Mwanamke alazimishwa kuvua nguo zake ili aachiwe huru na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke alazimishwa kuvua nguo zake ili aachiwe huru na polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 30, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Polisi 15 wa nchini Mexico wamesimamishwa kazi baada ya kumlazimisha mwanamke waliyemkamata avue nguo zake na kisha acheze uchi mbele yao.

  Polisi 15 wakiwemo polisi watatu wa kike wa nchini Mexico wamesimamishwa kazi baada ya video yao wakimlazimisha mwanamke waliyemkamata acheze uchi kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari.

  Mwanamke huyo alikamatwa na polisi katika mji wa Tijuana akiwa pamoja na mpenzi wake ambapo alituhumiwa kufanya wizi wa credit card na cheki za benki.

  Ili aweze kuachiwa huru mwanamke huyo alilazimishwa avue nguo zake zote na kisha acheze dansi uchi mbele ya mapolisi hao 15.

  Tukio hilo lilitokea mwezi machi mwaka huu lakini video ya tukio hilo iliyochukuliwa kwa kutumia simu ya mmoja wa polisi hao ilivuja na kuwafikia waandishi wa habari ambapo ilionyeshwa kwenye vyombo vya habari wiki hii.

  Polisi wote 15 walioshiriki kumlazimisha mwanamke huyo acheze uchi wamesimamishwa kazi huku wakisubiri kufikishwa mahakamani kwa unyanyasaji walioufanya kwa mwanamke huyo.

  Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  makubwaa
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Kilicho nifurahisha ni ufanisi wa wakubwa wao wa kazi, yani ingekuwa bongo ungesikia inaundwa tume na mwisho wa siku hakuna anayewajibishwa wala kuwajibika wakati ushahidi wa macho na mazingira upo wazi. Kama huami uliza tarime nn kimetokea,singida nn kimetokea,mabomu ya mbagala je,gongolamboto je..
   
 4. S

  Sebali Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndipo panadhihirisha kwamba polisi wengi hamnazo! Uwezo wao wa kufikiri ni finyu sana!
   
 5. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Bongo bila kuunda tume viongozi hawaridhiki.....ingetokea bongo sijui ingekuaje
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tz iyo mbona ingezimwa kimtindo!isingefika kote uko!
   
Loading...