Mwanamke aliyetokana na ubavu wangu anirudishie ubavu huo mara moja nikaunywe supu

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,697
9,774
Sasa ifikie wakati tuendane na kauli ya usawa wa 50 kwa 50

Haiwezekani kila demu ninayemfuata namtongoza huku nikiambulia matusi makali kutoka kwake, halafu mwisho wa siku nibahatike kumchakata, nitachakata mara mbili tatu kisha tutaachana. Kwani nyie mnategemea nikaoe makaa ya mawe?

Just imagine unamsimamisha mwanamke kumweleza hisia zako anakujibu "Sina huo muda mchafu wa kuskiliza kampeni uchwara" Sasa unataka swaag zangu nikamrushie mbuzi?

Juzi kati nimetoka kumtongoza msichana mmoja mzuri saana, pic qal, halafu mpole, rangi ya mzeituni ambae akipita karibu na gheto langu akanikuta nje atatabasamu na kucheka cheka kwa aibu. Cha ajabu wakati namsimamisha kanitusi matusi ya nguoni kwa hasira kali, hivi anadhani nikimaliza sabuni madukani, yeye atafulia majivu?

Sasa narudia kusema, "Mwanamke aliyeumbwa kwa ubavu wangu baada ya mimi kupigwa nusu kaputi na sir God anirudishie ubavu wangu mara moja, nikauchemshe, niunywe supu ijulikane moja! Acheni tu nife na utamu wangu
 
Sasa narudia kusema, "Mwanamke aliyeumbwa kwa ubavu wangu baada ya mimi kupigwa nusu kaputi na sir God anirudishie ubavu wangu mara moja, nikauchemshe, niunywe supu ijulikane moja! Acheni tu nife na utamu wangu
emoji26.png
emoji26.png
HAPA SIO FB NA INSTA KAKA.
 
HAPA SIO FB NA INSTA KAKA.
Sawa mkuu, hata jf ina official verified accounts kwenye social media za instagram na facebook.

Halafu kingine, jifunze kuandika. Kichwa cha habari pekee ndicho ambacho huandikwa kwa herufi kubwa

Kwenye ufupisho wa maneno, kila herufi itatenganishwa kwa nukta. mfano FB Ilitakiwa kuandikwa F.B

Hakuna mtandao wa kijamii unaoitwa INSTA, sahihisha hapo uandike Instagram

Kingine, sio kila uzi unaokutana nao ni lazima utupie comment yako. Halafu hili sio jukwaa la siasa.

Na liwe fundisho kwa wengine wenye shobo kama zako! Na hili tukalitizame
 
Back
Top Bottom