Mwanamke ajifungua jiwe!

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Baada ya kubeba mimba kwa miezi 11, hatimae jana, mwanamke huyo mkazi wa mkoani Mara amejifungua jiwe. Anasema tumbo lilikuwa likimuuma sana na alifurahi kupata uchungu akitegemea kupata mtoto wake wa kwanza. Mwenyekiti wa kijiji anachotoka mwanamke huyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema ni kweli limetokea na mama huyo amejifungua jiwe la uzito wa robo kilo!
Source: Matukio - RFA.

Kweli dunia imekaribia ukingoni....!!?

Hii habari ni uzushi tuwekee jina la huyo Mwanamke au picha yake pamoja na hilo jiwe

Mkuu,
Mimi nimesikia kwenye kipindi cha matukio cha Redio Free Afrika asubuhi hii. Nimepatwa na mshtuko baada ya kusikia maana ni ngumu kuamini. Sikuweza kusikia jina la huyo mama ila kama kuna ambaye kasikia atatujuza. Kuhusu picha, siwezi kuzipata maana sikuwepo huko na redio haitoi picha. Aliyeripoti redioni amemuhoji huyo mama na m/kiti wa kijiji chake na wote wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo!

Hapana! Haiwezekani! Science inagoma kabisa,othorwise kuna mazingaombwe hapo. Chromozome za binadamu haziwezi kucross na kuleta kitu kama hicho.Mazingaobwe hayo!

Jiwe limezaliwa siku ya eid!, hebu tuwekee photo bana tuone kama halin yale mmaandishi yetu.

huyu mama hakuwahi kwenda clinic? je alisharuiwa nini na madaktari hasa wakati tumbo linamuuma sana- majibu ya utra -sound yalionyesha nini?

Hapana! Haiwezekani! Science inagoma kabisa,othorwise kuna mazingaombwe hapo. Chromozome za binadamu haziwezi kucross na kuleta kitu kama hicho.Mazingaobwe hayo!

HUjui pia kuwa kuna science ya asili...nenda mikoa fulani ukimpa mtoto wa watu mimba na ukagoma wanakuhamishia wewe...tembea uone

huyu mama hakuwahi kwenda clinic? je alisharuiwa nini na madaktari hasa wakati tumbo linamuuma sana- majibu ya utra -sound yalionyesha nini?

Ni zahanati ya kijiji kipi chochote unachokifahamu ina huduma ya ultra sound? Au tunadhani watz wote wana access huduma za afya kama mlioko mjini?

huyu mama hakuwahi kwenda clinic? je alisharuiwa nini na madaktari hasa wakati tumbo linamuuma sana- majibu ya utra -sound yalionyesha nini?
mkuu, mama wa kijijini uswekeni kabisa, ambapo kituo cha afya kipo 19Km na hakuna usafiri, kituo cha afya kina clinical officer mmoja na nesi mmoja.
Hiyo ultra sound inatoka wapi?

mkuu, mama wa kijijini uswekeni kabisa, ambapo kituo cha afya kipo 19Km na hakuna usafiri, kituo cha afya kina clinical officer mmoja na nesi mmoja.

Hiyo ultra sound inatoka wapi?

MASHAKA MATUPU

Back
Top Bottom