Mwanamke anaweza kukupenda kweli kwa pesa zako, sio dhambi, pesa kweli inanunua mapenzi

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,164
15,839
Mwanamke anaweza kukupenda kwa PESA zako na akakupenda kweli kweli hili linawezekana.

Sio dhambi, sio vibaya, sio jinai na hili linawezekana kwa asilimia miamoja 100%

Kwanini?
😁😁😁

Kwa sababu ukiona unapendwa au mwanamke akikupenda lazima kuna kitu kakupendea tu sio bure kwamba akupende bila sababu ya msingi.

Mfano mwanamke anaweza kukupenda kwa sababu ya utanashati wako na akakupenda kweli kweli, hapa kakupenda kwa sababu utanashati umefungamana na wewe, yaani UNA utanashati ndio maana akakupenda.

Maana yake bila utanashati au ukianza kupungua utanashati na mapenzi yatapungua pia.

Hapa pia tunasema UTANASHATI UMENUNUA MAPENZI.

Au mwanamke anaweza kukupenda kwa ustaarabu wako, hapo maana yake uustaarabu umefungamana na wewe ndio maana akakupenda ama UNAO ustaarabu ndio maana akaupenda.

HAPA TUNASEMA USTAARABU UMENUNUA MAPENZI.

Au mwanamke anaweza kukupenda kwa sababu ya maneno yako mazuri, hapa maana yake maneno mazuri yameambatana na wewe ama una maneno mazuri. Ndio maana kakupenda.

NA HAPA MANENO MAZURI YAMENUNUA MAPENZI.

Sasa iweje pesa isinunue mapenzi ama isisababishe mtu kukupenda wakati ambapo pesa itakuwa imeambatana na wewe na unayo?

Pesa inapokuwa imeambatana na wewe,ama unapokuwa una pesa za kutosha maana yake hiko ni kivutio kama vivutio vingine kwa mwenzio yaani..

Pesa ni kivutio kama kivutio cha utanashati.
Pesa ni kivutio kama kivutio cha six pack.
Pesa ni kivutio kama kivutio cha urefu.
Pesa ni kivutio kama kivutio cha ustaarabu.

Kwa hiyo mwanamke anaweza kukupenda kwa sababu amevutiwa na pesa zako,na hili sio ubaya kukupenda kwa ajili hii kwa sababu pesa ni kivutio kama vivutio vingine.

Pengine mtu akauliza JE, PESA ZIKIISHA ATAENDELEA KUKUPENDA?

Sasa na utanashati ukiisha ataendelea kukupenda?
Kama jibu ni ndio basi na pesa ni ndio.

Je, ustaarabu ukiisha ataendelea kukupenda?
Kama jibu ni ndio pasi na pesa ni ndio.

Je, six pack zikiisha anaweza kukupenda?
Kama jibu ni ndio basi na pesa ni ndio.

Kwa hiyo pesa ni kivutio kwa mwanamke kama vivutio vingine vinavyoambatana na wewe yaani urefu,weupe,unene,wembamba n.k

Tusiwalaumu kutupenda kwa ajili ya pesa, kwani kila mmoja ana sababu yake ya kukupenda na pesa ni sababu pia ya kukupenda.

Na pesa ni sababu kubwa sana kwa sababu itamnufaisha na kumfanya apate mahitaji yake.
Lakini weupe wako hauwezi kumtimizia mahitaji yake.
Urefu wako hauwezi kumtimizia mahitaji yake.
Ustaarabu wako hauwezi kumtimizia mahitaji yake.

Pesa ina nafasi kubwa sana katika kujenga mahusiano na kununua mapenzi kwa mwanamke.

Kila mmoja ana chaguzi zake.
 
Umeongea #Fact mkuu mm bnafs nakupa 100%..... Ngoja waje wengne ila bla shak hakutakuwa na AnY criticism
emoji1545.png
emoji1545.png
emoji1545.png
 
Swala la pesa ni variable! Kuna waliopendwa wakiwa na pesa ila ndoa zao ziliishia kuvunjika.

Mapenzi sio pesa japo pesa hunogesha mapenzi. Inawavutia wengi sana pesa,wapenzi, marafiki, maadui.

Cha msingi nachoshauri ni kuwa vijana tuwe makini katika choice zetu. Wanawake waliopenda pesa sio wepesi kuvumilia siku pesa zikiwa hazipo. Hatuzungumizii negatively ila kuna mambo yanatokeaga na kutugharimu. Imagine Corona ilivyokuja na kuwaacha wengi matatizoni
 
Kuna waliopendwa wakiwa na pesa ila ndoa zao ziliishia kuvunjika.
Na ndivyo hivyo kuna ambao waliopendwa wakiwa na utanashati na ndoa zao zilovunjika.

Kuna ambao waliopendwa wakiwa na ukarimu na ndoa zao zilivunjika.

Kiukweli mkuu sababu ya kukupenda mwanamke inaweza isiondoke na bado hapo hao akakumwaga.

Yaani haina maana kuwa watu wanaachana ati kwa sababu tu kile ambacho walipendeana kimepotea ama kimetoweka.

Mwanamke anapokupenda kwa jambo moja tukumbuke kuwa kuna mambo mengi ambayo anayachukia kama binadamu.

Mapenzi sio pesa japo pesa hunogesha mapenzi. Inawavutia wengi sana pesa,wapenzi, marafiki, maadui.
Kwa nini useme sio pesa mkuu wakati ni kivutio cha mapenzi.

Yani ni sawa mtu aseme mapenzi sio ukarimu.
Au mapenzi sio utanashati.
Au mapenzi sio uhandsome.

Cha msingi nachoshauri ni kuwa vijana tuwe makini katika choice zetu. Wanawake waliopenda pesa sio wepesi kuvumilia siku pesa zikiwa hazipo.
Mkuu hivyo hivyo wanawake waliopenda ukarimu wako sio wepesi kuvumilia jgomvi wako.

Hivyo hivyo wanawake waliopenda utanashati wako sio wepesi kuvumilia uovyo ovyo wako.

Kwa maana ya kuwa mbali na pesa hiko ambacho mtu amekupendea basi sio rahisi kuvumilia kinyume na hivyo.
 
Hi
Na ndivyo hivyo kuna ambao waliopendwa wakiwa na utanashati na ndoa zao zilovunjika.

Kuna ambao waliopendwa wakiwa na ukarimu na ndoa zao zilivunjika.

Kiukweli mkuu sababu ya kukupenda mwanamke inaweza isiondoke na bado hapo hao akakumwaga.

Yaani haina maana kuwa watu wanaachana ati kwa sababu tu kile ambacho walipendeana kimepotea ama kimetoweka.

Mwanamke anapokupenda kwa jambo moja tukumbuke kuwa kuna mambo mengi ambayo anayachukia kama binadamu.

Kwa nini useme sio pesa mkuu wakati ni kivutio cha mapenzi.

Yani ni sawa mtu aseme mapenzi sio ukarimu.
Au mapenzi sio utanashati.
Au mapenzi sio uhandsome.

Mkuu hivyo hivyo wanawake waliopenda ukarimu wako sio wepesi kuvumilia jgomvi wako.

Hivyo hivyo wanawake waliopenda utanashati wako sio wepesi kuvumilia uovyo ovyo wako.

Kwa maana ya kuwa mbali na pesa hiko ambacho mtu amekupendea basi sio rahisi kuvumilia kinyume na hivyo.
Hivi unajua hussle ya kutafuta pesa mzee? Ama unaongea ilimradi tu. Halafu Pesa mahitaji yake ni infinity bro! Usifananishe hela na jambo lolote hapo juu!

Hayo ya utanashati sijui blablah ni rahisi kwa mtu kuya overlook ila sio tatizo la Security na Physiological needs!

Food, clothes and shelter plus money! Ubaya ni kwamba hela inaweza kusapoti mahitaji mengine yote...its at the center of the stage. Huwezi pata chakula, nguo wala malazi kama huna hela.
 
Haha nakueleea mkuu sasa unataka kusema vipi ?
Maana nakubaliana na wewe kwamba pesa inatafutwa kwa tabu,lakini kutafutwa kwake kwa tabu haimaanishi kuwa isimvutie mwanamke akakupenda.

Kama ambavyo kuna wanawake wanapenda tu mwanaume daktari,na udaktari unatafutwa kwa shida sana.

Ama mwanamke anampenda mchezaji maarufu,na umaarufu unatafutwa kwa shida sana.

Kitu kutafutwa kwa shida sidhani kama inamaanisha kuwa watu wasivutiwe na kitu hiko.

Ama ulikusudia vipi mkuu ...
 
Hela ina overshadow tamaa zote, ni means of exchange. Bila pesa hamna chochote kinaendelea.

Ni obvious wapo mabinti wanaopenda pesa kama watu wapendavyo vingine.
 
Hela ina overshadow tamaa zote, ni means of exchange. Bila pesa hamna chochote kinaendelea.

Ni obvious wapo mabinti wanaopenda pesa kama watu wapendavyo vingine.
Yes ndo mana nasema kuwa mwanamke anaweza kukupenda kwa pesa zako manake amependa pesa na kwa kuwa pesa zipo kwako na wewe anakupenda.

Kama ambayo anapenda utanashati na kwa vile utanashati upo kwako ama unao basi atakupenda wewe.

Hicho ndo nilichokusudia mkuu,kuhusu pesa kumaliza shida zote na naaaam sahihi kabisa ,hiyo ni kazi ya pesa bila shaka
 
"Olu in olu", hakuna mtu anaeweza kukupenda bila sababu yoyote. Hata mama yako anakupenda kwasababu wewe ni mtoto wake. Pesa ni kilainishi linapokuja swala la mapenzi, lakini sio kila kitu katika mapenzi. Ndio maana kuna watu wanaachana ingali bado pesa zipo. Sio kweli kwamba watu wanaachana tu pale pesa zinapoisha.

Mbona mondi na zari waliachana kwani mondi aliishiwa pesa? Mzee Mengi mwenyewe (rip) aliachana na mke wake ilihali akiwa bilionea. Kuachana ni ishu nyingine kabisa.. Uwe na pesa usiwe nazo unaweza kuachwa tu kama tabia zako nyingine hazivumiliki.
 
Swala la pesa ni variable! Kuna waliopendwa wakiwa na pesa ila ndoa zao ziliishia kuvunjika.

Mapenzi sio pesa japo pesa hunogesha mapenzi. Inawavutia wengi sana pesa,wapenzi, marafiki, maadui.

Cha msingi nachoshauri ni kuwa vijana tuwe makini katika choice zetu. Wanawake waliopenda pesa sio wepesi kuvumilia siku pesa zikiwa hazipo. Hatuzungumizii negatively ila kuna mambo yanatokeaga na kutugharimu. Imagine Corona ilivyokuja na kuwaacha wengi matatizoni

Hivi ukiwa na pesa kwa nini uoe? Unatakiwa uwagegede tuu
 
Mwanamke ni km dini. Tunaweza kukupa mwaka mzima uyazungumzie lakin bado usimalize.

Kwa hiyo wee ishi maisha yako. Kujitai mjuaji utajinyonga Siku moja ukija gundua hujui KTU..
 
"Olu in olu", hakuna mtu anaeweza kukupenda bila sababu yoyote. Hata mama yako anakupenda kwasababu wewe ni mtoto wake. Pesa ni kilainishi linapokuja swala la mapenzi, lakini sio kila kitu katika mapenzi. Ndio maana kuna watu wanaachana ingali bado pesa zipo. Sio kweli kwamba watu wanaachana tu pale pesa zinapoisha. Mbona mondi na zari waliachana kwani mondi aliishiwa pesa? Mzee Mengi mwenyewe (rip) aliachana na mke wake ilihali akiwa bilionea. Kuachana ni ishu nyingine kabisa.. Uwe na pesa usiwe nazo unaweza kuachwa tu kama tabia zako nyingine hazivumiliki.
Na ndivyo hivyo kuna ambao waliopendwa wakiwa na utanashati na ndoa zao zilovunjika.

Kuna ambao waliopendwa wakiwa na ukarimu na ndoa zao zilivunjika.

Kiukweli mkuu sababu ya kukupenda mwanamke inaweza isiondoke na bado hapo hao akakumwaga.

Yaani haina maana kuwa watu wanaachana ati kwa sababu tu kile ambacho walipendeana kimepotea ama kimetoweka.

Mwanamke anapokupenda kwa jambo moja tukumbuke kuwa kuna mambo mengi ambayo anayachukia kama binadamu.

Kwa hiyo anaweza kukupenda kwa pesa lakini akachukiwa na tabianzako mbovu nyingine nyingi,kama ambavyo anaweza kukupenda kwa uhandsome ama utanashata na ia akachukiwa na tabianzako mbovu nyingine.
Pesa ni kilainishi linapokuja swala la mapenzi, lakini sio kila kitu katika mapenzi.
Hata utanashati ama uhandsome au ukarimu katika mapenzi ni vilainishi tu lakini sio kila kitu katika mapenzi pia.

Kwa sababu kuna watu walipendana wakiwa masikini na baadae wanaachana wakiwa na umasikini huo huo,kama ambavyo kuna watu walipendana wakiwa na pesa na bado wanaachana wakiwa na esa.

Hii ina maana hata kisichokuwa pesa kinaweza kuwatenganisha watu.

Na maana yake hata kile ambacho kimewavutia wanandoa wawili kisichokuwa pesa pia sio kila kitu katika mapenzi kmndo maana pia watu huachana na wao sio matajiri ni masikini tu.

Yaaani watu waliowana kwa sababu lada mume ni handsome ila baadae wakaachana,hii ina maana uhandsome sio kila kitu.

Sio kweli kwamba watu wanaachana tu pale pesa zinapoisha
[/QUOT
NAKUBaiana na wewe ndugu..
Mbona mondi na zari waliachana kwani mondi aliishiwa pesa
Mimi na wewe tujiulize kwanini waliachana ?
 
Hi

Hivi unajua hussle ya kutafuta pesa mzee? Ama unaongea ilimradi tu. Halafu Pesa mahitaji yake ni infinity bro! Usifananishe hela na jambo lolote hapo juu!

Hayo ya utanashati sijui blablah ni rahisi kwa mtu kuya overlook ila sio tatizo la Security na Physiological needs!

Food, clothes and shelter plus money! Ubaya ni kwamba hela inaweza kusapoti mahitaji mengine yote...its at the center of the stage. Huwezi pata chakula, nguo wala malazi kama huna hela.
Hhhhhh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom