Mwanamke anayetuhumiwa kuhusika na mauaji adaiwa kuuwawa akiwa mahabusu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke anayetuhumiwa kuhusika na mauaji adaiwa kuuwawa akiwa mahabusu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Feb 21, 2009.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kuna tetesi kwamba yule mwanamke mwenye asili ya kiasia, miaka 23, ambaye yeye na mumewe, miaka 23, amefariki dunia baada ya kuteswa na askari polisi na magereza akiwa mahabusu jijini Dar es Salaam, kwenye mojawapo ya magereza ya Keko, Segerea au Ukonga, ambapo alikuwa amewekwa chini ya ulinzi.

  Inadaiwa kwamba, katika kujaribu kupata habari zaidi kutoka kwa mwanamke huyu kijana kabisa, ambaye alionekana kuwa na hofu iliyozidi kipimo alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, askari hao walitumia njia ambazo zimepigwa marufuku katika upelelezi, njia ambazo hata kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeharamishwa. Njia zinazosadikiwa kutumiwa ni pamoja na matumizi haramu ya umeme, ambao ulitumika kumpiga shoti mwanamke huyo.

  Chanzo cha habari hizi ni ndugu wa kiume wa mfanyabiashara aliyeuwawa na wanandoa hao, ambaye amesikika na kunukuliwa akipasha habari za kufariki kwa mwanamke huyo, huku akidai kwamba kuna njama za kuficha ukweli kuhusu kifo cha mwanamke huyo kwa kuupeleka mwili wake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili kuweza kudai kwamba mwanamke huyo amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.

  Tunawaomba walio na habari zaidi watusaidie kupata ukweli wa jambo hili, kwani ni aibu. Mara nyingi watu ambao bado hawajathibitika kuwa na hatia wamekuwa wakifariki kwa kipigo na mateso, ama wakiwa mikononi mwa polisi, ama wakiwa mahabusu. Tanzania ni nchi iliyoweka saini kwenye Mkataba wa Haki za Kibinadamu wa Geneva (Geneva Convention on Human Rights). Huu ni ukiukwaji wa haki za kibinadam, ambazo zimeainishwa kwenye katiba.

  Tuutafute ukweli ili haki itendeke. Tusikubaliane na watakaojaribu kuuficha ukweli.

  ./Mwana wa Haki
   
 2. s

  samsekwa Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eeeeeeeeeeh, kwa kweli kuna haja ya kubadilika sasa. Inaelekea bado mbinu za kizamani zinatumika katika kuhoji watuhumiwa. Maskini hata kuthibitishwa kuwa alihusika na kuua hakujafanyioka tayari ameshakufa ! This is too much.
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Kuna haja ya kuwalinda watuhumiwa. Tunahitaji mabadiliko ya katiba, kuweka kifungu cha kumlinda mtuhumiwa. Mfano mzuri ni suala la guarantee on due process and speedy trial na haki za mtuhumiwa lazima zibainishwe kwenye katiba yetu. Huwezi kumweka mahabusu miaka 10 akisubiri mashtaka. Kusema tu kwamba a suspect is innocent until proved guilty haitoshi.

  Suala jingine ni kumlinda mtuhumiwa katika suala la kukusanya ushaidi. Katiba lazima iweke wazi kuhusu torture. Tanzania imesaini maazimio mengi kuhusu kupiga vita mateso lakini jeshi lake la polisi linaongoza kwa kutesa watuhumiwa. Inabidi jeshi letu lifundishwe na lifanye kazi kisomi na kisasa zaidi na kuacha kutumia mbinu za karne ya kumi na nane katika kufanya kazi zake. Ebu Unganisha hii na suala la Kina Zombe ndo utajua vyombo hivi vya wizara ya mambo ya ndani vinatufanya tuamini sasa kuwa vinatumia njia za mkato kutatua matatizo. Visitufanye tukaanza kuamini kuwa sasa vimegeka kuwa magenge ya kimafia.

  I strongly disgree with the usage of torture to obtain confession. Courts you have to start not accepting such kind of evidence illegally obtained. There should be the right to have a lawyer present in the time of recording this kind of statement.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I hope sio kweli.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,211
  Trophy Points: 280
  Kusema ukweli tuna very high police brutality in Tanzania. Siku zote polisi wanapoua, huwa wanafanya cover-up. Baada ya zile kesi za Mauaji Mwanza na Shinyanga, kesi ya mauaji iliyohusisha polisi ni ile ya Kombe na Hii kesi ya Zombe inayoendelea lakini kuna mauaji mengi yanayotokea mikononi mwa polisi lakini hayaripotiwi.
  Mwaka jana kuna mtuhumiwa wa ujangili aliyekamatwa na silaha, akawaongoza polisi kuwakamata wenzake wanne wote wakatiwa mahabusu kituo ya Arusha. Kesho yake ndugu walipowatembelea wakaambiwa wote wameuwawa na wananchi wenye hasira. Walipokabidhiwa miili yako, ilikutwa na majeraha ya ajabu!.

  Kama ni kweli na hili limetokea, polisi itakuwa haina jinsi ya kukwepa lawama na sheria kuachwa ichukuwe mkondo wake.
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  kwani sheria zinasemaje mtu akiwa chini ya mahakama, anaweza kuhojiwa na polisi hivi hivi? askari magereza hawahusiki na upelelezi!. inatakiwa polisi waiombe mahakama iwarudishie ndo wanaweza kumchukua na kumhoji? Kama ni kweli basi Mkuu wa gereza awe wa kwanza kuwajibika kwa kumtoa mtuhumiwa na kuwakabidhi polisi bila kibali cha mahakama.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ni katika kutekeleza agizo la Mkuu tu. Ukikutwa umeuawa mtu na kuna ushahidi wa wazi, kwanini tusubiri mahakama? More power to the people!
   
 8. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #8
  Feb 21, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hakuna atakayewajibika kwa hili(kama ni kweli limetokea)!Believe me,huu utamaduni wa kuwajibika hapa Tz umebaki kuwa hekaya!But somehow it makes a bit of sense,kwa sababu let say nmefanya 'madudu' au watu walio under my authority wameshindwa kutimiza wajibu wao 'kizembe!' then watu wakapiga kelele kuwa niwajibike/nijiuzulu mimi nkaziba masikio na aliyeniteua kushika wadhifa huo ananiangalia tu...Then why should I bother with the resignation???Hilo la moral obligation liko low sana bongo,almost halipo.
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mbona watuhumiwa wa wizi wa pesa za EPA hawakuteswa?
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Haraka wenye uwezo toeni ripoti Amnesty International ,watalifuatilia kwa haraka jambo hilo ,na wekeni majina ya huyo binti aliefariki kwa kuteswa ili iwe rahisi kuripoti vile vile jalada la kesi yake siku saa na sababu za kukamatiwa wakiwemo asikari waliomkamata au gereza alilofikishwa ni muhimu.
   
 11. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  mwenye data amwage hapa hili tuweze kuwaandikia Amnesty na mashirika mengine yanayopiga vita 'torture'. I believe we can change things.
   
 12. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Dah, ule mchezo wa koleo na genitals kumbe bado unaendelea!! Angefanyiziwa Mramba hivyo ili atueleze fedha zetu zimetowekea wapi ningeelewa zaidi......
   
 13. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kama suala hili lina ukweli wake, Mh. Masha ana nini cha ku-offer mbele ya UMMA? Someone has to take RESPONSIBILITY for this unthinkable, unspeakable Home Affairs Ministry rubbish.
   
 14. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ni vyema kama tukisubiri maana sidhani kama kesi yao itachukua muda kuitwa tena ndipo tutajua mbivu na mbichi kuliko kuanza kushupali wakati hakuna aliyethibitisha hili.
   
 15. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Brother, huyu hakukutwa akiua, anatuhumiwa kuua hivyo hajamamatwa akiua. ha ha haaaaaa, anyway I know your joking
   
 16. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kweli kabisa mkuu, hivi kwa nini kamchezo haka haramu kakakutumika kwa Zombe,Mramba.Yona Liyumba, watuhumiwa wa EPA has Jeetu Patel.Masha anakesi ya kujibu au yeye dhamana ya Wizara yake inaishia kwenye Tenda kubwa kubwa tu?
   
 17. s

  skasuku Senior Member

  #17
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli kwamba hizi mbinu zakufanya watu waongee zinatumika, kwanini wakina EPA, matumizi mabaya wa madaraka, Liyumbaz et al hawakufanyiziwa. Mbona by now tungekua na upungufu wa mafisadi...

  Jokes aside, taifa letu linakuwa extreme to petty crimes, ila zile za Grand corruption (ambazo sijui zimeua watu wangapi) zina fanyiwa usanii.
   
 18. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nadhani sio kweli. Dah! inasikitisha kama ni kweli.
   
 19. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mtuhumiwa yeyote ni innocent mpaka sheria itakapo prove otherwise. Kama kweli binti amekufa kwa ghafla inabidi ndugu zake wasikubali kuzika maiti hiyo mpaka wajiridhishe na vipimo vyao kwa madaktari bingwa both private na public ili wapate ushahidi wa kutosha kuhusu kifo hicho. Walio karibu na hao nduguze please, wasaidieni.
   
 20. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nimesikia uchambuzi wa mgazeti wanadai habari zisizo thibitishwa alijinyonga kwa kutumia ushungi wake!
   
Loading...