Mwanamieleka wa Sumo Ainyofoa ATM na Kukimbia Nayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamieleka wa Sumo Ainyofoa ATM na Kukimbia Nayo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,683
  Likes Received: 4,716
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mwanamieleka wa Sumo wa nchini Urusi ametiwa mbaroni baada ya kuinyofoa mashine ya kutolea fedha toka kwenye ukuta wa duka moja nchini humo na kisha kuibeba mabegani na kukimbia nayo. Mwanamieleka wa mchezo wa Sumo wa nchini Urusi ametiwa mbaroni baada ya kuing'oa mashine ya kutolea fedha toka kwenye ukuta wa duka moja mjini Moscow na kisha kuanza kukimbia nayo.

  Polisi wa nchini Urusi walisema kuwa mwanamieleka huyo baada ya kuing'oa mashine hiyo yenye uzito wa kilo 90, aliiweka mabegani na kuanza kukimbia nayo.

  Polisi waliendelea kusema kuwa mwanamieleka huyo alifika kwenye eneo la tukio akiwa na wenzake wawili na kuing'oa mashine hiyo iliyokuwa na kiasi cha pesa za kirusi roubles 25,000 sawa na Tsh. Milioni 1.2.

  Mfanyakazi wa duka hilo aliyeshuhudia tukio hilo alipiga simu kuwaita polisi ambao waliwahi kufika na kuwakamata washirika wawili wa mwanamieleka huyo.

  Mwanamieleka huyo alikamatwa na kushikiliwa na polisi baada ya kukiri kosa lake.
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Du aliishiwa pesa ya vodka nadhani!
   
Loading...