi February ulikuwa mwezi wa wapendanao. Nikasema mwezi huo nitautumia kukutana na Mabazazi, washenzi, maharamia, wateka Manuwari na nyambizi, Pia nikakutana na wakata umeme, mabuzi, wazama uvinza, wanaapolo, wabambikaji, wanakemia na Aina zote za watu wapendao ngono, zinaa, uasherati, ufisadi, ufuska, ubakaji, na wote wanaoharibu ndoa za watu Kwa kuchukua wake za watu.

Jopo la kundi hilo nilipokutana nalo, halikufurahishwa na ujio wangu. Hata hivyo nilifanikiwa kuwatoa hofu kwani nami nilitaka nijiunge Katika jumuiya Yao ya madola. Baada ya kunipa utaratibu wa kujiunga na jumuiya Yao. Nikaridhishwa na taratibu zao. Mambo machache niliyoyapata huko ni pamoja na wao kuwa na mbinu za kimedani za kumtambua mwanamke ambaye hayupo chini ya uangalizi mzuri(mume wake hamjร li).

Naambiwa kuwa mwanamke asiyejaliwa na mume wake vizuri ni Kama nchi ambayo serikali imeshindwa kutawala.
Yaani nchi haitawaliki licha ya kuwa na serikali. Wanajumuiya wananambia kuwa Mwanamke asiyejaliwa na mume wake ni Kama nchi ya Congo huko Kivu ya Kaskazini, wakaongeza kuwa nchi isiyo na Serikali Imara husababisha kuinuka Kwa vijikundi mshenzi vya waasi na wahuni kufanya watakavyo.

Naambiwa hapa kuwa; wahuni huweza kuingia mpaka Ikulu ya nyumba(chumba cha mwanaume asiyejali) na kupora amali za nchi Kama sio nyara za serikali. Basi wanamboyoyo wakaniambia ati Kama nikijiunga na Dola lao, Dola la pekechua, sasambua, kisha pepetua; nitaweza kuteuliwa na kupewa Keki ya taifa. Naambiwa hapa ati nitaweza kutumia magari ya serikali ya madola bure, Mafuta bure,
Nikamuuliza; vipi na Hawa waume zao ambao ndio maraisi wa majimbo haya.

Nikajibiwa, hakuna mwanaume atakayeweza kuwa na nguvu kwenye Jimbo lake pasipo kumjali malkia wa nchi hiyo. Kitendo cha wao kushindwa kulihudumia Jimbo na kulijali basi ni wazi hawana ubavu wa kupambana na vikundi vya waasi. Nikauliza, sasa Mimi bado sio mzoefu, haya mambo yataniwia magumu. Mtanisaidiaje?

Wakanijibu, jumuiya ya madola ya maharamia, wachochea Moto wa jehanamu, itakusaidia kukuazima magari ya kifahari Kama utahitaji Kwa miaka mitatu, pia itakusaidia kukupa ofa za sehemu za Hoteli na Lodge nzuri Kwa kuliteka Jimbo. Jumuiya itatoa ufadhili wa Madawa ya kivita ya Mundende na Mkongo kukamilisha shambulizi la kuiteka Himaya.

Nikaridhika, lakini nikakumbuka,nikawauliza hivi; nitajuaje kuwa Jimbo hili serikali yake ni dhaifu na ninaweza anzisha mapinduzi ya kulikamata Jimbo. Ndipo wakanijibu kuwa mwanamke asiyejaliwa na mumewe atakuwa na moja au mbili ya Dalili Kati ya hizo;

1. Nywele mbofu mbofu,misuko ya minyoosho twende kilioni. Na zinakaa mpaka miezi miwili mitatu.
Naambiwa moja viashiria vya kuwa huyu Mwanamke ni nchi isiyotawalika, yaani serikali yake imeshindwa kutawala ni kuangalia kichwa chake tuu kitatoa majibu yote.

Wanajumuiya wananambia hapa kuwa endapo mwanamke akiwa Hali Tete kichwani, basi Mimi naweza kuiangusha Dola hilo hata na Ubua wa muhindi achilia mbali Rungu.


2. Nguo zilizofubaa na mtumba.
Taikon sikuamini walivyoniambia lakini ndivyo walivyosema. Ati wakaniambia uliona wapi nchi inaongozwa wakati bendera zimechakaa na kufubazwa na ukale; jua likizichoma na mvua zikizinyeshea.

Naambiwa Mwanamke akivaa marapurapu, ni hatari Kwa utawala huo kupindulikuwa na vijikundi vya waasi hata waendesha Bodaboda tuu wakiandamana wanachukua nchi.

Ati nikifika, cha Kwanza nipeleke zawadi ya nguo mpya nzuri nimpe, kisha nimwambie akazijaribu pia nimwambie ninaimani Itampendeza kutokana na uzuri wake uliofubazwa na serikali dhalimu iliyoshindwa kumtunza. Siku akizivaa nimsifie Kwa mapambio na masanturi.

Tena nikaambiwa na Hawa wahuni kuwa mwanamke anapenda viatu vizuri, urembo WA kuvaa Kama hereni nzuri, cheni na bangili. Tena nisisahau Bangili. Kisha nimsifie akizivaa kuwa amegeuka Malaika aliyekuja kutalii huku duniani. Hakika ni mzuri na anavutia Kama kitu kitamu,

Taikon nikaona hizi notes lazima nikazinukuu Kama zilivyo.

3. Mwanamke ambaye anamiezi Kama sio miaka hajatolewa Out Kula Raha.Nikauliza sasa nitajuaje kuwa mwanamke huyu hajatolewa out muda mrefu. Washikaji wakanicheka Sana. Wakasema Taikon Mimi ni mshamba Sana Kwa kutojua vitu vidogo.
Nikakubali, sasa ningefanyaje na Taikon ndugu yenu ni mshamba kweli wa Makanya huko.

Wakaniambia; mwanamke ambaye hajatolewa out siku nyingi anadalili zifuatazo;
1. Sanduku lake la nguo limejaa Madera mengi na marapurapu tuu. Wakaniambia Out huwezi toka na Dera.

2. Hana Marashi wala Mafuta mazuri.
Naambiwa hapa kuwa Out zinaendana na Mafuta na Marashi anayotumia mtu. Ati mtu Kama ananuka uvundo Kwa kukosa Mafuta mazuri ni Dalili kuwa hajatolewa out miezi mingi Kama sio miaka. Nikaikataa hiyo pwenti, wakasisitiza. Ati mwanamke kama anapaka Mafuta na marashi Kwa pamoja yasiyozidi elfu 20 ujue huo utawala umedondoka. Yaani Mafuta ya kupaka angalau yazidi elfu 10 na marashi yazidi 10 chini ya hapo hawezi tolewa Out.

Nikabaki mdomo wazi, nikasema; sasa Sisi wanaume masikini tutaishije sasa na wake zetu? Wakajibu tuu Kwa ufupi, wanaume masikini ni Kama watawala WA nchi za Afrika, wao lazima wakubali Misaada toka nchi tajiri tena Kama nchi zao zinamigodi na Mali nyingi. Ati msaada utapewa endapo mwanamke uliyenaye ni mzuri na anaamali na rupia zinazotafutwa na wanakale.

3. Kuagiza chipsi. Mayai na kuku au Wali kuku.
Naambiwa kuwa ati sababu nyingine inayoashiria mwanamke hajatolewa out miezi nenda ikarudi ni vitu atakavyoagiza.
Nikabaki nimeduwaa! Ila niliwapinga kuwatetea, Tuendelee;

3. Kuzuiwa STAREHE.
Wanajumuiya wakaniambia moja ya STAREHE kubwa ya Mwanamke baada ya urembo basi ni chakula kitamu na kizuri.
Wanaongeza Kwa kusema; wanawake wanapenda vitu vitamu, vinywaji vitamu na vitu vya kumung'unya na kunyonya view vitamin.
Naambiwa pia wanawake wanapenda Kula nyama choma na Aina zote za nyama na mayai. Hapa nikacheka mno.

Naambiwa Mwanamke aliyezuiwa Kula nyama na vitu vitamu ni Sawa na taifa lililowekewa vikwazo vya kiuchumi Kama Urusi. Lazima nchi isitawalike. Naambiwa kitu kinachowafanya wanajumuiya ya madola kuwateka Wake za watu wengi ni tabia za waume wengi Kupenda kupewa minofu ya nyama huku wakiwaachia wake zao vipapatio na miguu. Sasa wakikutana na wahuni wanapewa Kuku mzima kazi kwisha

Wakaongeza kuwa, wanawake wengi Kama sio wote kiasili wanapenda Sanaa za Ghibu, yaani zinazogusa Hisia moja Kwa Moja. Wanawake wote Duniani hupenda Muziki. Nadra Sana kumkuta mwanamke asiyependa muziki. Hivyo wanajumuiya ya Nyota ya Tibeli wakanambia, mwanamke angalau Kwa wiki umuwekee muziki au umpeleke sehemu za Muziki akacheze na kuimba

Naambiwa mwanaume anayeongoza familia yake pasipo kuweka muziki au nyimbo ni Sawa na taifa lisilo na wimbo wa taifa.


4. Mwanamke asiye na pesa zake.
Naambiwa Mwanamke anayeomba kila sumni kutoka Kwa mume wake ni Sawa nchi isiyo na Benki. Mwanamke asiyezoeshwa kushika pesa siku akishikishwa ni Sawa na jambazi lililoshikishwa silaha. Mwanamke anamahitaji yake mengi tuu ingawaje ni madogo madogo lakini ndio ya Msingi na ndio yanayomfanya awe Mwanamke. Kuomba omba Kwa mwanamke kila saa ni Sawa na kesi ya Madai mahakamani.

Mwanamke lazima umtengee Fungu lake la pesa Kwa ajili ya matumizi yake binafsi. Vinginevyo wanajumuiya wananiambia wanamkagua mwanamke na kumfanyia tathmini. Kisha Kama humpi pesa za matumizi yake binafsi, wao hutoa. Taikon niliyapata mengi kutoka Kwa Wateka vimondo. Kutokana na andiko kuwa Refu mniruhusu niishie Hapa.

Nikikamilisha Ada ya uanachama nitawapa ya ndani niliyofichwa kwani bado sijawa mwanachama.

Ni Yule Mtibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kihonda, Morogoro
 

nduza

JF-Expert Member
Feb 7, 2019
1,598
2,415
Nikajua lengo la kabinet uliyokutana nayo ni Kupeana mbinu za kujua wanawake wenye maisha yao safi wake za vigogo waliokosa upendo kwenye ndoa zao na jinsi ya kuwateka, Kumbe unaongelea hawa ambao hata hela ya kuweka nywele sawa hawana

Sasa tutumie nguvu yote hiyo ya nini yani lengo ni kuipata mbususu tu? Hizi zilipendwa mkuu

Nchi imevaa sketi hii tupeane mbinu za kuchukua hela zao kilaini

Yani nifanye yote hayo mpaka kuazima magari ikibidi hotel bila kutegemea faida ntakuwa nimeumia mimi
 

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,712
26,039
Nikajua lengo la kabinet uliyokutana nayo ni
Kupeana mbinu za kujua wanawake wenye maisha yao safi wake za vigogo waliokosa upendo kwenye ndoa zao na jinsi ya kuwateka
Kumbe unaongelea hawa ambao hata hela ya kuweka nywele sawa hawana
Sasa tutumie nguvu yote hiyo ya nini yani lengo ni kuipata mbususu tu
Hizi zilipendwa mkuu
Nchi imevaa sketi hii tupeane mbinu za kuchukua hela zao kilaini
Yani nifanye yote hayo mpaka kuazima magari ikibidi hotel bila kutegemea faida ntakuwa nimeumia mimi


๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

Mkuu huoni aibu kutangaza hadharani habari hii.
 

Mpunange

Senior Member
Apr 17, 2015
108
73
Assalamu Alyekum!

Mwezi February ulikuwa mwezi wa wapendanao. Nikasema mwezi huo nitautumia kukutana na Mabazazi, washenzi, maharamia, wateka Manuwari na nyambizi,
Umeandika kimzahamzaha lakini ndani yake kuna mafundisho ya maana sana kuhusu ndoa!
 

GRANDPUBA

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
733
766
Hapa kuna fundisho kubwa kwa "washkaji" zetu waliooa, kuwatunza wake zao kikamilifu.

Kwa sisi ambao ni "Ma_single Father" na tuliokwishaamua hatuoi, hii haituhusu. Sana sana, labda, tunaweza kujikuta tunakuwa kama waasi tunaovamia majimbo na Serikali huku tukitokea msituni
 

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,712
26,039
Hapa kuna fundisho kubwa kwa "washkaji" zetu waliooa, kuwatunza wake zao kikamilifu.

Kwa sisi ambao ni "Ma_single Father" na tuliokwishaamua hatuoi, hii haituhusu. Sana sana, labda, tunaweza kujikuta tunakuwa kama waasi tunaovamia majimbo na Serikali huku tukitokea msituni

Usikimbie kivuli chako Mzee Baba.

Wanawake ni vivuli vyetu.
 

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,712
26,039
Tufanye nn sasa


Kwa kweli Mkuu nashindwa hata Kueleza.

Ningeshauri hawa wahuni waache tabia zao mbofumbofu, maana Masikini na umasikini hautaisha mpaka mwisho wa Dunia,mwisho wa maisha yetu.

na Sisi waume wenye ndoa tujitahidi Kuwatunza Wake zetu. Nanyi wanawake mjitahidi kutosheka na hali za waume zenu hapo najua kutosheka kwenu ni msamiati Mgeni msioujua.

Mwanamke anatosheka asipokuwa na option nyingine ๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜Š
 

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,712
26,039
Umeandika kimzahamzaha lakini ndani yake kuna mafundisho ya maana sana kuhusu ndoa!


Najaribu kuzungumza na wahuni waache tabia zao za kuanzisha vikundi vya uasi kuzorotesha Amani ya serikali za majimbo tunayoyatawala
 

Mamy K

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
1,474
4,275
Wamesahau kukupa password ya nyuklia, Acha Mimi nikupe...MANENO MATAMU, hapa utapata wanawake wa kwenye utawala uliotetereka na hata ulio imara...Wanawake tunaponzwa na masikio, we msifie, msifie, msifie....unaweza hata kujikuta umekuwa first gentleman fastaaaaaa.
 

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,712
26,039
Wamesahau kukupa password ya nyuklia, Acha Mimi nikupe...MANENO MATAMU, hapa utapata wanawake wa kwenye utawala uliotetereka na hata ulio imara...Wanawake tunaponzwa na masikio, we msifie, msifie, msifie....unaweza hata kujikuta umekuwa first gentleman fastaaaaaa.


๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Hii password ni nyeti mno. Nimeisahau tena ingepaswa kuwa namba moja au mbili.

Wanawake mnapenda sifa Asee! Mnapenda kutukuzwa Kama miungu wadogo.
 

antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
35,022
90,359
4. Mwanamke asiye na pesa zake.
Naambiwa Mwanamke anayeomba kila sumni kutoka Kwa mume wake ni Sawa nchi isiyo na Benki.
Mwanamke asiyezoeshwa kushika pesa siku akishikishwa ni Sawa na jambazi lililoshikishwa silaha.

Mwanamke anamahitaji yake mengi tuu ingawaje ni madogo madogo lakini ndio ya Msingi na ndio yanayomfanya awe Mwanamke.
Kuomba omba Kwa mwanamke kila saa ni Sawa na kesi ya Madai mahakamani.

Mwanamke lazima umtengee Fungu lake la pesa Kwa ajili ya matumizi yake binafsi. Vinginevyo wanajumuiya wananiambia wanamkagua mwanamke na kumfanyia tathmini. Kisha Kama humpi pesa za matumizi yake binafsi,
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Mwanamke anayeomba kila sumni kutoka Kwa mume wake ni Sawa nchi isiyo na Benki..๐Ÿ˜Š
 

Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
13,166
10,586
Kuna walioumbwa kutotawalika, kutopendeka na kutojaliwa

Hata ufanye nini viburi vyao huwapeleka next level

Bahati mbaya wakishavuka 40 wanakimbilia nyumba za ibada, wanakua mabalozi wa kupandikiza chuki against men Kwa wasichana

With the digital revolution- donโ€™t bet anything for or against women
 

Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
13,166
10,586
Wewe mleta mada ni mwanaume lakini kutwa kuandika mambo ya wanawake una genes za kike au ?

Tabia kama hizo za wanaume wanaongelea sana mambo ya kike wanazo mashoga

Yaani Malala ndefu hii kuhusu mambo ya kike hakuna mtu aweza aamini. meandikwa na mwanaume ni lazima awe mwanamke au shoga
Ni dhaifu fulani hivi

Walio Karibu yake watathibitisha
 

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,712
26,039
Wewe mleta mada ni mwanaume lakini kutwa kuandika mambo ya wanawake una genes za kike au ?

Tabia kama hizo za wanaume wanaongelea sana mambo ya kike wanazo mashoga

Yaani Makala ndefu hii kuhusu mambo ya kike hakuna mtu aweza aamini. meandikwa na mwanaume ni lazima awe mwanamke au shoga


Huwaga sibishani na maoni ya mtu.

Upo sahihi Kwa Uelewa na akili yako.
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom