Mwanamke akikosa upendo Kwa Mumewe, huutafuta Upendo Kwa watoto

Na hata ufanyeje huwezi kutimizi hivyo vitu 99. Hapo ndipo complications zao zinapojitokeza
True Tycoon, utajitahidi umridhishe na hiki baada ya muda atataka kile,yaani ni vurugu mechi

kuna msemo unasema "wanawake hawajawahi kueleweka wanataka nini"
 
MWANAMKE AKIKOSA UPENDO KWA MUMEWE, HUUTAFUTA UPENDO KWA WATOTO.

Anaandika Robert Heriel.
Yule Mtibeli.

Je uliwahi kusikia maneno Kama hayo hapo chini?
Mama Mkwe kichomi!
Mama Mkwe anaingilia ndoa yangu!
Mawifi wanakera balaa!
Mawifi hawanipendi!

Bila Shaka wengi wetu tangu tungali wadogo tunajua tumeona Malalamiko haya. Mpaka imefikia hatua ya kuzoeleka na kuunda kasumba kuwa Mama wakwe wengi ni vichomi Kwa wakamwana wao(wake za watoto wao wakiume)

Leo Taikon sitaki kuwachosha.

Moja ya sababu kubwa zinazopelekea wamama wengi kuwa na wivu Kwa watoto wao wa kiume na kuingilia ndoa za watoto wao ni kutokana na kukosa mapenzi ya dhati Kutoka Kwa Waume zao(Baba zetu)

Na Kama ni WiFi, basi ukiona WiFi anaingilia ndoa yako basi ujue Mume wake anapwaya.

Mume asipompenda Mkewe husababisha hisia za mama na Mapenzi ya mama kuhamia Kwa Mtoto hasa mtoto wakiume.

Kiasili mwanamke huhitaji mwanaume kumfariji, kumpa maneno mazuri, kumpa mapenzi na kumpetipeti.

Mwanamke anadekezwa na Mwanaume, haiwezekan Mwanamke akadekezwa na Mwanamke mwenzake. Hiyo haipo.

Mwanamke asipodekezwa na Baba yake,
Basi atadekezwe na kupetiwapetiwa na Mume wake, Kama asipodekezwa na hao basi atadekezwa na kupetiwa na Mtoto wake wa kiume.

Asije akakudanganya Mtu, mwanamke anapenda kusifiwa, kudekezwa na kupetiwa petiwa kuliko kitu chochote Duniani.

Hata Mama Yako mzazi ukimsifia, ukamdekeza au kumpetipeti atakupenda kuliko watoto wake wote.
Kumdekeza mtu ni kujali mapungufu yake na kujifanya huyaoni, kumfariji, na Kama amekosea unampa adhabu ndogo hukuukimbembeleza😊😊.
Hata hivyo mwanamke hupenda pia kufokewa walau mara moja moja kama mtoto kwani hupenda umuone Kama mtoto wake.
Wanawake huchukulia kufokewa Kama sehemu ya Upendo wako kwake ili asiharibike. Ila sio umfokee fokee kila muda pasipo sababu ya Msingi.

Mwanamke akikosa Mapenzi Kwa Mumewe hutarajia upendo Kwa mtoto wake.
Kumbuka mtoto anauwezo WA kumiliki tofauti na Mume. Anammiliki Kwa sababu ndiye aliyeibeba mimba na kumzaa mtoto huyo. Hivyo kigezo hicho kinatosha kuona Kama anastahili kupendwa na mtoto wake wakiume na kudeka kwake.

Lakini lazima ujiulize mbona Mama hatafuti Mapenzi au kupendwa na watoto zake wa kike?
Jibu nilishasema huko juu kuwa, mwanaume ndiye mwenye kutoa Upendo.

Mwanamke hawezi kuupata upendo Kwa mwanamke mwenzake isipokuwa Kwa mwanaume tuu.

Ikiwa Mama akipendwa vizuri na mumewe kamwe hawezi ingilia mapenzi ya mtoto wake.
Hawezi kumuonea wivu Mke wa kijana wake,

Mkamwana akihudumiwa naye alihudumiwa
Mkamwana akipendwana kudekezwa mama hawezi jisikia vibaya Kwa sababu naye alipendwa na kudekezwa.

Taikon nimebaini kuwa Wamama wetu wengi wao walipitia maumivu makali mno kutoka Kwa Baba zetu. Hivyo hutaka Sisi tuwafute machozi.
Hili ni somo kwetu kuwa tunapaswa tuwapende wake zetu ili baadaye wasije wakavamia ndoa za watoto wao.

Ingawaje wapo Wamama wachache ambao walipendwa na waume zao na bado wanataka kupendwa na watoto. Ila hawa ni wachache Mno. Wengi WA wamama Gubu na wivu wao wanaoupeleka Kwa familia za watoto wao wakiume ni matokeo ya kukosa kwao upendo Kwa waume zao(Baba zetu).

Kumbuka; Mwanamke hapati mapenzi ya kweli kutoka Kwa mwanamke mwenzake isipokuwa mwanaume, iwe Baba yake, mume wake au mtoto wake wa Kiume.
Akikosa hapo basi atapata Kwa mchepuko wake.

Zingatia; Mwanaume ndiye mwenye Kupenda na Hilo wanawake wote wanalijua.
Kupenda ni Kutoa Huduma pasipo kutegemea kurudishiwa.

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Unaongeaga ukweli
 
Back
Top Bottom