Mwanamke ambaye alishafunga ndoa kanisani anaweza kuolewa tena kanisani?

Daah yaan wewe ndio umeishiwa anyway..biblia iko wazi angekua mjane ungeoa ila kwa kua ana nfoa na mumewe yupo huyo mke wa watu..
 
Wakuu leteni uzoefu

Mtu alikuwa ni mke wa mtu kwa ndoa ya kanisani kkkt, anataka kuolewa tena, na mahari itolewe imekaaje hii? walokole wamekubali, kutufungisha japo siyo waumini wao, sasa si utapeli wa kichaga huu kweli? au nioe tu, nimempata humuhumu member wa long time JF.
What part of 'till death do us apart' dont u understand...lol
Anyways..nadhani inabidi watalikiane rasmi na mumewe kwanza mahakamani ndipo msajili RITA ndoa mpya in peace
 
Mshauri huyo maanamke atafute talaka kwanza, baada ya hapo unaweza kumuoa, haijalishi ni talaka ya wapi, hata ya mahakamani inatosha.
Makanisa hasa RC wamekuwa wagumu sana kwenye talaka, ila KKKT wako very understanding kwenye hizo issue za divorce.

Akiwa na talaka, na kama kuna kanisa litakuruhusu kufunga ndoa, funga, na hiyo ndoa itakuwa halali kabisa.
 
We jamaa mbuzi kweli. Umekosa wanawake mpaka uoe mke wa mtu unalaana wewe sio bure
Wakuu leteni uzoefu

Mtu alikuwa ni mke wa mtu kwa ndoa ya kanisani kkkt, anataka kuolewa tena, na mahari itolewe imekaaje hii? walokole wamekubali, kutufungisha japo siyo waumini wao, sasa si utapeli wa kichaga huu kweli? au nioe tu, nimempata humuhumu member wa long time JF.
 
Mshauri huyo maanamke atafute talaka kwanza, baada ya hapo unaweza kumuoa, haijalishi ni talaka ya wapi, hata ya mahakamani inatosha.
Makanisa hasa RC wamekuwa wagumu sana kwenye talaka, ila KKKT wako very understanding kwenye hizo issue za divorce.

Akiwa na talaka, na kama kuna kanisa litakuruhusu kufunga ndoa, funga, na hiyo ndoa itakuwa halali kabisa.
FUATA HUU USHAURI...

SASA WATU WAMESHATENGANA...ETI KISA ALIFUNGA NDOA BASI HUWEZI ACHANA NAE...HATA KAMA MTU ANAWEZA KUKUDHURU...WEWE UNG'ANG'ANE TU NI MUME WANGU MKE WANGU...

NDIO MAANA ALLAH KAWATAJA KWENYE QURAN SURAT HADIID...(..Na mapadre walijizushia ibada zao ambazo Mungu hakuwandikia...eti wanajifanya kutafuta radhi za Allah...HATA SHERIA WALIZOJITUNGIA VILE VILE HAWAZIFUATI IPASAVYO.)

Hiyo till death mmeiongezea tu wenyewe...wala Mungu hakuandika hiko kitu...na wala iliposema "anayekiunga Mungu binadamu asikitenganishe" kwani ni mpaka Mungu aje akwambie wewe nenda kule na wewe nenda kule...mmejiwekea eti kifo tu ndio utengano...hata migogoro na kupotea kwa upendo ndani ya ndoa pamoja na chuki...ni sehemu ya UTENGANO...

KWA SABABU ALLAH PEKEE NDIYE ANAYEWEKA UPENDO KWENYE MOYO WA MTU...hata kama umpe mtu dunia nzima...kama huo upendo Mungu hajauweka hutopendwa...NA AKIWEKA ALLAH UPENDO...NI YEYE NDIYE ANAYEWEZA KUUTOA...

NYIE MMEKAZANA KUKAMATILIANA...MTAUANA BURE...
 
Aisee kumbe mna mlolongo mrefu hivi? Ingekua kwenyr dini ya kiislam kama amepewa talaka unaoa bila kipingamizi
 
Mkuu kama huyo mwanamke amekwisha kutalakiana na mumewe unaweza mkaoana naye bila shida pale bomani. Vyeti vya ndoa vyote ndani ya Tanzania vinatolewa na serikali kupitia Rita.
Hapo swala ni wapi utafungia hiyo ndoa yako kati ya kanisani na bomani tu , hakuna tofauti. Maana hata bomani mtaapishwa viapo vile vile tu na maombi juu.

Usichanganywe na maneno ya watu ndoa ni maelewano na makubaliano ya watu wawili tu, wa tatu ni yule anayewafungisha hiyo ndoa ambaye anakuwa anamuwakilisha MUNGU sawa na Malaki 2:14 --- na Rum 13: 1-13 kwamba mamlaka zote zimewekwa na MUNGU chini ya jua . Kwamba hata kama ndoa yako utaifungia bomani yaani serikalini ni ya MUNGU, na MUNGU ni shahidi.
Kwahiyo Talaka ni muhimu ili awe huru kuolewa na wewe kisheria, na pia akiwa na talaka itamzuia aliyekuwa mume wa huyo mwanamke kumfanyia fujo baadae.
Nakutakia kila la heri kwenye ndoa yako.
 
Sema watu wanakuza sana mambo, someni biblia vizuri na muyatafakari vizuri kwa undani yote yaliyoandikwa humo mpate kufanikiwa sana kwenye kila mlifanyalo. Joshua 1:8.
Kuna swali nitauliza mfano. Kwenye biblia kuna neno linasema ukipigwa shavu la kulia mgeuzie akupige na shavu la kushoto , sasa swali lipo hivi , " huyo mtu na ngumi ya uzito wa kilo 20 , na kisha kupiga shavu la upande wa kulia na ngumi yake ya kilo 20, je, utamuachia akupige na upande wa kushoto pia?" Hapo lazima utafakari kwanza ..... ndipo ufanye maamuzi sahihi.
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom