MwanaKJJ Ijumaa: Kati ya Makabila Yote Hili Litamsumbua Zaidi Magufuli

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,539
40,172
tunaweza.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli Watanzania tumejitahidi sana kujenga umoja bila kujali rangi, dini, asili na hata kwa kiasi kikubwa bila kujali makabila yetu. Makabila yetu mbalimbali yameweza kushirikiana katika mambo mbalimbali na kwa kweli pamoja na changamoto za hapa na pale bado tunaweza kusema kwa haki kabisa kuwa suala la ukabila nchini ni suala la mtu mmoja mmoja zaidi kuliko kundi zima. Hata hivyo, naomba kupendekeza kuwa hili kabila ninalolizungumzia leo tukubaliane sote kulipiga vita, na ikiwezakana kulibagua kwa nguvu zetu kwani ni tishio la mafanikio yetu kama taifa.

Kabila hili yawezekana ni kubwa kuliko makabila mengine; naamini kutokana na athari zake kwa taifa hadi hivi sasa na huko tunakoelekea kabila hili linapita makabila mengine yote. Kabila hili lina sifa nyingi; lakini sifa yake moja kubwa ni kwamba lina watu wake karibu kwenye nyanya na sekta mbalimbali – za binafsi na za umma, lina watu wa dini zote, lina watu wa jinsia zote na marika yote.

Ni kabila ambalo watu hawazaliwi ndani yake; ni kabila ambalo mtu unajiunga nalo kwa hiari. Na wengi wakishajiunga kutoka humo ni kazi sana. Kwani, hata wasome vipi, hata wafundishwe vipi watu walioko kwenye kabila hili ni vigumu kuachana nalo!

Kwa asili yao watu wa kabila hili ni wabishi; ni wabishi hata pale ambapo ukweli unawakodolea macho kama bundi! Ubishi wao unatokana na wao kuwa waumini watiifu wa kabila hili na hivyo kukubaliana na ukweli hata kama ni ukweli rahisi kukubalika kwao kunaweza kuwa ni tatizo.

Kabila hili ni lile la Wahatuwe! Ni Watanzania wenzetu ambao toka utoto hadi utu uzima wanaamini kabisa kuwa hakuna jambo ambalo sisi kama mtu mmoja mmoja tunaweza kufanyika vizuri na kufanikiwa na kuwa na ushindani ndani hata nje. Kabila hili haliamini kabisa kuwa tunaweza kuwa na timu nzuri za mpira na tukashindana na kuwa mabingwa siyo wa Afrika tu lakini hata kuweza kucheza kombe la dunia.

Wahatuwe wanaamini kabisa kuwa hakuna jambo lolote ambalo Mtanzania anaweza kulifanya likafanikiwa vizuri kabisa na kuwa la kiwango cha kukubalika hata kimataifa. Kwamba, akitaka jambo lake lifanikiwe au lifanyike vizuri bi lazima kwanza wawepo ‘wafadhili’ fulani fulani au wazungu. Na ukweli ni kuwa kabila hili linatukuza “uzungu” kuliko kitu kingine chochote. Hawa wakimuona mzungu wanafikiria ana mawazo bora kuliko wao; wakikaa na mzungu kwenye mkutano wanashindwa hata kumhoji au kumpinga kwani kumpinga “mzungu” kwao ni mwiko hata kama wanajua anachoongea ni utumbo!

Wahatuwe wana tabia moja mbaya – kama ilivyo kwa makabila mengine na tabia zao – tabia yao zaidi mbaya ambayo binafsi siipendi kabisa ni ile ya kujiona duni mbele ya wazungu na wageni wengine. Yaani unaweza kumkuta Mhatuwe ambaye amesoma Uhandisi na amesoma hadi shahada za juu kabisa lakini ukimuuliza akuandalie mpango wa kujenga kitu fulani atapata shida. Atahitaji mzungu fulani au mgeni fulani amsaidie.

Na ukimkuta Mhatuwe kwenye sehemu ya juu ya maamuzi utashangaa kuona kuwa hawaamini Watanzania wenzie. Haamini kama kuna kitu wanaweza kukifanya vizuri. Kiasi kwamba, hata kama wanakuja watu wawili wenye elimu na uzoefu sawa yeye yuko tayari kumpa kazi au mkataba yule mtu mgeni (hasa kama ni Mzungu) kwa vile vile tu haoni kama Mmatanzania mwenzie anaweza.

Chukulia kwa mfano suala la kuhamia Dodoma. Kama kuna wakati nimeona wingi wa watu kwenye kabila hili ni hili suala la kuhamia Dodoma. Sasa wapo ambao wanatoa maangalizo yanayostahili; kwamba utekelezaji huu ufikiriwe vizuri na isiwe kama kushindana kuonekana nani anaweza kuhamia Dodoma kwa haraka zaidi kabla ya 2020. Hawa Wahatuwe wao wanaona jambo hili haliwezekani. Haliwezekani kwa sababu wanaona tutaweza vipi wakati sisi hatuwezi?

Na hapa ndipo kabila la Wahatuwe linapojionesha; wao ni watu wa “Hatuwezi”; neno la kwanza vinywani mwao ni “haiwezekani” na linalofuatia ni “huwezi wewe”; na ukimsikiliza sana hatochelewa kusema “siwezi hili nahitaji msaada”. Kabila hili la Wasioweza linatusumbua sana.

Na kwa hakika litamsumbua sana Magufuli kwani kifikra watu wanaoamini kuwa hawawezi hata ukiwapa kitu watashindwa kwa sababu tayari fikra zao zimeshasema hatuwezi. Watu wanaenda kuchezi mechi na timu ya Misri, halafu moyoni wameshaambiana “hatuwezi kuwafunga Waarabu bana” na wanaenda kucheza na kufungwa na wanaamini kabisa wamefungwa kwa sababu “hawawezi”.

Ukiwaambia, tunaweza kushinda medali kwenye Olimpiki tukijiandaa vizuri wao wanaona kabisa kuwa “hawawezi”. Kumbe wanaenda huko nafikra za kushindwa na wanaposhindwa wanakuja na habari za “maandalizi zaidi” kumbe wakati mwingine matatizo yao yako kichwani kabisa.

Sasa Magufuli atapata shida na watu hawa kuliko wengine wote. Akisema tunaweza kuinua maisha yetu kwa haraka zaidi ndani ya miaka hii minne wao wanasema haiwezekani; akisema tunaweza kukusanya kodi zaidi wao hukimbilia kusema “haiwezekani”; akisema tunaweza kuinua viwanda vyetu utawasikia “haiwezekani” tena wanasema kwa majivuno na kebehi “Tanzania gani ya viwanda”! Akisema tunaweza wao wanasema “hatuwezi”.

Bahati mbaya sana ni kuwa hata watu wengine ambao hawakuwa kwenye kabila hili sasa hivi wanajiunga kwa hiari! Kabila la Wahatuwezi limeongeza na inaonekana limezidi kukua. Jambo pekee ambalo watu hawa wanaamini wanaweza kwa asilimia mia moja ni kusema hatuwezi.

Kabila hili ni la kulikataa, kulipinga na kulitenga kwani ni tishio la maendeleo. Watu wote walioendelea katika jamii za dunia ni wale ambao walisema “tunaweza”. Walisema tunaweza hata pale ambapo ilionekana haiwezekani na hakuna mwingine aliyewahi kufanya; walisema tunaweza na sasa wanakula matunda ya kujiamini huko.

Tukitaka kweli kushinda na mataifa mengi ya dunia ni lazima sisi wenyewe, wazazi, walimu, na jamii ikatae kurudia kiitikio cha “hatuwezi” na tuanze kusema “na sisi tunaweza” hata kama hatuoni kama tunaweza.

Na kipimo kizuri kwetu safari hii ni suala la Dodoma, je tunaweza kuujenga Mji Mkuu wa kisasa tukikusanya nguvu zetu, utaalamu na ujuzi wetu na uwezo wetu wote? Je, tunaweza ndani ya miaka hii michache kukamilisha mambo yale yote ambayo yamezuia kwa muda mrefu kuhamia Dodoma? Je, tunaweza kuufanya Dodoma kuwa mji wa kisasa, mdogo lakini wenye sifa za kimataifa kiasi cha kufanya uwe kama Kigali yetu na zaidi ya Kigali? Je, tunaweza kuufanya uwe mji ambao watu wakisema Dodoma watu wajue tunazungumzia Tanzania? Je, tunaweza kweli kulibadilisha taifa letu na kuinua maisha ya watu wetu kwa haraka zaidi kuliko taifa jingine lolote la Kiafrika ndani ya miaka hii mitano?

BInafsi naamini tunaweza kwani mimi niko kabila lile jingine, dogo lakini lenye matokeo – kabila la Watuna; Watunaweza! Ndugu zangu, haijalishi matatizo, haijalishi changamoto, haijalishi vikwazo; binadamu wenye akili timamu na uwezo na ujuzi wa kutosha tukiamua kufanya jambo kwa pamoja kushindwa basi isiwe sehemu ya mambo ya kutarajia (failure is not an option). NI lazima tufanikiwe kwa ajili yetu, na kwa ajili ya watoto wetu. Lakini zaidi pia ni kwa ajili ya watoto wa watoto wetu.

Tunaweza.

Niandikie: Mwanakijiji@zamampya.com
 
Umezunguka weee mwishoni umeonyesha rangi yako halisi...wewe wa kabila la tunaweza onyesha ni vipi tunaweza hamia Dodoma bila kuwa na bajeti katika hilo na vyanzo gani vya mapato vitafanikisha hilo na Tukajivunia Mji mkuu Dodoma kama tunavyoaminishwa..pengine ukinijibu Haya naweza badili kabila
 
Hilo kabila zuri sana linaangalia uwezo,na linajipa muda wa kutizama mambo kwa undani......na linaangalia historia....nashangaa pale mtu anakuambia naweza kwenda ulaya kuhubiri injili hata kama ,sina Viza na anaelekea uwanja wa ndege ..hawa ni kabila la Tunaweza...kusema tunaweza ni rahisi utekelezaji .....ni ngum sana......
 
Si useme kundi tu ijulikane? kabila maana yake nini?

Retardation ya kasi ya mwanga

Jpm mwenyewe ni kabila la wahatuwezi mbona nae anasema hatuwezi kuwa taifa omba omba hatuwezi kuwa taifa lenye kila kitu hewa watumishi barabara hatuwezi kuwa taifa linalofikisha walarushwa mahakamani halafu wanaachwa na dpp huyohuyo nk mwanakijiji mwenzi jpm ni mkemia wewe sijui una fani gani chunga kuamini vitu kwa kiswahili
 
Jamii ya WAHATUWE waliikimbia mama Tanzania wakaenda kuishi ughaibuni wakifanya kazi za kitwana kabisa yaani upagazi,kuogesha wazee na kuosha matairi ya magari.Kabila hili liliamini HALIWEZI kupigania maendeleo ya taifa wakiwa nyumbani wakaamua kwenda kuishi utumwani uhamishoni.Last year Musa ameenda huko utumwani ughaibuni na huenda akaliokoa kabila lake la Wahatuwe na kurejea nao hapa nyumbani kwenye utajiri wa rasilimali LUKUKI
 
MwanaKJJ,
Ushafanikiwa kujipa likizo kutoka huko kwa wadhungu kuja kusalimia nyumbani?
 
Muheshimiwa tangu uwe upande huo naona nawewe umeanza kuamini maendeleo ya mwendokasi,

Ngoja mi nijitafutie kabila langu la kati ya hayo mawili. Hili langu ni la tunaweza ikiwa tunamikakati na mipango thabiti. Usipojipanga kwa jambo lolote umejiandaa kufeli jambo hilo. Lazima tu~tanabaishe ni vitu gani tunataka kufanya? then tuweke mikakati ya ni namna gani tufanikishe kwa haraka? Halafu tuanze kutekeleza na organ zetu zote, kulala na kuamka kwetu kuendane na malengo hayo.
Mfano, bujet yetu iseme hivyo, sera zetu mbali mbali ziseme hivyo ndo hivyo tutafanikiwa.

Lakini kama kweli budget ilishapita, na kati ya fedha zilizopita ni pamoja na za ujenzi na ukarabati wa majengo mbali mbali ambayo yapo dar. Na baadaye mtu akafurahi saaaaaaaaana akiwa dodoma akaona wacha tuhamie huku. Nawatakia kila la heri katika hayo maendeleo ya mwendokasi.


Najua unajua lakini siku hizi umeanza kupepesa macho kwenye kusema ukweli.
 
Ukiwa CCCM unaweza sema chochote bila ya kujali kelele za Nzi ,kwa nini uzongwe nazo wakati una teargas!!?....

Tumeona vipaumbele vyenu namna mnavyo andamana na Lisu ,kuanzia mtukufu sana /msemaji wa Lumumb na Geshi ra porisi kwa vitendo ....Wanaosubiri Nchi ya viwanda wana moyo wa chuma ,Elimu bure tu imeshafeli na tunaona kasi ya kucangushwa madawati....
 
Kuna dalili ya kuchoka kifikra...nitoe angalizo si kila king'aacho ni almasi pengine ni kipande cha chupa..kuzunguka kote mwisho umerudi pale pale!Mda wote huo umepotea bure!!
 
ANC wanatumbuliwa sasa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
Zuma aliingia kwa mbwembwe kama huyu japo alikuwa na uzoefu kwenye chama,
Sijui itakuwaje kwa huyu mkuu yako!!
 
Back
Top Bottom