Mwanamke amuua Chui baada ya kupigana nae kwa muda wa nusu saa

mwanamke-chui.jpg


madaktari wakimpatia matibabu mwanamke aliyeua chui

mama mwenye umri wa miaka 54, kamla devi amefanikiwa kumuua chui baada ya kupigana nae kwa takribani dakika 30 huko india.mkasa huo ulimkuta mwanamke huyo akiwa katika harakati zakurudi nyumba baada ya kuhitimisha shughuli za shamba ndipo njiani mamaa! Kakutana na chui ndipo vurugu zikaanza, kwakuwa mama huyo alikuwa na mundu najembe dogo aliweza kumdhibiti mnyama huyo asiweze kumdhuru.

mapigano hayo yalidumu kwa dakika kadhaa baada ya kila mmojakujeruliwa, ila mama huyo alipoteza nguvu nyingi kutokana na kuvuja damu sanakabla ya kupata msaada, na baadae watu walimtafuta chui na kumkuta amekufa pembeni yake kichakani.

mama huyo anaendelea na matibabu katika hospital kuu ya india. Kuna wanaume wanajifanya wababe sana na kuwaonea wanawake kwa kuwapiga au kuwanyanyasa, sasa wamfuate na huyo mama wakakione cha moto, chui kafa! Wewe sijui atakufanyaje huyu mama,tusiwachukulie poa wanawake wako fiti pia. Mia

chanzo: Tabianchi

shujaa huyooo.
 
Halafu vichui vyao kama vimbwa koko,tena chui wao hawana mafunzo ya kukwepa mundu na jembe angekutana na chui wa ruaha au serengeti wangemkuta huyo mama kabaki khanga -no sari zake tu!
 
Halafu vichui vyao kama vimbwa koko,tena chui wao hawana mafunzo ya kukwepa mundu na jembe angekutana na chui wa ruaha au serengeti wangemkuta huyo mama kabaki khanga -no sari zake tu!

Kungekuwa kuna kujaribu tungekupeleka wewe up ambiance na huyo chui, mana usije kuwa wasema hayo Wakati ndo wale ndani kuna Panya unatoka nduki
 
huyo chui alikiuwa mzee.....alfu mgonjwa....chui auawe na mwanamke....tena mdosi...????
 
Kungekuwa kuna kujaribu tungekupeleka wewe up ambiance na huyo chui, mana usije kuwa wasema hayo Wakati ndo wale ndani kuna Panya unatoka nduki

Tafadhali usiniletee hata ndotoni! We koma kabisa mawazo hayo! Hapana chezea hayo makitu! Lol! Natania siogopi chui wala vyui!
 
Inapobidi binadamu huwa anafanya tukio ambalo wewe mwenyewe ukijasikia huwezi amini, ndio huyu sasa. Katika kutetea uhai wake ameonesha ujasiri wa hali ya juu
 
kweli wakina mama mkiwezeshwa mnaweza[/QUOTE]

Haa sasa hapo kawezeshwa nini labda jamani appreciate tu hata kwa shingo upande
 
Back
Top Bottom