Mwanamke anaweza akiwezeshwa: The case of anne makinda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke anaweza akiwezeshwa: The case of anne makinda!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Analyst, Apr 9, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Misemo ipo mingi sana hapa nchini kuonesha kwamba kuna haja ya kuwawezesha wanawake kupiga hatua katika kuendeleza familia zao na taifa kwa ujumla. Inawezekana msemo huu ndiyo uliotumiwa na Mfalme R.A wa CCM kumwondoa mshirika wake wa zamani ktk mtandao, Bw. Sammy 6 (tena bila taarifa ya mapema) na kumweka Bi Anne Ma.K kuhakikisha Bunge linapunguza kasi ya kumchunguza na kumkosesha usingizi mfalme huyo wa Maf. Papa na chama chao.

  Ninapojaribu kuchanganua kauli za huyu mama na mambo yake naanza kuhofia kwamba pengine namna ya kuwawezesha kina mama si kwa staili hii iliyotumiwa na Mfalme RA na washirika wake wakipigiwa solo na Mzee Makamba. Labda ingekuwa vizuri apewe nafasi ya kujiendeleza kitaaluma, kisaikolojia, kimaadili na kitamaduni (kwa kuwa ni tabia njema kwa mwanamke makini wa kibantu kuona haya anapofanya jambo la aibu hadharani kama yeye anavyofanya ndani ya Bunge). Mama mtu mzima kama yeye kukosa staha na kuwa katika jazba kila anapoona mbunge wa CDM anatoa hoja kukosoa uongo na majibu ya hovyohovyo ya mawaziri si mfano mzuri kwa wanawake wengi makini, wenye elimu nzuri na uwezo wa uongozi ambao kwa bahati mbaya mfalme hakuwaona na kuwatengea bajeti ili wapate nafasi ya kuonesha uwezo wao ktk nafasi ya uspika.

  Naomba kutoa rai kwa watanzania wenye nia ya dhati ya kuwasaidia Mama na dada zetu, kupiga kelele na kuhakikisha serikali na familia zetu wanashirikiana kuimarisha elimu ili kupata wanawake watakaoweza kweli kufanya kazi na kusimamia maslahi ya taifa kwa dhati na si kwa lengo la kuwafurahisha watu wanaowawezesha kufika hapo kwa mbinu chafu tena za underground. Mwanamke aina ya spika wetu hata asitumike kuwaaminisha watanzania kwamba ameweza baada ya kuwezeshwa kwa kuwa anachokifanya sasa ni kutaka kudumu ktk nafasi hiyo endapo Mfalme RA atendelea kuwa nje ya Magereza (mahala ambako haswa anastahili kuwa) na kuendeleza mbinu zake chafu.
   
Loading...