Mwanamke Abadilishana Watoto Wawili Kwa Kasuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke Abadilishana Watoto Wawili Kwa Kasuku

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ametupwa jela miezi 30 na kufanyishwa kazi ngumu baada ya kukiri kubadilishana watoto wawili kwa ndege aina ya Kasuku Kishungi. Donna Louise Greenwell mwenye umri wa miaka 52 alipatikana na hatia ya kufanya biashara ya kuuza watoto wawili kwa kubadilishana kwa ndege aina ya Kockatoo (Kasuku Kishungi) pamoja na pesa dola 175.

  Donna amehukumiwa kwenda jela miaka 15 pamoja kazi ngumu kwa kila kosa moja alilokiri la kuuza watoto na ataanza kutumikia adhabu yake machi 25 mwaka huu.

  Donna anatuhumiwa kuwauza watoto wawili mmoja wa kike mwenye umri wa miaka minne na mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka mitano.

  Donna aliwauza watoto hao baada ya kukubali kupokea malipo ya kasuku kishungi mmoja na pesa kiasi cha dola 175.

  Watoto hao walikuwa si wa Donna. Wazazi halisi wa watoto hao walimuachia Donna watoto hao awalee.
   
Loading...