Mwanamama tajiri Oprah alipata mimba akiwa na miaka 14

Unataka tupate ujumbe gani kwa hii story ya huyu mama ukizingatia zama tuliyonayo ya JPM kuhusu wanafunzi watakaopewa ujauzito shuleni.

kupata mimba haimaanishi kutoendelea shule bali atasoma shule binafsi sio za serikali.

natoka hapa umemwelewa DADDYNOLAN na mleta mada kwamba kuna fursa nyingi maishani, kwa mfano wake Oprah.

Ni sahihi kwa Rais kuzuia mabinti wadogo kupata mimba wasiendelee na masomo katika shule za Serikali. Wao badala ya kuzingatia masomo wamechagua maisha ya ndoa. Kuruhusu mimba za mabinti wa shule ni budi kwanza tuondoe sheria ya ndoa za utotoni.

Historia ya Oprah inatoa funzo kuwa hakuna kukata tamaa maishani, kwani kuna fursa nyingi tu.

Kuna stori imetolewa leo kanisani. Kwamba Panya kwa kuwa anamwogopa Paka alipenda kuwa Paka. Akaenda kwa mganga wa mazingaombwe (magician) amgeuze kuwa Paka na akabadilishwa kuwa Paka.

Alipokuwa Paka aliwindwa sana na Mbwa, hivyo akarudi kwa mganga abadilishwe kuwa Mbwa. Akabadilishwa kuwa mbwa.

Woga wake haukupata jibu kwa kubadilishwa kuwa Mbwa kwa kuwa kulikuwa na nyoka Chatu aliyemwinda. Hivyo, akarudi kwa mganga kubadilishwa kuwa Chatu.

Hilo la kubadilishwa kuwa Chatu alikuwa suluhisho la woga wake. Zamu hii aliwindwa sana na binadamu. Alirudi tena kwa Mganga abadilishwe kuwa binadamu. Alivyorudi kwa Mganga, aliambiwa hakuna jinsi ila kumrudisha katika hali yake ya zamani kuwa Panya na aikubali hali yake hiyo.

Funzo hapa ni kwamba binadamu tusisukumwe na woga kukabili kila hali (nzuri/mbaya au rahisi/ngumu), katika maisha yetu. Mabinti wanaochagua kuwa wamama, waendelea na maisha hayo na kuzitumia fursa zilizopo.
 
Na hili nalo litapita ila ndo Mh ashasema, hasomeshi wazazi of which binafsi namuunga mkono!!
 
Watoto wa sasa hv ni tukutu mnooo...mimba zikiruhusiwa wanazidisha jeuri na ujinga...bora wapigwe biti hivyo hivyo...
Ukiwakuta kwenye singeli wanakata mauno ....wacheza shoo hawaon ndani
 
Suala sio rais suala ni ujenzi wa jamii yenye maadili, hivi leo hii Magufuli asimame aseme mimba ruksa mashuleni hivi jamii yetu ya wasichana wa kiafrika umeisahau?
Huko shuleni kutasomeka tena?
Acheni kulaumu kwa kila jambo kisa aliyeko madarakani hampendi awepo
Na asingelizungumzia ikawa kama zamani jinsi ilivyokua angekufa?
 
Suala sio rais suala ni ujenzi wa jamii yenye maadili, hivi leo hii Magufuli asimame aseme mimba ruksa mashuleni hivi jamii yetu ya wasichana wa kiafrika umeisahau?
Huko shuleni kutasomeka tena?
Acheni kulaumu kwa kila jambo kisa aliyeko madarakani hampendi awepo
Maadili yanaanza na wewe mwenyewe kisha ndani ya familia yako, baadae ni kwenye jamii inayokuzunguka.
Alichokifanya "Pombe" ni sawa na kufunika Moshi usitoke wakati moto unawaka na kuteketeza kwa ndani. Jana kaalika wanyoa vuduku na wavaa milegezo Ikulu, je jamii yetu inaruhusu hayo? Au kuzuia mimba kwa maneno ndio kulinda maadili, ila kuruhusu wanaume kusuka na kunyoa vuduku ndio maadili?
 
natoka hapa umemwelewa DADDYNOLAN na mleta mada kwamba kuna fursa nyingi maishani, kwa mfano wake Oprah.

Ni sahihi kwa Rais kuzuia mabinti wadogo kupata mimba wasiendelee na masomo katika shule za Serikali. Wao badala ya kuzingatia masomo wamechagua maisha ya ndoa. Kuruhusu mimba za mabinti wa shule ni budi kwanza tuondoe sheria ya ndoa za utotoni.

Historia ya Oprah inatoa funzo kuwa hakuna kukata tamaa maishani, kwani kuna fursa nyingi tu.

Kuna stori imetolewa leo kanisani. Kwamba Panya kwa kuwa anamwogopa Paka alipenda kuwa Paka. Akaenda kwa mganga wa mazingaombwe (magician) amgeuze kuwa Paka na akabadilishwa kuwa Paka.

Alipokuwa Paka aliwindwa sana na Mbwa, hivyo akarudi kwa mganga abadilishwe kuwa Mbwa. Akabadilishwa kuwa mbwa.

Woga wake haukupata jibu kwa kubadilishwa kuwa Mbwa kwa kuwa kulikuwa na nyoka Chatu aliyemwinda. Hivyo, akarudi kwa mganga kubadilishwa kuwa Chatu.

Hilo la kubadilishwa kuwa Chatu alikuwa suluhisho la woga wake. Zamu hii aliwindwa sana na binadamu. Alirudi tena kwa Mganga abadilishwe kuwa binadamu. Alivyorudi kwa Mganga, aliambiwa hakuna jinsi ila kumrudisha katika hali yake ya zamani kuwa Panya na aikubali hali yake hiyo.

Funzo hapa ni kwamba binadamu tusisukumwe na woga kukabili kila hali (nzuri/mbaya au rahisi/ngumu), katika maisha yetu. Mabinti wanaochagua kuwa wamama, waendelea na maisha hayo na kuzitumia fursa zilizopo.
Umeandika kweli tupu kama elimu anaitaka atatafuta njia nyingine sio kurudi shule za serikali kuharibu watoto wengine kiakili hasara itakua kubwa kuliko faida
 
Hebu tujadili faida za hilo katazo tuone kama uamuzi huo utaondoa tatizo au ni kukimbia tatizo?
 
Back
Top Bottom