Mwanamke afariki kwa kuliwa na nguruwe wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,265
Mwanamke mmoja nchini Urusi ameauawa na nguruwe aliokuwa anawafuga baada ya kuanguka kwenye banda la wanyama hao.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Urusi, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 56 alikuwa akiwalisha nguruwe ndipo ghafla akaanguka na nguruwe hao wakamtafuna.

Inasadikiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwake ilikuwa ni kuzirai ama kupatwa na kifafa.

Tukio hilo limeripotiwa kwenye wilaya Malopurginsky jimboni Udmurtia, lililopo katikati ya Urusi.

Vyombo vya habari vya urusi vinaarifu kuwa mume wa marehemu alikuwa amelala wakati mkewe alipokuwa akiwahudumia nguruwe hao. Bwana huyo inasemekana alikuwa mgonjwa.

Baada ya kuamka alianza kumtafuta mkewe na kukuta mwili wake ndani ya banda la nguruwe.

Inataarifiwa kuwa alifariki baada ya kupoteza damu nyingi. Tayari upelelezi jwa polisi juu ya tukio hilo umeshafunguliwa. Media reports say an investigation into the incident has been launched.

Oktoba mwaka 2012 tukio kama hilo liliripoptiwa nchini Marekani katika jimbo la Oregon. Bwana Terry Vance Garner, aliyekuwa na miaka 69 wakati huo alienda kuwalisha nguruwe wake lakini hakurejea.

Baadae, familia yake ilikuta mabaki ya mwili wake kwenye banda la nguruwe huku sehemu kubwa ya mwili huo ikiwa imeshaliwa na wanyama hao.

Mamlaka za eneo hilo ziliripoti kuwa mmoja wa nguruwe hao hapo awali alishawahi kumng'ata marehemu lakini aliweza kujinasua.

Kaka wa bwana huyo, Michael, alidai kuwa nguruwe hao walishawahi kujaribu kumtafuna na yeye na bwana Garner aliahidi kuliua dume kubwa ambalo ndio lilikuwa tishio zaidi.

Hata hivyo, baadae alibadili mawazo na kuendelea kuwafuga mpaka pale walipomuua.

Bbc
 
Ndo maana ni mnyama haramu kwa mjibu wa Imaani za Dini zingine, angefunga ngombe hata agezirai wiki nzima wasinge mla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Mungu gani kasema nguruwe ni haramu? Ingekua haramu isingeumbwa.

Alafu mmenikumbusha ngoja nipige simu niweke oda ya kitimoto!! Wekend leo..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ya Walawi 11:7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

Kumbukumbu la Torati 14:8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
 
Yesu aliua iyo mistari maana alisema kinachoingia mwilini akiwezi kumnajisi mtu. Bali kimtokacho mtu, maana hutoka moyoni mwake...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo ya Walawi 11:7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

Kumbukumbu la Torati 14:8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
sasa huo uharamu si ni kwa wewe unayeamini hilo andiko,,kwanini mnataka wote waamini hivyo.
 
Ni kweli kabisa ni Kwa wanaoamini tu Maandiko Matakatifu ya Mwenyezi Mungu muumbaji wa mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo sio kwa wote
Hivyo basi kwa wasioamini sio haramu.
 
Mambo ya Walawi 11:7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

Kumbukumbu la Torati 14:8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
Marko 7:14--23
 
Back
Top Bottom