Mwanamke anahitaji nini kutoka kwa mwanaume?

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
1259302262_mahaba.jpg

KUTATULIWA MATATIZO​
Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidika katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

KUBEMBELEZWA​
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.

KUWA NAMBA MOJA​
Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumiliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo.

Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa. Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya.

4. KURIDHISHWA KWENYE TENDO​
Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo. Utundu unahitajika ili kumkata kiu ya penzi.

5. MAZUNGUMZO
Wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na maana kuwa wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine.

Kwa msingi huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao. Kama una mpenzi wako mpe uhuru wa kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali.

se5dnc.jpg
 
KUBEMBELEZWA​

Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.

Ndicho wapendacho

Lakini wengine mnapenda vitu ambavyo mhhhhh, hata hamuangalii jamani. Utakuta mwnamke analazimisha vitu ambavyo yeye mwenyewe anaona hali sio.
 
Kikubwa na Financial Security, hayo mambo mengine yatajipanga yenyewe!!!

Finances zina mchango wake mkubwa lakini siyo kweli kuwa mengine yatajipanga kwa vile unazo fedha.
Hujasikia mtu anamkimbia mwenye pesa na kuishia kwa mtu asiye na kitu ilimradi kuna penzi?
 
Pamoja na Kilimanjaro stars kushinda , jamani hivi Maximo aliletwa kwa ajili ya Bara au Tanzania nzima? Hivi kiutaratibu si angebaki kama mshauri tu kwa timu zetu za Zanzibar na Kilimanjaro ? Naomba ufafanuzi na mnieleweshe.
 
Hujakosea jukwa kweli wewe?
 
watu wawili msichana na mvulana walisimama kwa karibu kabisa....msichana alikuwa anaangalia mbele ya suruali ya mvulana pakiwa pamesimama wima akawa anaangalia kwa tamaa na hamu kubwa ya kingono ngono.....mvulana nae akawa anaangalia mbele ya sidiria ya msichana pakiwa pamesimama chuchu saa sita akashikwa na tamaa na hamu ya kingongono pia.......ghafla kwa wakati mmoja msichana akapeleka mkono wake kunako suruali ili ajaribu bahati yake wakati huo huo mvulana nae alisha peleka mkono wake kukagua mzigo wa kifua ndipo..........mvulana akakuta kumbe ni APPLE akafurahi sana akala....na msichana nae akakuta kumbe ni NDIZI akafurahi sana pia akala.....
ndicho akipendacho mwanamke kwa mwanaume..................
 
Pamoja na Kilimanjaro stars kushinda , jamani hivi Maximo aliletwa kwa ajili ya Bara au Tanzania nzima? Hivi kiutaratibu si angebaki kama mshauri tu kwa timu zetu za Zanzibar na Kilimanjaro ? Naomba ufafanuzi na mnieleweshe.
..Mpwa vipi tena? mbona umeingia choo cha kike??? Hii sio mahala pake hapa!! Modes help p'se..
 
Pamoja na Kilimanjaro stars kushinda , jamani hivi Maximo aliletwa kwa ajili ya Bara au Tanzania nzima? Hivi kiutaratibu si angebaki kama mshauri tu kwa timu zetu za Zanzibar na Kilimanjaro ? Naomba ufafanuzi na mnieleweshe.

offtopic! tazama jukwaa la michezo! ila karibu jf
 
Back
Top Bottom