Mwanamitindo nguli Flaviana Matata hatimae amekiri kutalikiana na aliyekuwa mume wake

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,748
2,436
Katika mtandao wa kijamii wa Instagram, mwanamitindo, mwanaharakati ambae pia ni mfanyabiashara Flaviana Matata ameonekana kukiri ndoa yake ilikwishavunjika. Mara nyingi watu wamekua wakijiuliza kwanini haonekani na mume wake, wengine wakiuliza alipo mumewe.

Ni wazi kwamba ndoa nyingi za mastar ulimwenguni hua hazidumu, hivi tatizo hua ni nini haswa??

Kwa upande wa huyu mlimbwende wetu Flaviana Matata, je kuishi mbali na mume muda mrefu ndo kulipelekea ndoa kuvunjika??

Huyo mume wake yupo wapi kwa Sasa?? Je amekwishaoa?

LAVY_MARRIAGE.jpg


Screen Shot 2021-11-17 at 17.13.29.png

 
Hata ndoa za mtaani nyingi hazidumu ni vile tu hazipo kwa spotlight.

Kuna haja ya wanaume kupewa mafunzo kama wanavyosisitizwa wanawake.

Na kuna haja ya watu kuacha kuoana ili tu kuonekana wameolewa na kuoa.

Mwisho ndoa ikiwa ngumu mnaachana tu, sio kila ndoa lazima idumu
 
Ndoa zina kanuni constant milele, hakuna namna inaweza kubadilisha hiyo asili.

Watu maarufu na wenye kipato huwa wanajichanganya na kuja na kanuni nyingine kwenye ndoa zao,wanapoteza kimoja wapo.

Umeolewa usiku uko kwenye event za kibiashara na watu wengine.

Umeolewa jamaa anakula peke yake mgahawani au home peke yake.

Umeolewa watoto na mume wanahudumiwa na wasaidizi wa kazi.

Kuwa mke wa mtu ni fani nyingine ambayo inahitaji muda maalum kwenye maisha ya mwanamke sio sehem tu ya muda wake.
 
Ndoa nyingi siku hizi zimekua hazidumu

Nina mtu wangu wa karibu alioa ndoa yake ilidumu wiki2 na nusu tuu, tena wanandoa walifahamiana kwa miaka6 na walikua marafiki wazuri tuu.

Flaviana analo lililomkuta jamani, hapa analaumiwa sababu tuu ya umaarufu wake.
 
Yaani sijui kwa nini watu kenye ndoa waki achana wanawake ndio hulalamika, ila wanaume kimya na unaweza kuta hawana kosa hata kidogo ila wameamua kuya hifadhi.
Kuongea ongea sio hulka ya wanaume. Psychology ya wanawake na wanaume ni tofauti kabisa, jielimishe. Halafu dada hajalalamika kaweka wazi tu kitu ambacho hajawahi weka wazi mitandaoni
 
Flaviana analo lililomkuta jamani, hapa analaumiwa sababu tuu ya umaarufu wake.

Huyu hakuwa material ya kuolewa na DEO MASSAWE kwani alishatumika sana na wale promoters wake!! Kuolewa ilikuwa kutoa GUNDU basi!!! Huyu aliyekuwa mumewe anaendelea na maisha yake huko Marekani; aliwahi kuishi Seattle nadhani sasa anaweza kuwa Atlanta.

Hawa models mara zote ni high class prostitutes!!
 
Hayo ni maneno ya Adele ,,,na si kwamba Flaviana ndo kayasema kwa maana hiyo Flaviano ameya koti maneno aliyoyasema Adele
Kumbuka Adele nae ni Mwanamke, mimi sija mzungumzia mtu bali nime izungumzia jinsia kiujumla, wewe fuatilia sana pindi wana ndoa wanapo achana, mara nyingi wanaume ndio tunaonekana tuna makosa,labda sababu ya ukimya wetu ndio unatufanya tuonekane tuna makosa.
 
Kuongea ongea sio hulka ya wanaume. Psychology ya wanawake na wanaume ni tofauti kabisa, jielimishe. Halafu dada hajalalamika kaweka wazi tu kitu ambacho hajawahi weka wazi mitandaoni
Sasa ni jieleimishe nini wakati naijua reality na baadhi watu wangu wa karibu wana yaishi haya.

Sijui labda kwa uelewa wako ww umeelewa nini.
Screenshot_20211117-111139_Instagram.jpg
 
Huyu hakuwa material ya kuolewa na MASSAWE kwani alishatumika sana na wale promoters wake!! Kuolewa ilikuwa kutoa GUNDU basi!!! Huyu aliyekuwa mumewe anaendelea na maisha yake huko Marekani; aliwahi kuishi Seattle nadhani sasa anaweza kuwa Atlanta.

Hawa models mara zote ni high class prostitutes!!

IFIKE MAHALA TUWE NA MAWAZO MAZURI PALE AMBAPO HATUNA SABABU YA KUMCHAFU MTU BILA USHAHIDI

Umeamua kumbebea bango na kumhukumu flavy kuwa mkosaji lakini hujatuambia

Huyo Massawe unayemtete unajua mambo yake ya ndani?

Hayo ya kutumika sana na promota wake umeyapimaje? Je, hadi kuamua kumuoa huyo Massawe yeye hakuwa anayajua?? Unaposema hakuwa wife material kwani Vigezo vyako vya mwanamke kuwa wife material kwako ndio vigezo vya kila mwanaume??

Unasema models mara zote ni highclass prostitutes, kwa hiyo prostitutes wote wa high class ni models🙄🙄
 
Aisee kumbe flavy ametalikiana miaka 3 iliyopita!?? Anyway mtu ambaye anaweza kunipa mawasiliano ya flaviana matata, kuna laki Moja yake hapa. Msisitizo nahitaji mawasiliano tu siyo kunikuwadia,nitamtongoza mwenyewe na nitaoana naye tukiafikiana! Laki Moja ipo hapa mwenye mawasiliano ya flavy...
 
Hata ndoa za mtaani nyingi hazidumu ni vile tu hazipo kwa spotlight.
Kuna haja ya wanaume kupewa mafunzo kama wanavyosisitizwa wanawake.
Na kuna haja ya watu kuacha kuoana ili tu kuonekana wameolewa na kuoa.
Mwisho ndoa ikiwa ngumu mnaachana tu, sio kila ndoa lazima idumu
Tuache kuangalia mambo ya kujenga ndoa tuangalie mambo ya kuidhoofisha. Wewe haujitambui.

Kwanza umeolewa maana wanawake mkishaharibu mnataka na wenzenu waharibu ili muwe wengi mjisikie vizuri kuishi kinungayembe.....


Wewe umeolewa upo ndani ya ndoa if no then jua huwezi comment mazuri kuhusu ndoa coz ipo wazi wanawake ambao umri wa kuchumbiwa umewatupa mkono, au ambao mshaharibu mazingira ya kuwa na vigezo vyakuwa mke wa mtu mnakuwa na kisirani na wanawake wenzenu ambao wapo katika nafasi nzuri kupata ndoa ili kuwashawishi waharibu wafeli kama ninyi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom