Mwanamke Anayekoroma Sana Kuliko Watu Wote nchini Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke Anayekoroma Sana Kuliko Watu Wote nchini Uingereza

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Oct 18, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Bibi Jenny Chapman na mumewe Sunday, October 18, 2009 1:37 AM
  Mwanamke mmoja nchini Uingereza ametangazwa kuwa ndiye mtu anayekoroma kwa sauti kubwa kuliko watu wote nchini Uingereza. Sauti anayotoa wakati akikoroma humkimbiza mumewe chumba cha pili kwani ni huwa ni kubwa sana kuliko hata sauti inayotolewa na ndege inayopita chini chini. Ni bora ndege ndogo ipite chini ya nyumba yako ukiwa umelala kuliko kulala chumba kimoja au karibu na Bibi Jenny Chapman wa nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 60.

  Wakati anapolala na kuanza kukoroma bibi Chapman hutoa sauti kubwa sana kuliko sauti inayotolewa na ndege ndogo ikipita chini chini.

  Bibi Chapman hutoa sauti ya desibeli 111.6 ambayo ni desibeli nane zaidi ya sauti inayotolewa na ndege inayopita chini chini.

  Sauti ya kukoroma ya Bibi Chapman ni kubwa sana kuliko sauti zinazotolewa na mashine ya kufulia nguo, lori, trekta na sauti ya treni likiwa kwenye spidi.

  Mumewe Colin, 62, hulazimika kuhamia chumba cha jirani wakati mkewe wa miaka 18 anapoanza kukoroma.

  Amekuwa akikoroma sana katika maisha yake yote na mojawapo ya kumbukumbu katika maisha yake ni kuminywa pua yake na dada zake wakati alipokuwa akiwaamsha usiku kwa sauti za kukoroma kwake wakati huo akiwa na umri wa miaka mitano.

  Bi Chapman amejaribu njia mbali mbali za kutibu tatizo lake la kukoroma lakini hamna njia yoyote iliyofanikiwa kuondoa tatizo hilo.

  Mwisho wa wiki iliyopita bi Chapman alishiriki kwenye kambi ya siku mbili kwenye hoteli ya Hilton Warwick Hotel ambapo watu sita wenye matatizo sugu ya kukoroma walikusanyika kujaribu tiba za za asili za tatizo hilo.

  Katika kambi hiyo, bi Chapman aliwafunika kwa kelele zake za kukoroma washiriki wote katika kambi hiyo, wanaume wanne na wanawake wawili.

  Bi Chapman alisema kwamba ushauri ailiopewa katika kambi hiyo umemsaidia kidogo lakini tatizo lake halitaondoka kamwe.

  Utafiti uliofanyika nchini Uingereza ulionyesha kwamba asilimia 70 ya watu wanaoishi nchini Uingereza hukoroma wakati wa wanapolala.

  Miongoni mwa vitu vinavyosababisha watu wengi kukoroma wanapolala vimeelezwa kuwa ni ulaji wa kiasi kikubwa cha chakula kupita kiasi na unywaji wa pombe.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3348938&&Cat=7
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Du huyo mama kiboko! Huyu anafaa kuishi sehemu kuliko na kelele masaa 24 kama vile manzese uwanja wa fisi, na sehemu kuliko na viwanda vinavyopiga kelele wakati wa kuzalisha bidhaa.
   
Loading...