Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenza wa maisha

Ivi kweli mtu umeubeba moyo wako na hisia unazo, uje kuuliza mke mwema utampataje?Tafuta kitu cha machame then after one year ulete report hapa
 
306027_186727278062199_5555547_n.jpg


[h=3]Mithali 14:1"Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye -------- hibomoa kwa mikono yake mwenyewe"[/h]Kuna mithali isemayo "MAJUTO MJUKUU", ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo. Matatizo mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu aliyeanzisha Ndoa. Baadhi ya sifa za Mwanamke mwenye Hekima – Pia Soma Mithali 31:10-31.


1. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema I katika ulimi wake (31:26). Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mumewe anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni Mbaya.
2. Hufanya kazi kwa Moyo na Huamka alfajiri na mapema
Kuna wanawake ambao ni wavivu kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaribu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haichelewi mwanaume kulipa fadhila kwa wema anaotendewa.


3. Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yake
Kuna wanawake ambao ni wachafu – usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala ni stoo ya nepi za mikojo na nguo chafu, wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti mwanamke awe msafi muda wote. Wanaume wote wanapenda Usafi, marashi hata ya mchina yasikose, Mwanamke hakikisha "Reception" inakuwa Safi na kuwa katika hali ya kumfanya Mume ajisikie kujipumzisha kwa Raha mstarehe.


4. Jali na timiza Mahitaji ya NDOA kwa mume wako
Sulemani anasema mwanamke mwema "Taa yake haizimiki usiku", kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama apanda kitandani huku amevaa "KOMBATI" utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya Ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.


5. Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho familia itafurahia.
Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha "Test", mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.


6. Mwamini Mume wako, wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza Ndoa kwa Uadilifu na Upendo.
 
mke mwema ni yule anayejitambua yeye mwenyewe kama mke/mchumba au mpenzi wa mtu.mwenye heshima pande zote kwao na upande wamume.anayemsikiliza mwezie na kutoa maoni yake mazuli ayasifie na mabaya ayakosoe.anayeelewa nin maana ya maisha kwenye shida avumilie na kwenye raha ajue kuweka akiba.asiwetegemezi sana kwa mume .kama hana elimu au kazi atafute biashara yoyote ya kuongeza kipata cha familia.asiwe mpenda starehe hasa zinazozuilika kama disko.mwisho awe mlezi bora wa watoto na kuwaongoza katika misingi imara.yangu ni hayo tuu...
 
Awe mfupi, mwenye chunusi, kisirani, mitusi, gubu, mchawi,tena asiwe ana kuheshimu hata kidogo, kisha akupige na limbwata... Huyo ndiye mwanamke mzuri sana kuoa

Walioulizwa wametajwa, iltakiwa usome tu usubiri majibu yao
 
Anayefaa kwa mtu mwenye sifa gani?

Mke wa mchungaji na mke wa mpika gongo sifa zao tofauti, hata mapishi yao ni kwa hadhira tofauti.
 
Anayefaa kwa mtu mwenye sifa gani?

Mke wa mchungaji na mke wa mpika gongo sifa zao tofauti, hata mapishi yao ni kwa hadhira tofauti.

Hahahaaaaaa Kiranga u made my evening! Mume mzinzi pia anapata mke mzinzi! Mume mwema muaminifu, kiongozi, anayejali na kutunza mkewe, mwenye akili, mvumilivu, mchapakazi, asiye chapombe na muadilifu ndiye hupata mke mwema!
 
mtu mwenye jinsia ya kike na ana uwezo wakuzaa watoto na kutimiza majukumu yote kama mama .
 
Mwanamke yoyote anafaa kuwa mke kwa kuwa ni mwanamke...

Suala muhimu ni mwanamke gani anafaa kuwa mke wa mwanaume gani....
 
Kila mtu anavigezo vyake,hivi unavyotajiwa nivigezo vya wanao kutajia wao,mfano kuna mtu anapenda msichana anayekunywa pombe siajabu wewe hata harufu haupendi.Lala1 atakwambia anapenda mwenye pesa kumbe wewe haupend kabisa kusikia,.mie ntakwambia napenda mtu mwenye hofu ya Mungu kumbe wewe ndugu kila siku kwa waganga mtaendana kweli?,wewe pia unavigezo vyako,kaa tulia utavipata..My way is not your way

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Wow nice,from Ellen G Whte eeh,...?nakumbuka nishaisoma sehemu,ni nzuri sana,
Mungu namwachia anichagulie mume,i pray for it everyday..amen
 
Mwanamke anayefaa kuolewa anapaswa kuwa na tabia hizi hapa. Please read and confirm.
A -Appearance
B -Body structure
C -Character
D -Decipline
E- Education
F -Fashion.
Mwanamke mwenye sifa hizo anafaa kabisa maana atakuwa amekidhi vigezo na masharti. Je, wewe una nyongeza hapo?
 
Body structure bado ni appearance ile ile,kwaio hapo A. Weka neno lingine
Halafu sio Decipline ni Discipline..
 
hapo kwenye c=character mi sijaelewa kidhungu kwangu kigumu! ni sawa na kusema ' mhusika' au?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom