Mwanamke Aliyesingizia Kubakwa Atupwa Jela baada ya kutubu kanisani


Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
38,383
Likes
7,326
Points
280

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
38,383 7,326 280
Mwanamke Aliyesingizia Kubakwa Atupwa Jela


Biurny Peguero Thursday, February 25, 2010 2:00 AM
Mwanamke wa nchini Marekani aliyemsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka na kusababisha mwanaume huyo atupwe jela, amehukumiwa kwenda jela baada ya kutubu kanisani kuwa aliongopa kubakwa na mwanaume huyo.
Biurny Peguero mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa jiji la New York nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu baada ya kukiri kumsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.

Mwaka 2005, Biurny alimsingizia mwanaume huyo kuwa alimtishia na kisu kabla ya kumbaka. Mwanaume huyo alihukumiwa kwenda jela miaka minne.

Mwaka jana Biurny alienda kutubu madhambi yake kanisani na kukiri mbele ya mchungaji kuwa alimsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.

Hatua hiyo ilisababisha polisi wapewe taarifa ambapo mwanaume huyo aliachiliwa huru muda mfupi baadae.

Akisomewa hukumu yake, Biurny alihukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu.
 
Joined
Mar 17, 2009
Messages
37
Likes
0
Points
0

Shelute Mamu

Member
Joined Mar 17, 2009
37 0 0
Huyu mama ameonyesha mfano mzuri. Watu wengi wamefungwa au kuuwawa kwa mambo ya kusingiziwa. Wengine wapenzi wao baada ya kuwachoka wanaitiwa watu kuwa wezi hivyo wanashambuliwa hadi kuwa - wengi wamepoteza maisha! Watu waige mfano wa KUTUBU ili wawe na maisha ya amani kwa muda waliopangiwa na Mola hapa duniani.
 

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
20
Points
135

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 20 135
Basi kweli dunia inakaribia ukingoni. Lakini wapo wengi wanaofanyizia wenzao makosa yasiyokuwapo. Kuna mmoja aliifanya kazi hiyo kwa advantage ya mahusiano aliyo nayo kwa watu wa usalama wa Taifa na Ikulu, limbikeni kabisa, japo anacho cheo kiheshimiwa katika jamii, mwanaume rijari kabisa, alifanyizia enzake kazini hadi kuwapeleka polisi ati kapigwa ofisini. Akatishia vingi tu akiwaambia wenzake atahakikisha wastaafu vibaya hata kuwapa kamisheni ya utawala bora na haki za binadamu kuhaha kila mahali kuchunguza, lakini wakubwa wake mpaka sasa hawataki kumfahamu vizuri jamaa huyu, kiasi kwamba alitimuliwa sehemu yake ya kazi, lakini wakubwa wake wakamrudisha kwa nyundo aendelee kuwa tishio mahali pa kazi.

Sasa hapo ndipo tunapotofautiana na wazungu, wao wakikaa chini na kutfakari huingiwa na utu halisi na kusema ukweli. Ngozi nyeusi mara nyingi akitaka kumharibia mwenzake anaapa kwa jina la Mungu kabisa. Hata umwambieje huwa na kiburi mpaka apate akitakacho. Hujasikia maofisini wengine wanafukuzwa kazi kwa sababu bosi kasema umeiba kwa sababu tu ameomba umfungulie kitasa umemkatalia? Si wanaume si wanawake, wote ni uchuro mtupu. Mambo ya kuingiliana ni complex maana inakuwa ni lazima watu waamini usemacho
 

cheusimangala

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2010
Messages
2,590
Likes
12
Points
0

cheusimangala

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2010
2,590 12 0
ni mbaya sana kwa kweli imagine unatumikia kifungo bila hatia!na majuu wanafanya sana hii kitu ,wengine wakiachana wanasema baba anawasexualy abuse watoto maana hiyo ndiyo njia itakayosaidia baba kupigwa marufuku kuwasogelea watoto wake.
 

Forum statistics

Threads 1,204,698
Members 457,411
Posts 28,167,132