Mwanamke apigwa na Mumewe hadi kuzirai kwa kushiriki Sensa 2012

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
HabariLeo, SHINYANGA – Mkazi wa Ndembezi mjini Shinyanga amepigwa na mumewe hadi kuzirai na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu baada ya kutoa ushirikiano kwa karani wa Sensa ya Watu na Makazi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Evarist Mangala, alisema jana kuwa mwanamke huyo, Esther Zablon (40) alipigwa juzi saa mbili asubuhi baada ya mumewe, Ismail Yahya kupata taarifa kuwa karani wa sensa alifika nyumbani kwao na mkewe kukubali kuhesabiwa na kutoa takwimu za familia yao.

Akisimulia, Kamanda Mangala alisema karani huyo alipokwenda nyumbani hapo, mume hakuwapo na kama mkuu wa kaya, Esther akazungumza na kutoa taarifa.
Alisema baada ya mume kurudi nyumbani na kugundua kuwa mkewe alikubali kuhesabiwa, alimshambulia kwa ngumi na mateke na kusababisha mke huyo kupoteza fahamu.
Kutokana na kipigo hicho, kwa mujibu wa Kamanda Mangala, Esther alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa kwa uchunguzi na matibabu.
“Wakati mwanamke huyo akichukua fomu namba tatu ya Polisi (PF3) kituoni kabla ya kufikishwa hospitalini, huku akilia kuwa sababu ya kipigo ni yeye kukubali kuhesabiwa, jambo ambalo ni kinyume na msimamo wa dini ya mumewe (Uislamu),” alisema Kamanda Mangala.
Hata hivyo, Kamanda alisema Esther alitoroka wodini kwa kuhofia mumewe kukamatwa na hatimaye kufungwa.
Kamanda Mangala alisema Polisi wanaendelea kumtafuta Yahya na akipatikana atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.

Source: www.wavuti.com
 
Angalia kina Sheick Ponda walivyofanikiwa kugawanya hata ndugu watanzania kwa vigezo vya udini!Mke ni mkristo,walishi kwa amani,sasa ona haya.Na hii ni kwa wanandugu kabisa,vipi kuhusu marafiki na watu baki.Udini umeshaingia,I don't see how we'll fix it.It might be too late!
 
Mkazi wa Ndembezi mjini Shinyanga amepigwa na mumewe hadi kuzirai na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu baada ya kutoa ushirikiano kwa karani wa Sensa ya Watu na Makazi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Evarist Mangala, alisema jana kuwa mwanamke huyo, Esther Zablon (40) alipigwa juzi saa mbili asubuhi baada ya mumewe, Ismail Yahya kupata taarifa kuwa karani wa sensa alifika nyumbani kwao na mkewe kukubali kuhesabiwa na kutoa takwimu za familia yao.
Akisimulia, Kamanda Mangala alisema karani huyo alipokwenda nyumbani hapo, mume hakuwapo na kama mkuu wa kaya, Esther akazungumza na kutoa taarifa.
Alisema baada ya mume kurudi nyumbani na kugundua kuwa mkewe alikubali kuhesabiwa, alimshambulia kwa ngumi na mateke na kusababisha mke huyo kupoteza fahamu.
Kutokana na kipigo hicho, kwa mujibu wa Kamanda Mangala, Esther alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa kwa uchunguzi na matibabu.
"Wakati mwanamke huyo akichukua fomu namba tatu ya Polisi (PF3) kituoni kabla ya kufikishwa hospitalini, huku akilia kuwa sababu ya kipigo ni yeye kukubali kuhesabiwa, jambo ambalo ni kinyume na msimamo wa dini ya mumewe (Uislamu)," alisema Kamanda Mangala.

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
Kwanini huyo mume asingebaki nyumbani ili awakatalie watu wa sensa wasimuhesabu,***** tu huyo
 
misimamo mingine ni ya kijinga sana, kumpiga mke kisa kakubali kuhesabiwa! anajua thamani ya mwanamke huyo? nawapenda sana kina mama kwsbb hakuna kama mama.Huyo mwanaume pamoja na wanaume wengine wote wanaonyanyasa kina mama WALAANIWE KABISA na maisha yao yawe ya mikosi kwa kila wanachofanya.
 
Back
Top Bottom