George Maige Nhigula Jr.
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 470
- 149
kinachonishangaza pia ni kuwa watu wameshindwa kusoma hiyo alama ya 'kuuliza' ambayo ilikuwepo kwenye makala tangu mwanzo na hawajajiuliza kwanini sikuiweka kama statement of fact. Mada nzima ni swali wala haitoji jibu lakini kwa anayelisoma hilo swali anapata jibu ndani yake. Lakini watu wamekuja juu na kufikiria nimesema CCM ni chama cha Waislamu na Chadema chama cha Wachagga. Wanasahau hata ufunguzi wa hoja yangu umewekwa kwenye misingi ipi: NImeanza hoja kwa kusema hivi:
Hivi ni gumu sana kujua maana ya kujenga hoja ya kimantiki na kuonesha ukweli kwa kutumia kuizungusha lugha?
Mzee Mwanakijiji,
Tatizo ni reading skills zetu sisi watanzania ziko chini sana, watu huwa hatusomi kwa weledi unaotakiwa na kujiridhisha kuwa mantiki ya hoja aliyo andika mwandishi ndo hiyo niliyoelewa?
Unajua tena watanzania hatujazoea kusoma makala zilizoandikwa kwa kumfikirisha msomaji na kuwa makini kuvumbua lengo la kimantiki la mwandishi, jamani tujaribu kuboresha our reading skills vile vile