Mwanamke akutwa kama alivyozaliwa ndani ya kanisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke akutwa kama alivyozaliwa ndani ya kanisa

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Nov 4, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280  Makongoro Oging' na Haruni Sanchawa
  Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 mpaka 40 (pichani), amekutwa ndani ya Kanisa la House of Prayer Center ‘HPC' akiwa mtupu hali iliyomchanganya akili Mchungaji wa kanisa hilo.

  Tukio hilo la aina yake lilijiri saa kumi ya alfajiri katikati ya wiki iliyopita, Tabata ya Liwiti jijini Dar es Salaam.

  Mashuhuda wa mkasa huo walilitonya Risasi Mchanganyiko kuwa, mwanamke huyo alitambulika kwa jina la Neema Komba na alikuwa na binti yake wa miaka 3 ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

  Mashuhuda hao waliendelea kusema kwamba, katika kujieleza kwake, mama huyo alisema ni mwenyeji wa mkoa wa Ruvuma, akitokea Wilaya ya Songea, alifika jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusalimia ndugu na jamaa.

  Aidha, taarifa kutoka katika kanisa hilo zinasema kuwa, Neema alinaswa na walinzi wa kanisa hilo kitu ambacho kilizua hofu na tafrani kanisani hapo kwa muda wa saa kadhaa.

  "Ile hali ilizua hofu na tafrani kubwa kwa muda wa saa kadhaa, unajua mambo kama haya halafu kwa kanisani ni vitu vya ajabu sana," alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.

  Aliongeza kuwa, ilikuwa walinzi wa kanisa hilo wanafanya doria kwa kuzunguka kila eneo la kanisa hilo, ndipo waliposikia sauti ya nyao za miguu ya binadamu, "ndipo walipoamua kuingia na kumkuta mama huyo akiwa uchi jambo ambalo lilitushangaza sana ukilinganisha na muda wenyewe," aliongeza muumini huyo.

  Inadaiwa baada ya hapo walinzi hao walimjulisha Mchungaji wa kanisa hilo kwa lengo la kumtambua mwanamke huyo lakini naye alionekana kuwa mgeni machoni pake.

  Hata hivyo, baadhi ya watu walionesha masikitiko yao kwa hali ya mama huyo, ingawa baadhi yao waliamini ni mchawi na kutaka kumpa kichapo cha mbwa mwizi.

  Mwishowe, uongozi wa kanisa hilo ukiongozwa na Mchungaji Patrick Kayimbi Emanuel na akina mama waliokuwepo eneo la tukio walijitolea kumpa khanga kwa nia ya kujisitiri.

  Akihojiwa na Mchungaji Kayimbi, mwanamke huyo alisema hajui amefikaje ndani ya kanisa hilo kwani ana akili zake timamu.

  Baadaye Mchungaji Kayimbi alitia neneo la Bwana kwa nia ya kufukuza mapepo akiamini ndiyo yaliyomfikisha mwanamke huyo ndani ya kanisa hilo.

  Lakini wakati hayo yakiendelea walitokea ndugu zake waliodai ndiyo wenyeji wa mwanamke huyo, Dar na kuuomba uongozi wa kanisa hilo kumwachia ndugu yao waende naye nyumbani.

  Mchungaji aliwakubalia lakini kwa masharti kuwa, siku iliyofuata wamrudishe kwa ajili ya kuendelea kumfanyia maombi kupitia Neno la Mungu.

  Naye Mchungaji huyo alipoulizwa na Risasi kuhusiana na hali hiyo huku akionekana kushangaa, alisema kabla ya tukio hilo kutokea walifanya maombi kwa muda wa siku tatu mfululizo ili kuombea yale yote mabaya ambayo yanaweza kutokea kanisani hapo, kasema: "Naamini kuwa matokeo yake ndiyo haya sasa."
  CHANZO:http://lukemusicfactory.blogspot.com/2010/11/mwanamke-akutwa-kama-alivyozaliwa-ndani.html
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kuelekea huko tunakotaka haki nawaambia,Majaribu ni mengi sana wajamen.
   
 3. k

  kinyongarangi Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is jamii photo mbona unaleta stori tu bila picha.Unachanganya masomo wewe
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Je kanisa lako limekosa waumini? Ni PM nikupe mbinu kedekede za kulifanya kanisa lako maarufu na lenye waumini wengi.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  mchawimm.jpg

  Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35 mpaka 40 (pichani), amekutwa ndani ya Kanisa la House of Prayer Center ‘HPC’ akiwa mtupu hali iliyomchanganya akili Mchungaji wa kanisa hilo.
   
 6. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mbona ananguo,, au macho yangu!!
   
 7. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Chanzo hakiaminiki, Tupa kule!!
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Ulitaka nimuweke uchi kwani? kwani hapa ni jukwaa la wakubwa?au ulita nipewe BAN?
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,151
  Trophy Points: 280
  Makanisa yanatafuta kujitangaza, hizo ni mbinu za kibiashara. "Biashara ni matangazo na matangazo ni biashara kubwa zaidi".
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
 11. che-guavara

  che-guavara Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ohooooo.napita tu
   
 12. Dumelang

  Dumelang JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 2,190
  Likes Received: 1,540
  Trophy Points: 280
  Ilibidi ndugu waulizwe wanajua nini kuhusu jamaa yao na wanafikiri nini kuhusiana na tukio hilo..na wao wanahsi alifikaje! then ilibidi ijulikana alilala wapi usiku huo kama ni kwa ndugu zake bado kuna maswali.. otherwise mother ni mchawi kaingia anga za watu bila taarifa rada za wakina mzee naniii pale Tabata LIWITI zikamtungua
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Pita tu lakini usije ukajikwaa na chupa.....
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  mkuu usitoe Siri za watu utakunja kulogwa wewe.... huyu atakuwa ni mchawi aliyeingia kwenye anga za watu wengine ndege yake anayotumia ni Ungo imekosea njia Rada yake haikukamata vizuri ndio maana amenasa ndani ya kanisa hahahahahahahahah
   
 15. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Inamaana makanisa yanafanya business? Au ni kejeli?
   
 16. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Biashara matangazo mkuu.
   
 17. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #17
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kanisa kama ni la bwana! Wakristo tunaamini limejengwa juu ya ngome imara, Hata wachawi, wazinzi, waabudu miungu, mashoga, hawawezi kulitikisa Kanisa.
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Je Mafisadi hawawezi kulitingisha Kanisa?
   
 19. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  kanisa la mungu lililo Imara hawawezi kulitikisa!
   
 20. Sele Mkonje

  Sele Mkonje Verified User

  #20
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 180
  kweli kabisa! Lakini Anglican wanaruhusu ushoga! Sa sjui hawa 2waweke wapi? Huyu mama Alikuja kuiba sadaka 2!
   
Loading...