Mwanamke akiamua kulipiza kisasi, ni kisasi hicho!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke akiamua kulipiza kisasi, ni kisasi hicho!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 16, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna msemo katika Kiingereza kuwa kuzimu hakuna moto mkali kama mwanamke mwenye kuwaka moto (hell has no fury like woman scotched!) Kimsingi msemo huu unatuambia kuwa mapenzi ya mwanamke yakigeuka hasira ni hasira hiyo. Hasira hiyo inaweza kumfanya mwanamke afanye kitu kibaya ambacho ikisimuliwa kuwa ni mwanamke amekifanya huwezi kuamini. Na anaweza akakifanya kikiwa kimepangwa vizuri sana (methodical) lakini pia kibaya sana (brutal).

  Kesi moja ambayo naikumbuka zamani sana ni ile ya mwanamke mmoja huko mikoani ambaye baada ya kuchoshwa sana na vitendo vya mumewe vya ulevi, unyanyasaji na matumizi ya nguvu siku moja aliamua kulimaliza hilo. Alimsubiri ametoka kwenye ulevi wake alipoingia ndani mwanamme alianza kumtukana na kumsema lakini mwanamke alikuwa mkimya wala hajibu. Mwanamme akajilaza kwenye kochi na kupitiwa na usingizi. Mwanamke alikuwa anachemsha mafuta ya kupikia kwenye sufuria... akayachukua mafuta yale na kummiminia mwanamke aliyekuwa amelala chali mdomo wazi.... mwanamke akauburua mwili na kuuweka kwenye gari lao la landrover, na yeye mwenyewe akarudi kwenda kulala; usingizi mtamu!!

  Katika simulizi la Majeruhi wa Mapenzi.. ninadokeza upande mwingine wa mwanamke aliyeumizwa anapoamua kufanya kisasi. Kutokana na kitabu hiki kupendwa na kusomwa kila kona ya dunia sasa (kuanzia Ujerumani, Marekani, Australia, Uingereza, TZ na kwingine) tumeweza kwenda kwenye chapisho la pili nakala chache wakati nikiendelea na toleo jipya la "Kumbatio la Mwenye Makosa" (extended version) na lile simulizi linalosubiriwa kwa hamu la "Uso kwa Uso na Kamanda".

  Mwanamme yeyote atajikuta anafanya makosa makubwa sana akifikiria upendo wa mwanamke hauwezi kugeuka chuki; na ukigeuka chuki shetani mwenyewe hujikunyata na kuziba macho yake! Na mwanamke akiamua kulipiza kisasi moto wa radi hauunguzi kushinda!

  UKITAKA KUPATA NAKALA YAKO SASA MLIMANI CITY, QUALITY CENTER NA SAMORA AVENUE PAMOJA NA MADUKA MENGINE YA SCHOLASTIC TZ... BONYEZA HAPA.

  Unajua kisa cha mwanamke aliyeamua kulipiza kisasi?
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hell has no fury like a woman scorned
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  right on thanks.. meant scorned..!
   
 4. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  I was once that woman (scorned) the hell i unleashed hadi leo anaisoma namba inaitwa mateso bila chuki lakini sijafikia calibre za Erica Tossi....yule mdada ni balaa
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa mkuu tulioko rural areas tunakipata vipi?
   
 6. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji hapo kwenye Mwanamke aliyekuwa amelala mdomo wazi ungebadili pawe mwanamme
  Pia nakueleza Mwanamke ni Binadamu mvumilivu sana na anasamehe kuliko Mwanamme, wanawakimbia Hivi ingekuwa tunazaa sisi Wanaume au tunapeana zamu ingekuwaje?
  Musoma mapenzi.jpg Huyo Mume kamcharanga na bado Bibie anadai anmpenda mumewe siku hiyo ilikuwa NI POMBE TU Mahakama imsamehe
  Hicho kitabu Mzee Mwanakijiji na sisi tutumie huku Bara
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ooh pole sana; tatizo wanaume tunaonesha tofauti sana maumivu ya moyoni...
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Rural ya wapi Ciello? maana mahali popote Tanzania ambapo magazeti yanaweza kufika basi kitabu hiki kinaweza kukufikia...
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kweli, nadhani kwa asili kuna u-serial killer kwenye hasira ya mwanamke.
   
Loading...