Mwanamke Aliyebadilishiwa Mtoto Wake Hospitali ya Mwananyamala Ampata Mtoto Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke Aliyebadilishiwa Mtoto Wake Hospitali ya Mwananyamala Ampata Mtoto Wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 27, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  MWANAMKE aliyebadilishiwa mtoto wake wodini alimpata baada ya kuanza msako mkali uliofanyika wodini humo Wakunga na wauguzi waliokuwa zamu walianza kuwahoji wakinamama waliokuwa wodini humo na kubaini kuwa kuna mama mwingine alimchukua mtoto huyo ambaye hakuwa wake.

  Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kilisema kuwa, mama yule alirudi wodini na kuwaeleza kuwa aliondoka na mtoto ambaye hakuwa wake na manesi kuanza kulishughulikia suala hilo kwa kuwa lilikuwa ni jambo hatari la kumfukuzisha mtu kazi.

  Kwa juhudi za manesi wakishirikiana na wakunga walipita kwa kila mwanamke ambaye alijifungua kwa wakati ule na huku wakiwa na faili lililoonyesha kuwa mwanamke amejifungua mtoto gani na kubaini kuwa kuna mama mmoja alimbadilisha mtoto wake na kumchukua mtoto ambaye hakuwa wake.

  Mama huyo alibainika baada ya kuonekana amembeba mtoto wa kike wakati yeye alijifungua mtoto wa kiume na wakati akihojiwa alikuwa hana jibu.

  Hivyo manesi walimchukua mtoto yule na mama aliyeibiwa mtoto wake alimgungua mtoto yule kuwa ni wa kwake kwa kuwa alimuweka alama katika moja ya sehemu katika mwili wa mtoto yule na alikiona kitenge alichomviringisha mtoto yule.

  Hatua iliyofuata mama yule alikabidhiwa mtoto wake na yule mwingine kupewa mtoto wake ambaye alimbadilisha.

  Kwa vitisho vilivyotoka kwa manesi mama yule alipohojiwa alikiri kuwa alimbadilishia mwenzake wakati alipokwenda ****** na kukiri na yeye alikuwa anatamani mtoto wa kike kwa muda mrefu.

  Kwa huruma za manesi wengine ambao walimuonea huruma mama huyo na kuamua kutomchukulia hatua kwakuwa alitoka kujifungua lakini manesi wengine wenye hasira walionekana kumpachika maneno makali mama huyo na wengine walionekana kuwa na jazba ya kutaka kumpiga kwa kuwa alikuwa anataka kuwafukuzisha kazi.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2626902&&Cat=1
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni heri amempata mwanae halali, hii inaonyesha wengi wetu tunaishi pengine na watu ambao siyo mama zetu.
   
 3. U

  Umushoshoro Senior Member

  #3
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45

  Vipi maambukizi ikiwa mama mmoja au wote wawili atakua ameathirika?

  Uwezekano wa watoto au mtoto kuambukizwa kwa kunyonyeshwa ukoje?

  Kwa kweli hii ni hatari sana,hawa manesi si wa kuwaacha hivi hivi
   
Loading...