Mwanamichezo mashuhuri Marekani abadili rangi ya ngozi yake awe Mzungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamichezo mashuhuri Marekani abadili rangi ya ngozi yake awe Mzungu

Discussion in 'Sports' started by GAMBLER, Jan 18, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Sammy Sosa alivyokuwa mwanzo na sasaMonday, January 18, 2010 4:58 AM
  Mmarekani mweusi Sammy Sosa ambaye aliwika sana enzi zake kwenye mchezo wa Baseball amebadili rangi ya ngozi yake kutoka nyeusi kuwa nyeupe kama mzungu.Mchezaji maarufu wa zamani wa Baseball, Sammy Sosa mwenye umri wa miaka 41 amejibadilisha rangi ya ngozi yake kuwa mweupe kama mzungu kwa kutumia krimu za kujichubua.

  Sosa alianza kujichubua kuanzia mwaka 2007 na wiki iliyopita alionekana kwenye tuzo za Latin Grammy jijini Las Vegas akiwa hana tena rangi yake nyeusi ya kuonyesha asili yake ya Afrika.

  Sosa alionekana mweupe kama mzungu na kwa watu ambao hawamfahamu ni vigumu kuamini alikuwa mweusi 'tii' zamani.

  Sosa amesema kuwa nia yake kubadili rangi ya ngozi yake ni kutokana na mapenzi yake mwenyewe na si kumuiga marehemu mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson.

  Sosa amekiri pia kubadilika kwa rangi hakutokani na maradhi yoyote ya ngozi bali ni kutokana na krimu anayoitumia ambayo alisema ataipigia kampeni za kibiashara.

  Hivi karibuni idadi ya watu weusi wanaojichubua nchini Marekani ili wakubalike katika soko la wazungu imezidi kuongezeka na wataalamu wa ngozi wanaonya kuwa matumizi ya krimu kujichubua ni hatari kwa afya.

  Magonjwa mengi ya ngozi kama vile kansa ya ngozi yamekuwa yakihusishwa na madawa na krimu za kujichubua.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  MWache aende zake, simtofautishi huyu na wale wanaobadili jinsia zao... too bad hawezi kurudi kwetu tena..

  Many of them huwa ni matunda ya abuse wakiwa wadogo
   
 3. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wale wale tu. Aende zake kule bana...
   
 5. K

  Kasanga Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu atakufa muda sio mrefu! amuulize Michael Jackson kuhusu kupenda kuwa mzungu!
   
Loading...