Serikali isiache kuhusishwa na Jaribio Dhidi ya Lissu; Ijisafishe!

Mwanakijiji umechambua vizuri sana nadhani mheshimiwa Raisi inabidi awe mkali kweli kwa vyombo vyake vya usalama awambie mimi na serikali tunachafuliwa sasa liwe jua iwe mvua nataka wahusika wafahamike na jamii itambue pasipo shaka kuwa hatuhusiki
 
FB_IMG_1504849970189.jpg
 
Yule mtu asiyefahamika aliyeonekana kwenye Camera za Clouds na watu waliobeba silaha na baadaye akatutabiria kuonekana kwa Roma kabla ya Jumapili aje atuambie na perpetrators wa hili wanapatikana lini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hili hata iweje sidhani kama serikali inaweza kujisafisha na ikaaminika kwa wananchi.

Mbaya zaidi ni kwamba kiongozi mwenyewe wa serikali, yaani rais Magufuli, ndiye yuko mstari wa mbele kuwafanya watu wasiiamini serikali yake kwa sababu ya nyingi ya kauli zake.

Laiti angekuwa yupo makini na maneno atumiayo labda walau kungewepo na nafasi ya kuaminiwa.

Lakini kwa sasa sidhani. Labda ambacho wanaweza kufanya ni kupunguza makali ya tuhuma hizo za kuhisiwa.

Ushahidi wa kimazingira dhidi ya uhusika wa serikali ni mwingi wa kutosha.

NB: Ni Jusa Mwaikusa au ni Jwani Mwaikusa..???
Jwani, nadhani mwandishi kateleza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wale viongozi wa CCM Kibiti unaongeleaje mkuu
Yote ni mipango,, naanza na kwangu ili nikija kwako waseme " hata yeye mbona,,,,,,,,,
Kwanza kilichofanyika ni aibu kubwa kwa taifa ingawa siwezi kuamini moja kwa moja kwamba serikali hapa inahusika. najaribu kurefer kwenye mabandiko ya The bold na bandiko la Nifar (
Ulimwengu mzima kiganjani mwa CIA)

Tanzania kwa sasa chini ya Rais Magufuli tuko kwenye vita hatari zaidi, vita vya kiuchumi sasa kwa kutumia makala ya the bold na Nifar nimeona ni vizuri tukatafakari tukio hili kwa upana wake badala ya kuelekeza moja kwa moja lawama au kutuhumu moja kwa moja serikali kwa kutumia logic ifuatayo.

1. Utawala wa Magufuli umegusa maslahi ya wakubwa ambayo kwa miaka mingi wanachuma kupitia raslimali zetu, jambo ambalo haliwezi kuwafurahisha na kuvumilia kuona Rais Magufuli anaendelea kusalia madarakani.

2. As long as magufuli ataendelea kuwa Rais, na ushawishi alionao katika kipindi kifupi baada ya kuingia madarakani na uwezekano wa kushindwa kwenye uchaguzi ujao kwa njia ya sanduku la kura kuwa mdogo

Yawezekana wakubwa hawa wanatumia mbinu zile zile walizowahi kuzitumia kuwaondoa watawala ambao walienda kinyume nao kwa kupanga matukio ambayo yanatengeneza chuki kwa wananchi dhidi ya utawala wao na hatimaye kuweka watawala vibaraka wa nchi zao.

Kwa nini Tundu Lissu, Logic ni simple, Tundu Lissu ndiye ameonyesha kwa kiwango kikubwa kupinga utawala wa Magufuli na ndiyo pekee anaweza kutumika mtaji wa uchonganishi kati ya wananchi na utawala wa Magufuli.

Wazungu hawa wameshikwa pabaya and they can do anything hasa kutumia hizo coincidence za ugomvi kati ya LISSU na utawala kuhakikisha wanendelea kutunyonya hata kwa kutoa uhai

Ni vizuri tukawa watulivu huku tukimuombea Lissu kupona na kumuomba Mungu awaumbue/amuumbue yeyote aliyefanya tendo hilo la kinyama huku tukijizuia kunyooshea serikali kidole bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Pitieni kidogo hiyo thread ya Nifar pengine inaweza kusaidia kujua namna mataifa makubwa yasivyopenda viongozi wa aina ya Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hili hata iweje sidhani kama serikali inaweza kujisafisha na ikaaminika kwa wananchi.

Mbaya zaidi ni kwamba kiongozi mwenyewe wa serikali, yaani rais Magufuli, ndiye yuko mstari wa mbele kuwafanya watu wasiiamini serikali yake kwa sababu ya nyingi ya kauli zake.

Laiti angekuwa yupo makini na maneno atumiayo labda walau kungewepo na nafasi ya kuaminiwa.

Lakini kwa sasa sidhani. Labda ambacho wanaweza kufanya ni kupunguza makali ya tuhuma hizo za kuhisiwa.

Ushahidi wa kimazingira dhidi ya uhusika wa serikali ni mwingi wa kutosha.

NB: Ni Jusa Mwaikusa au ni Jwani Mwaikusa..???
MKUU POST ZAKO UNAZIBALANCE VIZURI NAZIPENDA.
 
Kwanza napenda kumwombea Tundu Lissu Allah ampe afya njema. Naiomba serikali itumie kila aina ya Recourses kuhakikisha hawa watu wanatiwa nguvuni kwani huu ni ugaidi wa kuleta chuki dhidi ya serikali.
Utaletewa mazezeta wasioleweka kumbuka kisa cha Dr Ulimboka, Com Mawazo, Olasitti Arusha etc. Hawawezi kuleta suspect wa maana

Cairo's
 
Siyo maslahi ya Rais Magufuli kuonekana kama Rais ambaye ameanza kushindwa hoja za maneno na sasa serikali yake inataka kuingia kwenye hoja za damu.
wewe ni magufuli????? ngoja niishie hapa tu..mimi nina ki starlet...kikipigwa zile risasi kinawaka moto
 
Mwanakijiji unatetea haya ilihaji unajua kabisa hadi leo Ben hajulikani alipo..na serikali hii hii haisemi nini inafanya..mtu sio sindano ya kupotea potea tu
 
Kwanza kilichofanyika ni aibu kubwa kwa taifa ingawa siwezi kuamini moja kwa moja kwamba serikali hapa inahusika. najaribu kurefer kwenye mabandiko ya The bold na bandiko la Nifar (
Ulimwengu mzima kiganjani mwa CIA)

Tanzania kwa sasa chini ya Rais Magufuli tuko kwenye vita hatari zaidi, vita vya kiuchumi sasa kwa kutumia makala ya the bold na Nifar nimeona ni vizuri tukatafakari tukio hili kwa upana wake badala ya kuelekeza moja kwa moja lawama au kutuhumu moja kwa moja serikali kwa kutumia logic ifuatayo.

1. Utawala wa Magufuli umegusa maslahi ya wakubwa ambayo kwa miaka mingi wanachuma kupitia raslimali zetu, jambo ambalo haliwezi kuwafurahisha na kuvumilia kuona Rais Magufuli anaendelea kusalia madarakani.

2. As long as magufuli ataendelea kuwa Rais, na ushawishi alionao katika kipindi kifupi baada ya kuingia madarakani na uwezekano wa kushindwa kwenye uchaguzi ujao kwa njia ya sanduku la kura kuwa mdogo

Yawezekana wakubwa hawa wanatumia mbinu zile zile walizowahi kuzitumia kuwaondoa watawala ambao walienda kinyume nao kwa kupanga matukio ambayo yanatengeneza chuki kwa wananchi dhidi ya utawala wao na hatimaye kuweka watawala vibaraka wa nchi zao.

Kwa nini Tundu Lissu, Logic ni simple, Tundu Lissu ndiye ameonyesha kwa kiwango kikubwa kupinga utawala wa Magufuli na ndiyo pekee anaweza kutumika mtaji wa uchonganishi kati ya wananchi na utawala wa Magufuli.

Wazungu hawa wameshikwa pabaya and they can do anything hasa kutumia hizo coincidence za ugomvi kati ya LISSU na utawala kuhakikisha wanendelea kutunyonya hata kwa kutoa uhai

Ni vizuri tukawa watulivu huku tukimuombea Lissu kupona na kumuomba Mungu awaumbue/amuumbue yeyote aliyefanya tendo hilo la kinyama huku tukijizuia kunyooshea serikali kidole bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Pitieni kidogo hiyo thread ya Nifar pengine inaweza kusaidia kujua namna mataifa makubwa yasivyopenda viongozi wa aina ya Magufuli.

Hizi logic na assumption zako waweza kubaki nazo tu....

Anyway, tu - assume kuwa uko sawa. Then kwa nini wasimuue yeye mwenyewe huyo anayehatarisha maslahi ya mabepari?

Ama kwa nini wasimuue waziri mkuu wake?

Huyu bwana ni Iddi Amini wetu na hawezi kukwepa lawama hizi.....

Kwanza Jana wakati anapokea vijiripoti vyake vya almasi sijui na Tanzanite, wengi wetu tulishangaa sana kutomtaja Tundu Lissu kwenye kijihotuba chake akaishia kutoa kiji - flash na kutuhadadaa eti ameshanyonya taarifa za wazungu wawekezaji wote wa sekta ya madini na taarifa zao anazo long time....

Amini usiamini, huyu jamaa hafai kuwa kiongozi ktk nafasi aliyonayo.... haiwezi!!

Kama unatarajia makubwa chini ya Magufuli kwa Tanzania yako, rudi na anza kufikiri upya..... umepotea!!
 
Kauli za serikali zinajulikana , Mara kwa Mara imekuwa ikihubiri chuki kwa wapinzani na kuapa kuwashughulikia,na kweli shughuli ya Jana tumeiona ila hawajafanikiwa kumuua tu,hongera zao kwa hiyo shughuli
 
Na. M. M. Mwanakijiji
Ni muhimu pia kwa wananchi kuwa na utulivu na hekima ya kutafakari kwa kujiuliza swali la msingi hasa – ni nani angenufaika kama Lissu angeuawa? Huu ndio msingi wa uchunguzi. Japo wengi tayari wameshahitimisha kuwa “serikali inahusika” au kuwa ni “Magufuli”; kuna uwezekano mkubwa kuwa ambaye/ambao wangenufaika na Lissu kuuawa bila ya shaka siyo Magufuli. Ni maslahi ya Magufuli kuona kuwa Lissu hapatwi na janga kama kama hili. Wengine wanaweza kusema “vipi kama Magufuli hajali kama angenufaika au la?” Swali hili ni zito na jibu lake siyo rahisi lakini linaweza kufikirisha wengi.

Kuna watu huku mtaani wanahoji...kua Bashite huwa anakua na mzee katika shughuli zooote za kiki...kama kufungua mabweni, kuzindua bomba la mafuta,na riport za makinikia....lakini jana KWENYE RIPORT YA MAKINIKIA YA ALMASI BASHITE HAKUWEPO...je unaweza kutuulizia huko alikuwa wapi jana??
 
Back
Top Bottom