Mwanamke aliyefiwa na mume huitwa mjane, Mwanaume aliyefiwa na mke nimwite nani?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,204
42,066
Wakuu,

Tupo sehemu tunabishana na wadau. Mwanamke aliyefiwa na mumewe huwa anaitwa Mjane, vipi mwanaume akifiwa na mke anaitwaje?

Kuna sehemu nilisema anaitwa mgane wakasema siyo kweli kuwa kunajinalake!

Waswahili mnisaidie tafadhali
 
kuna sehemu nilisema anaitwa mgane wakasema siyo kweli kuwa kunajinalake! waswahili mnisaidie

Sidhani kama kuna namna yoyote ya kumwita mtu wa namna hii. Nimetafuta na nimeshindwa. Nafikiri kuna haja ya kutengeneza neno na kuliongeza kwenye msamiati wa kiswahili. Mgane lingefaa tu...:wink2:
 
Sidhani kama kuna namna yoyote ya kumwita mtu wa namna hii. Nimetafuta na nimeshindwa. Nafikiri kuna haja ya kutengeneza neno na kuliongeza kwenye msamiati wa kiswahili. Mgane lingefaa tu...:wink2:

kama ujui bora kunyamaza wapo wanaojua na mdau jina aliloweka ndilo linatumika.
 
muite mjane...

kwa tafsiri, neno mjane hutumika kumaanisha mwanaume asiye na mke na mwanamke asiye na mume ima ni kwa kufiwa, kuachika/kuacha au hajawahi kabisa kuwa na mwenza wa ndoa inayokubalika katika sheria za pahala/nchi husika.
 
kama ujui bora kunyamaza wapo wanaojua na mdau jina aliloweka ndilo linatumika.

Unaweza kunyoosha sentenso yako kama hivi: Kama hujui, ni vema unyamaze kwani wapo wanaojua. Kwa taarifa yako, mdau aliyependekeza neno "mgane" yupo sahihi...hi hi hi hi hi ha ha ha ha ha!:wink2:
 
Mjane na mgane maneno yote ni sahihi na wana maana moja ya mtu aliyefiwa na mwenza, na kuisha pale tu anapopata mwenza mwingine. Hivyo mara nyingi huwa wanawake ndio hutumiliwa neno hilo kwa kuwa wanaume hukaa muda mfupi sana kabla ya kupata mwenza mwingine ikilinganishwa na wanawake.
 
kuna sehemu nilisema anaitwa mgane wakasema siyo kweli kuwa kunajinalake! waswahili mnisaidie
Ni kweli ulikosea kwakuwa haitwi mgane bali mjane

Au kama vipi ukiona limekushinda sana waweza mwita wifi.:lalala:
 
neno sahihi ni mgane.
Source: radio one kipindi cha kiswahili. Jibu kutoka kwa Makii Hassan.
 
kuna sehemu nilisema anaitwa mgane wakasema siyo kweli kuwa kunajinalake! waswahili mnisaidie

.
Kwa mujibu kwa kamusi ya TUKI

1. Mjane nm wa- [a-/wa-] 1 widow, widower.

2. Mjane mwanamke - widow

3. Mjane mwanamume - widower

4. Mjane nm wa- [a-/wa-] 2 unmarried person, bachelor, spinster.

.
 
MGANE ni sahihi zaidi. Isitoshe limeshaanza kuzoeleka. Popote utakapotaja Mjane inaeleweka ni Mwanamke aliyefiwa na mume wake. Haileti maana mwanamke ambaye hajaolewa kabisa kuitwa Mjane. Hebu jaribu kumwita Mjane mwanamke ambaye hajaolewa kabisa au aliyeachika uone moto wake..
 
Back
Top Bottom