Mwanamke Afungwa Jela ya Wanaume Kwa Miezi Sita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke Afungwa Jela ya Wanaume Kwa Miezi Sita

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by major mkandala, Mar 23, 2010.

 1. m

  major mkandala Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanamke Afungwa Jela ya Wanaume Kwa Miezi Sita
  [​IMG]
  Tuesday, March 23, 2010 3:15 AM
  Skendo limeikumba kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini ambapo mwanamke aliyakamatwa kwa makosa ya ujambazi anadaiwa kufungwa kwenye jela ya wanaume kwa kipindi cha miezi sita na kupelekea mwanamke huyo abakwe na kulawitiwa na wafungwa wa kiume.Denise Wilson au maarufu kwa jina la Abbah wa mji wa Isipingo nchini Afrika Kusini amekifungulia mashtaka kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini kwa kumweka kwenye jela ya wanaume kwa miezi sita wakati alipokuwa akisubiria kufikishwa mahakamani kwa makosa ya ujambazi, kujaribu kuua na kuteka watu.

  Denise anadai fidia ya rand 100,000 kwa madhila aliyoyapata wakati alipokuwa kwenye jela ya wanaume.

  Katika nyaraka za mahakama, Denise alisema kuwa alikamatwa septemba 24 mwaka 2002 na kupelekwa kwenye jela ya wanaume.

  Alisema kuwa kitendo chake cha kupinga kuwekwa jela moja na wanaume kilisababisha avuliwe nguo mbele ya wanaume huku akizomewa na kuchekwa.

  Wakati wa kipindi chake cha miezi sita kwenye jela ya wanaume, Denise anadai kuwa walinzi wa jela walikuwa wakimlazimisha afanye matendo ya ngono bila ya idhini yake.

  Alidai pia kuwa wafungwa wa kiume walikuwa wakimpapasa mara kwa mara kwenye sehemu zake za siri bila ya idhini yake.

  Denise pia hakusita kusema kuwa alibakwa na kulawitiwa katika kipindi cha miezi sita kwenye jela ya wanaume.

  Alisema kuwa ingawa maafisa wa jela walikuwa wakijua kuwa yeye ni mwanamke, waliendelea kumweka jela moja pamoja na wanaume.

  Alisema kuwa hata daktari wa wilaya alipomfanyia uchunguzi wa kuthibitisha jinsia yake, aliendelea kuwekwa kwenye jela hiyo.

  Kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini kimeamua kukaa kimya kikisubiria kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,111
  Likes Received: 3,031
  Trophy Points: 280
  hawakumtendea haki....unyama mkubwa sana huo
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...huwezi jua bana, labda naye ni 'semenya' mwingine, na hasa hayo makosa yake yenye muelekeo wa matendo ya kiume.
  BTW, kitengo ni kwa ajili ya kurekebisha tabia, inaonekana 'lengo' limetimia.
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Itakuwa ana mushkeri ndio maana wakashindwaa wamuweke wapi!!hata daktari alichemsha hahaha duniani kuna mambooo!!
   
 5. m

  major mkandala Member

  #5
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu atakuwa alikuwa ana kamchezo mchafu kwa wenzake wakaamua kumpa real pic wamwangalie atafanyaje
   
 6. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Teh Teh Teh Teh, No Comment
   
 7. Sydney

  Sydney Senior Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini ni lazima tuelewe kuwa yule bado ni binaadamu kama sisi na ana haki, waliomuweka jela ya pamoja na wanaume wataambulia walichokuwa wanakitaka, lakini humu JF nawaombeni jamani tusimuone kakosea saaaaana kwa vitendo vyake hatujui yaliyokuwa yanamsibu jamani, plz MBU, MAJOR MKANDALA please jamani ubinaadamu kwanza!
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Vitendo vyake ndio vilisababisha yote hayo.. sasa hana wa kumlaumu.
   
 9. T

  Tall JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kuna baadhi ya binadamu huwahukumu wenzao kuwa wana hatia hata kabla
  ya mahakama kufanya hivyo.nina imani atapata haki yake
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  :eek: ???
  ...am speechless na hizi tafsiri za "Human Rights!" ungeniambia ni mtuhumiwa i.e Innocent until proven Guilty, kidogo ningekuelewa!
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hata kama alitenda kosa gani hakutakiwa kuwekwa jela moja na wanaume!! Haki za binadamu zichukue mkondo wake na asilimia mia moja hiyo kesi atashinda. Kila mtu ahukumiwe kwa kosa lake, after all she is innocent until proves otherwise!!! Huyo Bwana jela ajiandae!!!
   
 12. e

  engels29t New Member

  #12
  Mar 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli hii si haki. Waliofanya kitendo hiki wanapaswa kuwajibika. Everybody's rights should always be respected.
   
 13. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,023
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ukifanya kazi ya kiume lazima uchangamane na NYAMAUME sioni tatizo la yeye kuwekwa kundi moja na hao aliowekwa nao kwani hata akiwa uraiani anchangamana nao kazini. Huku ndiko kurekebisha tabia; sidhani kama atarudia tena ubaradhuli wake
   
Loading...