Mwanamke anapokubali kufujwa kwenye ndoa au uhusiano…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
2,000
black-couple-yelling-360x414.jpg

Kufujwa ni kitendo cha mpenzi mmoja kuwa na mamlaka aliyojipa dhidi ya uhuru na haki ya mwenzake. Inaweza kuwa ni kusimanga, kukosoa kupita kiasi kumuita mwenzie mjinga, mbumbumbu n.k. Pia naweza kusema ni kile kitendo cha mpenzi mmoja kumuumiza mwenzake kwa kauli zake au kimwili mara kwa mara. Kwa bahati mbaya sana wanaokubali kufujwa ni wanawake ukilinganisha na wanaume. Miongoni mwa matatizo ya ndoa ambayo mtu hashauriwi kuendelea kuyavumilia ni kufujwa. Ndani ya kufujwa kuna maumivu makubwa ya hisia na mwili.

Kuna ufujaji wa aina kadhaa ukiwemo ule ambao kwa mazoea huwa hautazamwi kama ufujaji hasa. Mazoea maana yake ni kwamba, unafanywa sana na ni kama vile jamii imekubaliana nao kwa njia moja ama nyingine, ingawa una maumivu na madhara yakutosha.

Hapa chini nitataja baadhi ya aina za ufujaji:

1. Ufujaji wa kimwili: Huu ni ufujaji ambao mpenzi anatumia nguvu za mwili dhidi ya mwenzake, ambapo mara nyingi, humwacha anayefujwa akiwa ameumia au kumweka katika mazingira ya kuumia. Ufujaji huu hutofautiana kutoka kukwaruzwa kwa mwili au kupigwa hadi kifo kwa mhusika. Na hii hufanyika kwa kupigwa, kusukumana, kumtupa mtu chini, kupiga mateke, kupiga vibao, kuminya, kugonga, kukaba, kutikisa, kung'ata, kubamiza, kubonyeza na kudhuru kwa kutumia silaha, kisu bunduki, bastola, kumwagia mwenzake maji ya moto au mafuta ya moto au wakati mwingine kuchoma nyumba moto wakati mwenzake akiwa ndani amelala…

2. Ufujaji wa kihisia: Kufuja kisaikolojia au kihisia kunaweza kuwa kwa kauli au bila kauli. Tabia zinazooneshwa hapa zinaweza kuwa zimejificha sana kiasi kwamba si rahisi mtu kubaini kwamba kuna ufujaji unaendelea katika uhusiano huo. Ufujaji huu unaelezwa kwamba ni mbaya zaidi ya ule wa kimwili kwani makovu ya ufujaji huenda ndani kwa kina kirefu sana. Ufujaji huu huhusisha masimango, kutisha kwa maneno, uharibifu wa mali za mpenzi, au hata wanyama wa ndani kama paka, ikiwa ni juhudi za mfujaji kumtisha mpenzi ili afuate yale anayotaka. Kwa kifupi tunaweza kusema ni matumizi ya ‘mkwara'. Pia kuna kupiga kelele, kutukana kwa kashfa, majibu ya mkato na dharau, kudhalilisha kwa maneno ya kebehi, kutania kwa lengo la kuudhi na kumbeza mpenzi akiwa peke yake au mbele ya watu wengine wa familia au hadharani….. Pia kukosoa, kutoamini uamuzi wowote au ushauri wa mpenzi na wakati mwingine kumdharau waziwazi, kujitahidi kuthibiti, kumchonganisha mpenzi na ndugu au na marafiki zake, kumdhalilisha mpenzi kwa maneno wakati mfujaji akiwa amelewa na baadaye kusingizia pombe. Lengo la ufujaji wa aina hii ni kumfanya mfujwaji ahisi kushtakiwa na dhamira na kukubaliana na yale anayotendewa na mfujaji.

3. Ufujaji wa kimapenzi: Ufujaji wa aina hii huweza kubainika kwa vitendo kama hivi vifuatavyo: Kumlazimisha mfujwaji kufanya mapenzi nje ya utashi wake, kumlazimisha kufanya ngono isiyo salama, kulazimisha kufanya mapenzi yenye kudhalilisha (hususan kulawiti), kujaribu kumwekea mpenzi mipaka ya uchaguzi wake kimapenzi au uzazi. Pia kukagua simu kuona ni akina nani mpenzi anawasiliana nao, kuulizia habari za wapenzi wa zamani kwa marafiki au ndugu zake. Hapa ndipo ambapo neno, ‘malaya' hutumiwa sana na mfujaji. Kwa kawaida mwanamke anayefujwa anakuwa hana kauli kuhusu mwili wake mwenyewe na suala zima la mapenzi. Mwanaume mfujaji ndiye anapanga lini, kwa vipi na kwa nini tendo la ndoa lifanyike. Ndiye ambaye anapanga lifanyike au lisifanyike. Ndiye ambaye anapanga kuhusu watoto wangapi wapatikane kwenye ndoa na lini wapatikane. Lakini pia tendo la ndoa huweza kutumiwa kumdhalilisha mwanamke. Kwa mfano. Kumwambia mke, ‘unazaa kama panya tu,'au ‘nina wasiwasi mtoto huyu siyo wangu,' au ‘unanizalia wahudumu wa baa tu,' kufuatia ndoa kujaaliwa watoto wa kike mfululizo. Kuna suala la mwanaume kulinganisha mkewe na hawara zake, 'Kwa kweli humfikii fulani kwa vitimbwi vyake kitandani, ndiyo maana na nafikiria kumwoa,' mume anaweza kumwmabia mkewe maneno hayo bla wasiwasi….

4. Ufujaji wa kiuchumi: Huu ni pamoja na kumnyang'anya mpenzi nguvu na uwezo wa kudhalisha, kutumia njia ya wizi au kuharibu pato la mpenzi. Je hujawahi kusikia mume anamkataza mkewe kufanya biashara au ametuma majambazi kuvamia shughuli ya mkewe ya biashara ili asiwe na nguvu ya kuzalisha? Kama hujasikia, kwa taarifa yako tu ni kwamba, mambo haya yapo sana kutoka kwa wanaume wafujaji. Lakini kingine ni pamoja na kumnyima mpenzi kama adhabu au kwa sababu nyingine mahitaji ya msingi kama chakula, nguo, matibabu na kumwachisha mpenzi kazi kwa ushawishi au kwa nguvu.

5. Ufujaji wa kiroho: Ni pale ambapo mpenzi anatumia dini au imani ya mwenzake kumwendesha. Kuna wakati mpenzi anabaini kwamba, kwenye imani yao au ya mpenzi wake kuna kipengele anachoweza kukitumia kumkandamiza mwenzake, ambapo hukitumia. Kwa mfano, kama imani ya mwenzake au imani yao inasema mwanamke amtii mumewe, basi kipengele hicho kitapindwapindwa na mpenzi hadi mfujwaji akubali yale anayotaka mfujaji kupitia kipengele hicho. Lakini pia humzuia mpenzi kushiriki kwenye ibada au maombi au huduma yoyote ya imani yake. Kuzuia huku kunaweza kuwa ni kwa moja kwa moja au kwa mbinu za kulaghai na kukashifu. Mara nyingi hata hivyo kashfa, matusi, kebehi na matumizi ya nguvu hutumika katika suala hili. Kuna wakati watoto hulazimishwa kufuata imani ambayo mzazi mmoja haitaki na ambayo pengine haikuwa imani ya yeyote kati ya wapenzi wawili. Mpenzi mmoja kabadili dini wakiwa tayari kwenye ndoa, halafu analazimisha watoto kufuata hiyo dini yake mpya, bila makubaliano na mwenzake ambaye yeye hajabadili dini. Mara nyingi hii hufanywa na wanawake………. Hii ni aina ya udhalilishaji kupitia dini au imani ambao ni udhalilishaji wa kiroho. Imani inatumika kutoa maumivu kwa mwingine………
 
Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,010
2,000
Hakuna sababu ya kumpigia mtu kelele kama vile unaonea na mtu half deaf. Unaweza kutoa warning softly like a mafia don.
Hii inasababishwa na confusion. Do not amplify your anger. Umeiona ile crime programme katika DSTV,''Beyong Scared Stright',ambapo vijana wajeuri wanapelekwa jela kuona maisha ya wafungwa ili waweze kufikiria kama wanataka kupelekwa pale. Those prisoners are always shouting at them. How can you shout at someone and spit in his face and expect that he will listen to you?
 
Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
2,000
huwezi kukubali kufujwa kama umejitambua, me naona dhana hii ni kutokana na kuamini mapenzi upofu ila si kweli, love or relation shud be constructive n not destructive like this
 
decruca

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
295
195
mara nyingi hii hutokea kwa wanawake ambao hawana shule ya kutosha, au wamekuwa watumwa wa penzi. Maana kuna wanawake wasiojiamini kabisa, kiasi kwamba wanafikiri wamezaliwa hapa duniani kwa ajili ya hao wanaume wanaowafuja, yaani kiasi kwamba wakiachana nao bac hawatasonga mbele kimaisha. Lakini kama una shule yako na unajiamini huwezi kutumbukia ktk hili kundi la ufujwaji wa namana hii.Wito: enyi wanaume wapendeni wake zenu.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,392

Hata wasomi hufujwa. Kufujwa kunatokana kwa asilimia kubwa na malezi ya jamii zetu.
Mara nyingi wasichana huelezwa ndoa ni ngumu na inahitaji uvumilivu. Pia hufundishwa kuachika ni jambo baya na lenye fedheha kubwa kwa familia. Wazazi huwafundisha watoto wao kuvumilia ili wasilete aibu kwa familia. Kwa sababu hakuna kipimo cha uvumilivu let say kama uvumilivu ungekuwa unapimwa kwa digrii kama joto basi wangwambia uvumilivu ukifika digrii 39 basi waweza kuachika.

Nafikiri kuna haja ya kuwaambia mabinti. Kama mme wako anakufanyia hivi na hivi basi huyo siyo mme mwema hakufai ondoka urudi nyumbani.
 
Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,461
2,000
Decrusa asante sana hayopia yalikuwa mawazo yangu.sikubali mtu anionee anifuje kwa jinsi yyt ninacho sina nabeba wanangu utaisoma namba ya gari,its not too late to start afreash.
 
Last edited by a moderator:

Thomas Odera

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
659
250
Hilo somo ni fundisho tosha lakini si kwa wanawake tu kwamba ndio wanaofujwa hata wanaume piaila hawasemi maana huona aibu. Ahsante mkuu kwa darasa
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,546
2,000
Kuacha tafsiri yako, kufuja hasa maana yake nini?

Kwanini umechagua neno hilo?

Ungetumia 'kuumiza' usingeleta maana uliyokusudia?

Nguo unaweza ifuja si ndio? Kitu kilichofujwa kinapoteza ubora, uzuri na muonekano wake wa awali eeh?

Umesisitiza kuwa wanawake wanakubali kufujwa kuliko wanaume, hivyo kama nguo au furniture hufifia, right?

Ni maswali tu, sina comment!
 
snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,140

Kaunga my dear mi najua ndo mtaalamu wako wa lugha ngija nifanye kazi yangu hapa mpenzi!
Mtambuzi yupo sahihi kabisa kutumia istilahi hii''kufujwa''

kama vile nguo iliyofujwa isivotamanika ndivyo mwanamke au hata pengine mwanaume aliyefujwa anakuwa.
anayefujwa huwa hivi

-hajitambui thamani wala upekee wake vivo hiyo kwa nguo iliyofujwa huwa mara nyini inaishia kuwa tambara la deki tu!(SO SAD TO SAY THIS)

-hawezi kufit in kwenye mahusiano ya jamii nyingine since haamini katika kupendwa wala kupenda anaamini katika kutumika(ngo iliyofujwa huwa haifai kuvaliwa popote wakati mwingine hata jikoni tu unaona kazi kuivaa)

-haamini tena kuwa ana mamlaka juu ya nini aamue au nini aache maana anahitaji ridhiko la macho ya wengine katika kila anachofanya

-kila kitu kwake hewala since hana maamuzi ya mwili wake,mali zake,hisia zake,majina ya watoto wake,wapi afanye kazi,nani aongee nae,nani asiongee nae(vivo hvo kwa nguo iliyofujwa huwa haina uchaguzi wapi iwekwe itawekwa kwenye kapu sawa,kwenye boxi sawa,chini sawa,haichanganywi kwenye nguo pendwa!pitia kabati lako la nguo utalithibithisha hili)

-huamini anachofanyiwa ni sawa na ndo majaaliwa yake so hata ukimwambia kuwa mamii au papito hapo unafujwa huwa hawezi kukuamini na hata akikuamini ataishia kusema sasa nifanyaje mimi jamani ndo nimeshaolewa na ndo nimeshaoa sina jinsi!(tofauti na nguo pendwa ambayo ukiivaa tu tofauti ya makubaliano like haka kasuti kangu ni ka kakanisani au harusini ukaenda kukamenyea ndizi bukoba au mshale kataonyesha madoa au usugu mahala fulani,nguo iliyofujwa haina hizo haina sauti italimiwa shambani,itakatiwa ng'ombe majani,itabebewa gunia la mkaa itafutiwa miguu itapangusiwa jasho wala imetulia tu,huoni chochote cha tofauti)

mradi tu kufujwa ni hatari na janga kubwa sana kimahusiano!
 
Ahsante sana Shemeji yangu snowhite, maana ndio nilikuwa najiandaa kumjibu Kaunga, lakini umeniwahi na umeelezea kwa usahihi kabisa na mifano mizuri ambayo haiachi maswali nyuma.

Naamini sasa Kaunga atakuwa ameelewa somo hli vizuri sana.
 
karibu shemeji yangu!ila huu ushemeji huu unafanya nakosa power of attorney sa nyingine ah!
(how i miss habari za we mzee na wee binti lol!)
ahahahhahahah !
leo umenipa thread ambayo inahusiana moja kwa moja na sms nimetumiwa jana kutoka kwa binti mmoja anayelalamika ufujaji anaofanyiwa rafiki yake yani habari za wewe una nini hapa,hujui kupika hiyo ni mbele za wageni enh!unanuka sijui hata mara ya mwisho umeoga lini
watoot hawa hawafanani na ukoo wetu sijui
ndo maisha ya kila siku ndani ya hiyo nyumba !sasa huyo binti ananiuliza antie nifanyeje kumsaidia rafiki ayngu anateseka sana !
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,154
1,250
Kuacha tafsiri yako, kufuja hasa maana yake nini?

Kwanini umechagua neno hilo?

Ungetumia 'kuumiza' usingeleta maana uliyokusudia?

Nguo unaweza ifuja si ndio? Kitu kilichofujwa kinapoteza ubora, uzuri na muonekano wake wa awali eeh?

Umesisitiza kuwa wanawake wanakubali kufujwa kuliko wanaume, hivyo kama nguo au furniture hufifia, right?

Ni maswali tu, sina comment!

Was thinking kama wewe dada.......yawezekana kufuja hapa haileti maana kusudiwa

Mfano; Nimemuachia gari yangu niliposafiri......kaifuja sana jamaa yule....!!!!!! wataalamu wa lugha mtusaidie

Mkuu mtambuzi kufuja ni tofauti na unyanyasaji wa namna kama ya kijinsia??????

But maudhui ya mada inafundisha na kukumbusha mengi.......bravo
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,154
1,250
Kaunga my dear mi najua ndo mtaalamu wako wa lugha ngija nifanye kazi yangu hapa mpenzi!
Mtambuzi yupo sahihi kabisa kutumia istilahi hii''kufujwa''

kama vile nguo iliyofujwa isivotamanika ndivyo mwanamke au hata pengine mwanaume aliyefujwa anakuwa.
anayefujwa huwa hivi

-hajitambui thamani wala upekee wake vivo hiyo kwa nguo iliyofujwa huwa mara nyini inaishia kuwa tambara la deki tu!(SO SAD TO SAY THIS)

-hawezi kufit in kwenye mahusiano ya jamii nyingine since haamini katika kupendwa wala kupenda anaamini katika kutumika(ngo iliyofujwa huwa haifai kuvaliwa popote wakati mwingine hata jikoni tu unaona kazi kuivaa)

-haamini tena kuwa ana mamlaka juu ya nini aamue au nini aache maana anahitaji ridhiko la macho ya wengine katika kila anachofanya

-kila kitu kwake hewala since hana maamuzi ya mwili wake,mali zake,hisia zake,majina ya watoto wake,wapi afanye kazi,nani aongee nae,nani asiongee nae(vivo hvo kwa nguo iliyofujwa huwa haina uchaguzi wapi iwekwe itawekwa kwenye kapu sawa,kwenye boxi sawa,chini sawa,haichanganywi kwenye nguo pendwa!pitia kabati lako la nguo utalithibithisha hili)

-huamini anachofanyiwa ni sawa na ndo majaaliwa yake so hata ukimwambia kuwa mamii au papito hapo unafujwa huwa hawezi kukuamini na hata akikuamini ataishia kusema sasa nifanyaje mimi jamani ndo nimeshaolewa na ndo nimeshaoa sina jinsi!(tofauti na nguo pendwa ambayo ukiivaa tu tofauti ya makubaliano like haka kasuti kangu ni ka kakanisani au harusini ukaenda kukamenyea ndizi bukoba au mshale kataonyesha madoa au usugu mahala fulani,nguo iliyofujwa haina hizo haina sauti italimiwa shambani,itakatiwa ng'ombe majani,itabebewa gunia la mkaa itafutiwa miguu itapangusiwa jasho wala imetulia tu,huoni chochote cha tofauti)

mradi tu kufujwa ni hatari na janga kubwa sana kimahusiano!

Pamoja na majibu mazuri nina swali la nyongeza mkuu

Hivi binadamu na ufahamu wake wote na jinsi anavyojitambua yeye na mazingira husika unaweza kumlinganisha moja kwa moja na nguo ambayo haiwezi hata kutoka kwenye tenga yenyewe???????? Is not this reductionism????

Binadamu sio passive kabisa kama nguo hata kama haamui kivitendo but akili yake sio kuwa imelala....mara ngapi tunasikia retaliation za ajabu na kutisha kutoka kwa hao mnaowaita "waliofujwa"???????

Si tunasikia siku hiz kuna counseling.......haya iwaje tena ukamkatia tamaa kama tambara la deki?????

Natamani kujua zaidi
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,546
2,000
Asante my ticha snowhite, nimeelewa zaidi.
Nazidi kuchunguza lengo la mtoa mada, nikuongelea kwa mpangilio vitu ambavyo watu wanaviishi? Maana heading kwa heading nilitegemea zaidi ya kufafanua aina ya ufujaji. Halafu matumizi ya neno (ufujaji), huzidi kumfanya mwanamke kujiona kama kitu kinachotumika na mwisho kufubaa (ndio maana nikauliza kama kulikuwa na better word); kwa maoni yangu tumizi hilo la neno linabomoa zaidi ya kujenga IMO.

Mleta mada hajasema root cause ya wanawake kukubali 'kufubaliwa na wanaume', na wala hajapropose nini wafanye ili ku undo huo ufubaaji (sijui tambala la deki lina second chance).

Kama umegundua post zangu at least recent najaribu kupinga kitu kinachomfanya mwanamke aone mtu mwingine ndie anayesababisha maamuzi yake. Sasa hiiterminology ya kufubaa na kufubazwa haijanikalia sawa kwenye namna yangu ya kufikiri. Ningeridhishwa na neno kama 'kuumizwa au hata kunyanyaswa' na hapo tungeenda mbele at least kutafakari tu ni jinsi gani tutoke huko, inaweza isiwe kwa kizazi chetu lkn kwa watoto tunaowazaa; tuwaandaaje wajitambue na kujua nini wanachotaka na kustahili ktk mahusiano.
 
Last edited by a moderator:

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,154
1,250
Mkuu Mtambuzi.......kumpa mtu like ni vizuri na ahsante

But ni kama mtu ana njaa na unampa chewing gum.........hebu jibu basi na hoja on top of liking
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom