Mwanamke ambaye alijifungua kwa operation (kwa kisu), anaweza kujifungua tena kwa njia ya kawaida?

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,375
29,732
Habari zenu!

Nimewahi sikia kuwa endapo mwanamke atajifungua mtoto wa kwanza kwa njia ya operation, basi watoto wanaofuata yeye kujifungua basi nao watazaliwa kwa njia ya operation.

Je kuna ukweli katika hili?
 
jamani hata mim inanitesa sana hyo sipendi kabsa kujifungua kwa opresheni kama kuna mtu anamajibu na jinsi ya kufanya ili mtoto wa pili usijifungue kwa opresheni aniambie
 
Mamangu watoto wote watatu ni upasuaji , dadangu watoto wote wawili ni upasuaji , rafiki wa dadangu nui hivyo hivyo watu wanasema kama mtu ukifanyiwa upasuaji kwaajili ya maswala ya uzazi hata mtoto wa pili na watatu ni hivyo hivyo na ushauri uzae zaidi ya watatu
 
Nadhani ulimaanisha "USIZAE"
 
Mtoto wangu wa kwanza now seven years alizaliwa Kwan njia ha operation, miaka mitatu baadae tukajaliwa mtoto wa pili na wife alijifungua kawaida tu.
Usiogope mkuu inawezekana bila Shida.
 
pole sana. Kama tatizo ni la kimaumbile kwa mama ni lazima na wengine wazaliwe kwa kisu. Na anaweza kuzaa hadi mara nne. ila kama shida ni uchungu pingamizi, ukubwa wa mtoto, mlalo wa mtoto na yafananayo na hayo, anaweza kujifungua kawaida uzazi unaofuata ila ni lazima watoto wapishane kiasi cha kutosha.
 
ukishaanza kwa operation mtoto wa kwanza lazima uendelee kwa operation watoto wanaofuata
 
Mtoto wangu wa kwanza now seven years alizaliwa Kwan njia ha operation, miaka mitatu baadae tukajaliwa mtoto wa pili na wife alijifungua kawaida tu.
Usiogope mkuu inawezekana bila Shida.
Nashukuru, ila sababu ya kujifungua kwa mkasi raundi ya kwanza ilikuwa ni nini? Na kilifanyika nini mpaka raundi ya pili ikawa ya kawaida?
 
pole sana. Kama tatizo ni la kimaumbile kwa mama ni lazima na wengine wazaliwe kwa kisu. Na anaweza kuzaa hadi mara nne. ila kama shida ni uchungu pingamizi, ukubwa wa mtoto, mlalo wa mtoto na yafananayo na hayo, anaweza kujifungua kawaida uzazi unaofuata ila ni lazima watoto wapishane kiasi cha kutosha.
Raundi ya kwanza walidai ana nyonga ndogo, yeye alikuwa na miaka 19 na imepita miaka minne na nusu sasa, sijui kama raundi hii atakuwa poa!
 
Mamangu watoto wote watatu ni upasuaji , dadangu watoto wote wawili ni upasuaji , rafiki wa dadangu nui hivyo hivyo watu wanasema kama mtu ukifanyiwa upasuaji kwaajili ya maswala ya uzazi hata mtoto wa pili na watatu ni hivyo hivyo na ushauri uzae zaidi ya watatu
Je sababu ya hizo operations ni nini? Yaani kwa nini hawakujifungua kwa njia za asili?
 
Mara nyingi inakuwa hivyo.

Kwa haraka haraka ninaowafahamu waliojifungua kwa njia ya kisu mara ya kwanza, basi na mara ya pili inakuwa kisu tena.

Na wakishajifungua mtoto wa pili kwa kisu basi ujue kinachofuata wanafungwa kizazi
 
Back
Top Bottom