Mwanamfalme wa Saudi Arabia ni Saddam Hussein mpya mashariki ya kati

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Imeonekana wazi ikiwa mwanamfalme Mohamed Bin Salman akaukwaa ufalme wa Saud Arabia kuna hatari mashariki ya kati kupata dikteta mbaya zaidi ya aliyekuwa Rais wa Iraq Saddam Hussein.
Mwanamfalme huo mwenye umri wa miaka 32 ameonyesha ukatili mbaya kwa vita vya Yemen ambapo mamilioni ya raia wameuwawa kinyama, kuua wapinzani na wanaharakati nchini Saudi Arabia,kutaka kuivamia Qatar na kuhusika kwake na mauuaji ya kikatili ya mwandishi wa habari Khashoghi katika ubalozi wa Saudi Arabia nchini Turkey.
Je ikiwa huyu mwanamfalme akiwa Mfalme wa Saudi Arabia dunia itegemee nini ?

Saudi crown prince's 'reformer' image fading amid Khashoggi crisis

 
Ategemee kuondolewa mamlakani kwa muda mchache Sana. Hafikishi hata miaka kumi.
Wakumtoa unafikiri atakua nani? Wapinzani wake ndani ya ufalme?,nchi za magharibi? Au mahasimu wa kikanda kama Iran,Qatar na kwa mbali Uturuki wakisaidia uasi ndani ya Saudia(Kama uasi utaibuka)?
 
Wote uliowataja inawezekana
Wakumtoa unafikiri atakua nani? Wapinzani wake ndani ya ufalme?,nchi za magharibi? Au mahasimu wa kikanda kama Iran,Qatar na kwa mbali Uturuki wakisaidia uasi ndani ya Saudia(Kama uasi utaibuka)?
 
Marekani,Uturuki na wengine bado wanatafuta ushahidi kuthibitisha uhusika wa Saudia. Jambo la kufurahisha mashia wa manzese tayari wao washapata ushahidi na tayari washatoa hukumu
Kwanini wachinje mtu kinyama halafu lawama kwa washia kama sio kuwa na IQ ndogo
 
Kwa hiyo hiyo ripoti ya NY Times ndio ushahidi?
Umejiuliza kwanini wapelelezi wa Uturuki jana walikwenda kupeleleza nyumbani kwa balozi mdogo wa Saudia?
CCTV%20video%20made%20available%20through%20Turkish%20Newspaper%20Sabah%20allegedly%20shows%2...jpeg
 
Back
Top Bottom